Kamati ya fedha na uongozi manispaa ya Ubungo yaagiza kusimamishwa kazi waliohujumu na kula mapato ya Halmashauri

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI MANISPAA YA UBUNGO YAAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI WALIOHUJUMU NA KULA MAPATO YA HALMASHAURI

Kamati ya fedha na uongozi ya Tarehe 05 june 2018, imepokea Ripoti ya Ukaguzi maalumu wa Mapato yatokanayo na Masoko ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kutoka kwa mkaguzi wa ndani,

Ikiwa ni agizo la kikao cha Kilichoketi 13-04 -2018 kuagiza kufanyiwa kwa ukaguzi maalumu katika masoko yote ya Halamshauri baada ya Wajumbe katika kikao kutilia shaka taarifa ya mapato ya Halmashauri ya Mwezi March kushuka Sana,ambapo ilionyesha kiasi cha Tsh Millioni 716 ndicho pekee kilikuwa kimekusanywa katika Masoko yote 16 kwa Muda wa Miezi 9,

kitu ambacho kikao hicho hakikuafikiana na taarifa hiyo.Sababu Soko la Mabibo peke yake lilikuwa linakusanya kiasi cha Zaidi ya Tsh Millioni 100 kila Mwezi.

Ukaguzi huo uliofanywa na mkaguzi wa Ndani kwa kipindi cha tarehe 17 mpaka 25 Mwezi wa Nne 2018. Kwa Masoko ya Mabibo,Simu2000,Mbezi Luis,Sinza,Sheikhlango,na Mburahati.
Matokeo ya Ukaguzi huo yalibainisha mapungufu na utofauti wa taarifa za fedha kati ya taarifa iliyoletwa kwenye kikao cha kamati ya fedha cha mwezi March

1.Taarifa ya awali ilionyesha Kiasi cha Tsh 716 Millioni ndizo zilizokusanywa kwa Miezi 9, wakati taarifa sahihi baada ya ukaguzi wa Mfumo *kiasi cha Tsh billioni 1.009* ndizo zikizokufanywa kwa miezi 9,Hivyo kubainika kwa utofauti wa *kiasi cha Tsh 273,131,941,00 ambazo zilikuwa azijulikani zilipo.

2.Ukaguzi umeonyesha kuwa wahusika walikuwa hawapeleki fedha za makusanyo ya kila siku Benki,ambapo kiasi cha fedha cha *Tsh 198 281,401.00* zilikuwa hazijulikani zilipo na kutoingizwa benki kama utaratibu unavyotaka.

3.Baada Ya Mkaguzi kubainisha upotevu wa kiasi hicho cha fedha,na Wahusika kushindwa kuainisha risiti za malipo ya fedha hizo benki kama ilivyotakiwa


badala yake wahusika walianza kurudisha fedha hizo ambazo ni kiasi cha *Tsh 131,045,644.00 kilianza kurudishwa na wahusika hao baada ya Ukaguzi maalum kufanyika.

4.Mpaka juzi siku ya tarehe 05 mwezi June kikao kinaketi kiasi cha *Tsh Millioni 67,235,757.00 kilikuwa bado hakijarejeshwa na Wahusika katika akaunti za Halmashauri.

Baada ya Ukaguzi kuainisha Mapungufu au Ubadhirifu huo, Ni dhahiri wahusika wamekiuka miongozo ya fedha, Sheria za fedha na Mapato
kama vile Sheria ya Mapato ya fedha ya Serikali za mitaa namba 9 ya Mwaka 1982, Sheria ya fedha ya serikali za Mitaa sura namba 290 ya Mwaka 2002,Sheria namba 6 ya fedha ya Mwaka 2001 na Marekebisho yake ya Mwaka 2004,The local authority Financial Memorandum ya Mwaka 1997,Sheria ndogo za fedha za Mwaka 2015 Tangazo la serikali namba 527.

Hivyo kwa Miongozo na Sheria hizo za fedha za umma kamati ya Fedha imejiridhisha kuwa wametenda Makosa yafuatayo

1.Kutokupeleka fedha za Serikali benki kwa wakati.

2.Kuhujumu mapato ya Halmashauri,na kusababisha mapato kushuka

3.Kutumia fedha za Serikali bila ruhusa ya Afisa masuhuri (Mkurugenzi) anayetambulika kisheria

4.Kuingopea kwa makusudi Mamlaka ya usimamizi wa fedha( kamati ya fedha) kiasi tofauti na wanachokusanya kwa nia ya kuficha pesa.

5.Kushindwa kuwajibika katika nafasi za Usimamizi wa fedha kama mikataba ya ajira ilivyo wataka kuwajibika.

Hivyo kamati ya fedha na uongozi iliazimia yafuatayo.

1.Wahusika warudishe fedha zote kama Zilivyo ainishwa na Mkaguzi aukuonekana katika Mfumo wa kielectronic (POS) ambazo wameshindwa kuzipeleka benki

2.Mameneja wa mapato wa Masoko yote Wasimamishwe kazi kupisha uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha uliotokea.
(a) Obote Etta-Mabibo Ndizi
(b)Greyson R.Sebastian-Simu2000
(c)Frida Michael-Shekhilango
(d)John D.Twakiondo-Mabibo
(e)Edwin Mugila-Mabibo
(f)Bakari Mshanga-Sinza 2

3.Wahusika wote ikiwemo Mwekahazina,Msiamizi wa Mfumo,na Afisa mapato wanahusika kusimamia mameneja wote wasimame kupisha Uchunguzi.

4.Mkurugenzi awakabizi wote waliotajwa kwenye taarifa ya Ukaguzi na walioshindwa kuwajibika kusimia fedha za Serikali katika Vyombo vya Dola.

5.Mkurugenzi hawachukulie hatua za kinidhamu wahasibu wote wa vituo vilivyotajwa na Mkaguzi wa ndani kuhusika kwa upotevu wa fedha na baadae kuzirudisha baada ya ukaguzi

6.Mamlaka ya Nidhamu kwa watumishi iunde kamati ya kinidhamu (inquiry committee) itakayo jumuisha wakaguzi,na wataalamu wengineo kutoka Mkoani ya kuwahoji wahusika baada ya kupokea taarifa za kiuchunguzi kutoka Mamlaka za vyombo vya Dola na kisha kuleta agenda hiyo vikaoni kwa Hatua stahiki.

MWISHO
kamati ya fedha na Uongozi ya Halmashauri ya manispaa ya Ubungo,inaendelea kuchunguza vyanzo vingine vya Mapato vilivyosalia kama vimehujumiwa au kama kunamianya ya upotevu wa mapato,na taarifa za uchukuaji hatua kwa Walengwa Wazembe,wabadhirifu,na Wanaohujumu mapato ya Halmashauri zitatolewa punde.

Imetolewa Na

Mwenyekiti wa kamati ya Fedha na Uongozi
Boniface Jacob
Mstahiki Meya
Manispaa ya Ubungo
 
Back
Top Bottom