Kamati ya EPA usanii mtupu!

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
...ushahidi gani tena wanaokusanya toka kwa wananchi!? Wananchi wasiokuwa waajiriwa wa BoT hivi wanaweza kujua ushahidi wowote kuhusiana na ufisadi uliofanywa ndani ya BoT!? :confused:
Wataufahamu vipi ushahidi huo wakati mafisadi wameweka mapesa hayo katika bank accounts za nje ya nchi!? ushahidi wa kutosha upo tunachotaka kuona ni kufanyiwa kazi kwa ushahidi huo:confused:

Ama kweli Kikwete ni msanii wa hali ya juu!

Dk. Slaa ashtukia Kamati ya Kashfa ya EPA

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa, ameeleza kushitushwa kwake na utaratibu wa kukusanya ushahidi unaotumiwa na Kamati ya Kuchunguza Kashfa ya EPA inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mwanyika.
Dk. Slaa, mmoja wa wanasiasa wanaoheshimika na kinara wa harakati ya kuuanika ufisadi ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katikati ya mwaka jana, aliyasema hayo jana kupitia katika ujumbe wa maandishi alioutuma kwa Tanzania Daima.

Kwa mujibu wa Slaa ambaye dhamira yake ya kuwasilisha hoja binafsi bungeni akitaka kuundwa kwa Kamati ya Bunge kuichunguza BoT ilizimwa na Spika wa Bunge, utaratibu mzima uliotangazwa na kamati hiyo ya Mwanyika ni wa kutia shaka.

"Kamati ya Mwanyika, IGP Mwema na Hosea isifanye kiinimacho. Nimeshangazwa na utaratibu waliotangaza wa mtu kupeleka ushahidi kwa mjumbe mmoja mmoja wa kamati.

"Nikipeleka taarifa zangu, nina uhakika gani kama zitafikishwa kama zilivyo? Mimi nadhani kamati ilipaswa kufanya kazi kwa pamoja kama timu na si mtu mmoja mmoja," alisema Dk. Slaa.

Dk. Slaa ambaye hoja yake bungeni ilisababisha serikali ilazimike kumwagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali kuipa kampuni ya kimataifa, kazi ya kukagua upya hesabu za BoT za mwaka 2005/2006 alisema uchunguzi wowote katika sakata hili hauna budi kuanza kufanyika baada ya aliyekuwa gavana wa BoT, Daudi Ballali kuwekwa chini ya ulinzi na kuhojiwa.

Mbali ya hilo, alisema kwa kufuata utaratibu huo huo, aliyekuwa Waziri wa Fedha mwaka 2005, Basil Mramba na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Gray Mgonja nao wanapaswa kukamatwa na kuhojiwa.

"Siri zote za EPA na ufisadi wote wa BoT anazo Ballali. Kwa utaratibu huo huo wakamatwe Mramba na Mgonja na wahojiwe. Ndio waidhinishaji wakuu wa malipo yote ya serikali na wasimamizi wakuu. Serikali isiendelee kutufanya Watanzania wendawazimu," alisisitiza Dk. Slaa.

Akitoa mifano mingine kuhusu ufisadi ndani ya BoT, mwanasiasa huyo alieleza kushangazwa na kuendelea kusuasua kwa serikali katika kuchukua hatua katika masuala mengine ya ufisadi yaliyo nje ya EPA.

Alisema katika taarifa yake kuhusu ufisadi BoT, alishapata kuwasilisha tarehe na kiasi cha fedha kilichohamishwa kutoka katika taasisi hiyo kwenda kwenye kampuni nyingine inayolalamikiwa ya Deep Green na namna zilivyopelekwa katika Benki ya NBC tawi la Corporate.

Slaa alisema, alitaja hata namba ya hundi iliyolipia malipo hayo na jinsi fedha taslimu zilivyochotwa.

"Bila hatua ya kuwakamata kwanza na kuwahoji wahusika hao, ni usanii. Ushahidi wa kwanza uko BRELA (wakala wa usajili wa makampuni) na pia katika taarifa ya Ernst & Young (taasisi ya ukaguzi wa kimataifa iliyogundua upotevu wa shilingi bilioni 133 kupitia akaunti ya EPA)," alisema Slaa.

Slaa anatoa kauli hiyo siku moja tu baada ya Kamati ya Kuchunguza Ubadhirifu BoT inayoongozwa na Mwanyika, kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu kuanza rasmi kwa uchunguzi wake.

Katika taarifa yake hiyo iliyotolewa juzi na kuchapwa katika magazeti mbalimbali jana, kamati hiyo iliwaomba wananchi wenye taarifa zaidi zinazowezesha kusaidia uchunguzi kujitokeza na kutoa taarifa ama moja kwa moja kwa kamati au kwa kuwasiliana na mjumbe mmoja mmoja binafsi.

Kamati hiyo iliwahakikishia wananchi kuwa, kila chembe ya habari itakayopatikana itafuatiliwa kwa makini kwa nia ya kuhakikisha kuwa ukweli unajulikana na kuwekwa hadharani, ili kulinda heshima ya taifa.

"Ili kuiwezesha timu kufanya kazi yake kwa uhakika, wananchi wanaombwa kuwa na subira na kutoa kila ushirikiano utakaoiwezesha kukamilisha majukumu yake.

"Utaratibu umewekwa wa kupokea taarifa hizo kupitia Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa. Wananchi wenye taarifa hizi wazipeleke kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Saidi Mwema kwa simu 0754 785 557.

"Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba simu 0754 206 326, Edward Hosea, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU simu 0754 763 741 au Lilian Mashaka, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU simu 0754 336 116," ilisema taarifa hiyo.
 
waache usanii wao uchunguzi wote ushatolewa kilichokuwa kimebaki nikukamata nakuweka ndani wahusika wote hii tume mimi binafsi sina imani nayo kwani imeandaliwwa ili kuwalinda hawa vigogo fisadi ndani yanchi yetu.
 
Mwinyi aficha neno KASHFA YA BOT

na Joseph Zablon

WAKATI watu wengi wakijitosa kuzungumzia kashfa ya ubadhirifu wa mabilioni ya shilingi katika Benki Kuu (BoT), Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, ameonekana kusita kuungana nao.
Mwinyi aliweka bayana msimamo wake huo, nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam juzi, muda mfupi tu baada ya kukamilika kwa hafla ya ufunguaji wa akaunti katika Benki ya NMB, kwa ajili ya michuano ya soka ya Kombe la Ali Hassan Mwinyi Orphans.

Rais huyo mstaafu ambaye alikuwa akijibu swali aliloulizwa na mwandishi wa gazeti hili, alisema ni mapema mno kwa sasa kueleza msimamo wake kuhusu jambo hilo na akaahidi kufanya hivyo wakati muafaka utakapowadia.

"Suala la BoT… aahaaa…, siwezi kuzungumzia, ni mapema mno ………(kicheko), wakati ukifika nitalizungumzia," alisema rais huyo mstaafu huku akiingia nyumbani kwake.

Mwinyi anaweka bayana uamuzi wake huo ikiwa ni takriban wiki mbili sasa tangu Rais Jakaya Kikwete alipochukua uamuzi wa kutengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Daudi Ballali, siku chache tu baada ya kupokea taarifa ya ukaguzi wa hesabu za taasisi hiyo nyeti, kazi iliyofanywa na Kampuni ya kimataifa ya Ernst & Young.

Ballali aliyeko nchini Marekani anakoaminika kuwa alikwenda kutibiwa tangu katikati ya mwaka jana, ndiye ofisa pekee wa juu wa serikali ambaye tayari amehusishwa kwa namna moja au nyingine na ufujaji wa shilingi bilioni 133, fedha za umma kupitia Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

Mbali ya Ballali, viongozi wengine kadhaa wakiwamo Basil Mramba, aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati fedha hizo zikichotwa mwaka 2005 na Gray Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu Hazina wakati huo, ni miongoni mwa viongozi ambao majina yao yanatajwatajwa kuwa miongoni mwa watu wanaostahili kuwajibika au kuwajibishwa kutokana na ubadhirifu huo.

Tangu Kikwete atoe uamuzi huo, kumekuwa na maoni tofauti kutoka kwa watu kadhaa binafsi na taasisi za kijamii na kidini zilizoeleza kushtushwa na kugundulika kwa ubadhirifu huo mkubwa wa kwanza kuwekwa hadharani hapa nchini.

Katika hatua ya hivi karibuni, Mwenyekiti wa Chama cha siasa cha PPT-Maendeleo, Peter Mziray, ameitaka kamati iliyoteuliwa na Rais Kikwete, kuacha kufanya uchunguzi zaidi, na badala yake iwakamate viongozi wa taasisi za serikali, makampuni binafsi na wafanyabiashara ambao wametajwa katika ripoti ya Kampuni ya ukaguzi wa hesabu ya Ernst & Young kuhusika katika uchotaji wa fedha katika akaunti ya madeni ya nje (EPA).

Mziray aliyasema hayo jana alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa kitendo cha wanasheria kuomba wapewe taarifa kutoka kwa wananchi ni kupoteza muda, kwani masuala mengi ya msingi ambayo yanaweza kutumika kama ushahidi mahakamani, yalishabainishwa na kampuni hiyo.

Alisema kilichotakiwa kwa timu hiyo ni kutafuta vielelezo zaidi kutokana na maelezo yaliyotolewa na Ernst & Young kama vile kutafuta kumbukumbu za makampuni hayo katika ofisi za wakala wa usajili wa makampuni - BRELA.

Kwa upande mwingine, Mziray alisisitiza kuwa, anauona uhusiano wa kisayansi kati ya uchotaji wa fedha kutoka BoT na ushindi wa kishindo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

"Mwaka 2004 magazeti humu nchini yaliandika kwamba NEC ya CCM ilimwomba mwenyekiti wake wa wakati huo kuziongezea uwezo wa kifedha, magari na vitendea kazi ofisi za chama hicho nchini pote.

Na baada ya muda mfupi, CCM ilimwaga magari ya kuzinufaisha ofisi za wilaya zote pamoja na kugawa kanga, fulana na kofia nchi nzima. Tunahoji walipata wapi pesa kwa muda huo mfupi?

"Mimi sioni lolote la kumpongeza Rais Kikwete eti kwa kutengua ajira ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu kwani ni sehemu ya utendaji wake," alisema.

Alisema yeye ataridhika iwapo waliotajwa kuhusika na upoteaji wa fedha hizo wakichukuliwa hatua stahili kama vile kukamatwa na kuhojiwa, kwani ukiacha Dk. Ballali ambaye yupo nje ya nchi, wengi wa waliotajwa wamo humuhumu nchini.

Alisema kuwa bila ya jambo hili kuchukuliwa hatua kwa umakini, uamuzi wa kuzirejesha fedha hizo unaweza usitekelezeke.

Aidha, Mziray alimtaka aliyekuwa waziri wa fedha wakati wizi huo ulipotokea, Basil Mramba, na Waziri wa Fedha wa sasa, Zakia Meghji, kujiuzulu, si kwa kuwa wanahusika na wizi huo, bali ili kulinda heshima zao.

...ushahidi gani tena wanaokusanya toka kwa wananchi!? Wananchi wasiokuwa waajiriwa wa BoT hivi wanaweza kujua ushahidi wowote kuhusiana na ufisadi uliofanywa ndani ya BoT!? :confused:
Wataufahamu vipi ushahidi huo wakati mafisadi wameweka mapesa hayo katika bank accounts za nje ya nchi!? ushahidi wa kutosha upo tunachotaka kuona ni kufanyiwa kazi kwa ushahidi huo:confused:

Ama kweli Kikwete ni msanii wa hali ya juu!

Dk. Slaa ashtukia Kamati ya Kashfa ya EPA

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa, ameeleza kushitushwa kwake na utaratibu wa kukusanya ushahidi unaotumiwa na Kamati ya Kuchunguza Kashfa ya EPA inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mwanyika.
Dk. Slaa, mmoja wa wanasiasa wanaoheshimika na kinara wa harakati ya kuuanika ufisadi ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katikati ya mwaka jana, aliyasema hayo jana kupitia katika ujumbe wa maandishi alioutuma kwa Tanzania Daima.

Kwa mujibu wa Slaa ambaye dhamira yake ya kuwasilisha hoja binafsi bungeni akitaka kuundwa kwa Kamati ya Bunge kuichunguza BoT ilizimwa na Spika wa Bunge, utaratibu mzima uliotangazwa na kamati hiyo ya Mwanyika ni wa kutia shaka.

"Kamati ya Mwanyika, IGP Mwema na Hosea isifanye kiinimacho. Nimeshangazwa na utaratibu waliotangaza wa mtu kupeleka ushahidi kwa mjumbe mmoja mmoja wa kamati.

"Nikipeleka taarifa zangu, nina uhakika gani kama zitafikishwa kama zilivyo? Mimi nadhani kamati ilipaswa kufanya kazi kwa pamoja kama timu na si mtu mmoja mmoja," alisema Dk. Slaa.

Dk. Slaa ambaye hoja yake bungeni ilisababisha serikali ilazimike kumwagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali kuipa kampuni ya kimataifa, kazi ya kukagua upya hesabu za BoT za mwaka 2005/2006 alisema uchunguzi wowote katika sakata hili hauna budi kuanza kufanyika baada ya aliyekuwa gavana wa BoT, Daudi Ballali kuwekwa chini ya ulinzi na kuhojiwa.

Mbali ya hilo, alisema kwa kufuata utaratibu huo huo, aliyekuwa Waziri wa Fedha mwaka 2005, Basil Mramba na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Gray Mgonja nao wanapaswa kukamatwa na kuhojiwa.

"Siri zote za EPA na ufisadi wote wa BoT anazo Ballali. Kwa utaratibu huo huo wakamatwe Mramba na Mgonja na wahojiwe. Ndio waidhinishaji wakuu wa malipo yote ya serikali na wasimamizi wakuu. Serikali isiendelee kutufanya Watanzania wendawazimu," alisisitiza Dk. Slaa.

Akitoa mifano mingine kuhusu ufisadi ndani ya BoT, mwanasiasa huyo alieleza kushangazwa na kuendelea kusuasua kwa serikali katika kuchukua hatua katika masuala mengine ya ufisadi yaliyo nje ya EPA.

Alisema katika taarifa yake kuhusu ufisadi BoT, alishapata kuwasilisha tarehe na kiasi cha fedha kilichohamishwa kutoka katika taasisi hiyo kwenda kwenye kampuni nyingine inayolalamikiwa ya Deep Green na namna zilivyopelekwa katika Benki ya NBC tawi la Corporate.

Slaa alisema, alitaja hata namba ya hundi iliyolipia malipo hayo na jinsi fedha taslimu zilivyochotwa.

"Bila hatua ya kuwakamata kwanza na kuwahoji wahusika hao, ni usanii. Ushahidi wa kwanza uko BRELA (wakala wa usajili wa makampuni) na pia katika taarifa ya Ernst & Young (taasisi ya ukaguzi wa kimataifa iliyogundua upotevu wa shilingi bilioni 133 kupitia akaunti ya EPA)," alisema Slaa.

Slaa anatoa kauli hiyo siku moja tu baada ya Kamati ya Kuchunguza Ubadhirifu BoT inayoongozwa na Mwanyika, kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu kuanza rasmi kwa uchunguzi wake.

Katika taarifa yake hiyo iliyotolewa juzi na kuchapwa katika magazeti mbalimbali jana, kamati hiyo iliwaomba wananchi wenye taarifa zaidi zinazowezesha kusaidia uchunguzi kujitokeza na kutoa taarifa ama moja kwa moja kwa kamati au kwa kuwasiliana na mjumbe mmoja mmoja binafsi.

Kamati hiyo iliwahakikishia wananchi kuwa, kila chembe ya habari itakayopatikana itafuatiliwa kwa makini kwa nia ya kuhakikisha kuwa ukweli unajulikana na kuwekwa hadharani, ili kulinda heshima ya taifa.

"Ili kuiwezesha timu kufanya kazi yake kwa uhakika, wananchi wanaombwa kuwa na subira na kutoa kila ushirikiano utakaoiwezesha kukamilisha majukumu yake.

"Utaratibu umewekwa wa kupokea taarifa hizo kupitia Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa. Wananchi wenye taarifa hizi wazipeleke kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Saidi Mwema kwa simu 0754 785 557.

"Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba simu 0754 206 326, Edward Hosea, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU simu 0754 763 741 au Lilian Mashaka, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU simu 0754 336 116," ilisema taarifa hiyo.
Leo hii Dr. Slaa mnamtukana n kumuita Dr mihogo baada ya kumuuzia chama Lowassa
 
Back
Top Bottom