KAMATI YA DINI YAIBUA IFISADI WA 1.7trillion DHIDI YA SERIKALI

mchaichai

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
648
76
NI MAASKOFU, MASHEHE, WASEMA WIZI UPO KWENYE MISAMAHA YA KODI, MAGENDO
Fredy Azzah na Raymond Kaminyoge KAMATI ya Viongozi wa Dini, imetoa ripoti yake ya utafiti kuhusu uchumi wa nchi na kusema Serikali inapoteza Sh1.7trilioni kutokana na ukwepaji kodi, misamaha ya kodi na utoroshwaji wa mali na fedha nje ya nchi.

Matokeo ya utafiti wa kamati hiyo yametolewa wakati kesho Serikali inatarajiwa kusoma Bajeti Kuu kwa mwaka 2012/13, huku ikitegemea misaada kutoka nchi wahisani wanaochangia katika Mfuko Mkuu wa Bajeti (GBS). Utafiti huo uliofanywa na Kamati ya Masuala ya Uchumi na Haki za Binadamu (ISCJIC) na kupewa jina la ‘The one billion dollar question: how can Tanzania Stop losing so much tax revenue’ (Suala la dola bilioni moja: Tanzania inawezaje kuzuia upotevu wa kiasi hicho cha kodi?) ilizinduliwa jana jijini Dar es Salaam.


SOURCE MWANANCHI SOMA HABARI KAMILI
 
Back
Top Bottom