BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,831
- 287,784
...ushahidi gani tena wanaokusanya toka kwa wananchi!? Wananchi wasiokuwa waajiriwa wa BoT hivi wanaweza kujua ushahidi wowote kuhusiana na ufisadi uliofanywa ndani ya BoT!? 
Wataufahamu vipi ushahidi huo wakati mafisadi wameweka mapesa hayo katika bank accounts za nje ya nchi!? ushahidi wa kutosha upo tunachotaka kuona ni kufanyiwa kazi kwa ushahidi huo
Ama kweli Kikwete ni msanii wa hali ya juu!
Dk. Slaa ashtukia Kamati ya Kashfa ya EPA
na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa, ameeleza kushitushwa kwake na utaratibu wa kukusanya ushahidi unaotumiwa na Kamati ya Kuchunguza Kashfa ya EPA inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mwanyika.
Dk. Slaa, mmoja wa wanasiasa wanaoheshimika na kinara wa harakati ya kuuanika ufisadi ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katikati ya mwaka jana, aliyasema hayo jana kupitia katika ujumbe wa maandishi alioutuma kwa Tanzania Daima.
Kwa mujibu wa Slaa ambaye dhamira yake ya kuwasilisha hoja binafsi bungeni akitaka kuundwa kwa Kamati ya Bunge kuichunguza BoT ilizimwa na Spika wa Bunge, utaratibu mzima uliotangazwa na kamati hiyo ya Mwanyika ni wa kutia shaka.
"Kamati ya Mwanyika, IGP Mwema na Hosea isifanye kiinimacho. Nimeshangazwa na utaratibu waliotangaza wa mtu kupeleka ushahidi kwa mjumbe mmoja mmoja wa kamati.
"Nikipeleka taarifa zangu, nina uhakika gani kama zitafikishwa kama zilivyo? Mimi nadhani kamati ilipaswa kufanya kazi kwa pamoja kama timu na si mtu mmoja mmoja," alisema Dk. Slaa.
Dk. Slaa ambaye hoja yake bungeni ilisababisha serikali ilazimike kumwagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali kuipa kampuni ya kimataifa, kazi ya kukagua upya hesabu za BoT za mwaka 2005/2006 alisema uchunguzi wowote katika sakata hili hauna budi kuanza kufanyika baada ya aliyekuwa gavana wa BoT, Daudi Ballali kuwekwa chini ya ulinzi na kuhojiwa.
Mbali ya hilo, alisema kwa kufuata utaratibu huo huo, aliyekuwa Waziri wa Fedha mwaka 2005, Basil Mramba na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Gray Mgonja nao wanapaswa kukamatwa na kuhojiwa.
"Siri zote za EPA na ufisadi wote wa BoT anazo Ballali. Kwa utaratibu huo huo wakamatwe Mramba na Mgonja na wahojiwe. Ndio waidhinishaji wakuu wa malipo yote ya serikali na wasimamizi wakuu. Serikali isiendelee kutufanya Watanzania wendawazimu," alisisitiza Dk. Slaa.
Akitoa mifano mingine kuhusu ufisadi ndani ya BoT, mwanasiasa huyo alieleza kushangazwa na kuendelea kusuasua kwa serikali katika kuchukua hatua katika masuala mengine ya ufisadi yaliyo nje ya EPA.
Alisema katika taarifa yake kuhusu ufisadi BoT, alishapata kuwasilisha tarehe na kiasi cha fedha kilichohamishwa kutoka katika taasisi hiyo kwenda kwenye kampuni nyingine inayolalamikiwa ya Deep Green na namna zilivyopelekwa katika Benki ya NBC tawi la Corporate.
Slaa alisema, alitaja hata namba ya hundi iliyolipia malipo hayo na jinsi fedha taslimu zilivyochotwa.
"Bila hatua ya kuwakamata kwanza na kuwahoji wahusika hao, ni usanii. Ushahidi wa kwanza uko BRELA (wakala wa usajili wa makampuni) na pia katika taarifa ya Ernst & Young (taasisi ya ukaguzi wa kimataifa iliyogundua upotevu wa shilingi bilioni 133 kupitia akaunti ya EPA)," alisema Slaa.
Slaa anatoa kauli hiyo siku moja tu baada ya Kamati ya Kuchunguza Ubadhirifu BoT inayoongozwa na Mwanyika, kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu kuanza rasmi kwa uchunguzi wake.
Katika taarifa yake hiyo iliyotolewa juzi na kuchapwa katika magazeti mbalimbali jana, kamati hiyo iliwaomba wananchi wenye taarifa zaidi zinazowezesha kusaidia uchunguzi kujitokeza na kutoa taarifa ama moja kwa moja kwa kamati au kwa kuwasiliana na mjumbe mmoja mmoja binafsi.
Kamati hiyo iliwahakikishia wananchi kuwa, kila chembe ya habari itakayopatikana itafuatiliwa kwa makini kwa nia ya kuhakikisha kuwa ukweli unajulikana na kuwekwa hadharani, ili kulinda heshima ya taifa.
"Ili kuiwezesha timu kufanya kazi yake kwa uhakika, wananchi wanaombwa kuwa na subira na kutoa kila ushirikiano utakaoiwezesha kukamilisha majukumu yake.
"Utaratibu umewekwa wa kupokea taarifa hizo kupitia Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa. Wananchi wenye taarifa hizi wazipeleke kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Saidi Mwema kwa simu 0754 785 557.
"Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba simu 0754 206 326, Edward Hosea, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU simu 0754 763 741 au Lilian Mashaka, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU simu 0754 336 116," ilisema taarifa hiyo.