Kamati ya Bunge yamweka kitimoto Anne Kilango; Ni kuhusiana na tuhuma za Rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati ya Bunge yamweka kitimoto Anne Kilango; Ni kuhusiana na tuhuma za Rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 13, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  *Ahojiwa na Kamati ya Bunge kwa saa mbili
  *Ni kuhusiana na tuhuma za rushwa

  Mtanzania | JUMAPILI, AGOSTI 12, 2012 | NA MWANDISHI WETU

  HATIMAYE Mbunge wa Same Mashariki (CCM) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Anne Kilango, juzi amehojiwa karibu saa mbili kutokana na tuhuma mbalimbali za rushwa zinazomkabili.

  Habari za kuaminika ambazo MTANZANIA Jumapili imezipata kutoka mjini Dodoma, zinasema Kilango aliitwa mbele ya Kamati Ndogo ya Bunge, iliyoundwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda kuchunguza tuhuma za rushwa zinazowakabili wabunge mbalimbali.

  Kamati hiyo, ambayo inaongozwa na Mwenyekiti Brigedia Jenerali mstaafu, Hassan Ngwilizi, ilimhoji Kilango kuhusiana na madai ya kupokea rushwa katika mradi wa ujenzi wa gati namba 12 katika Bandari ya Dar es Salaam.

  "Kama unavyosema ni kweli, juzi ameitwa mbele ya kamati kuja kutoa maelezo yake, kwa sababu amekuwa akihusishwa na tuhuma hizi kwa muda sasa… kama unavyojua yeye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu.

  "Tuliona ni mtu muhimu mno kwetu, kwa kweli alitupatia ushirikiano mzuri kwa kile anachokijua… sasa mambo mengi siwezi kuyasema ndugu yangu," kilisema chanzo chetu.

  "Moja ya masuala makubwa tulilomhoji ni kuhusiana na tuhuma za rushwa katika ujenzi wa geti namba 12 katika bandari ya Dar es Salaam, pia tulimhoji juu ya yeye kutajwa kupokea rushwa na kumtetea aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), William Mhando.

  "Kama utakumbuka Kilango ni mmoja wa wabunge ambao wanadaiwa kumtetea kwa nguvu zote Muhando, wakati anasimamishwa pale TANESCO… tumepata maelezo yake, lakini nakushauri ndugu yangu uwe na subira wakati huu ambao kamati inaendelea na kazi yake," kilisema chanzo chetu.

  Habari zinasema, pia Kilango anadaiwa kuwa mstari wa mbele kumtetea Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi, kuwa hakupokea rushwa kutoka kwa moja ya makampuni makubwa ya kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi (majina tunayo).

  Kamati hiyo, inaundwa na Mwenyekiti Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi, ambaye pia ni Mbunge wa Mlalo (CCM), wajumbe wengine ni Kapteni John Chiligati (Manyoni Mashariki-CCM), Riziki Omar Juma (Viti Maalum-CUF), Said Arfi (Mpanda Mjini-Chadema) na Gosbert Blandes (Karagwe-CCM).
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Hivi Anne Kilango Malecela alikuwapo kwenye List ya Wabunge waliokuwa wanakula na Tanesco?

  Au wanampakazia tu, sababu ya kujiingiza UWT??

  Sizijui SIASA za CCM lakini wanajua kuruka ruka kama Sungura na kumuangusha mtu mwingine kabisaa na kuacha

  Fisadi bobea palepale...
   
 3. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Sasa hii habari inachanganya, inasemekana kwamba Muhando alikuwa anshirikiana na makampuni ya kuuza mafuta wakati Maswi alipingingana nao, sasa haiwezekani mtu ukawatetea Muhando na Maswi kwa pamoja!!- labda nisaidiwe tafadhali
   
 4. p

  politiki JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  siwezi kushangaa kuhusu anna kilango kula rushwa kwani utetezi wake wa wala rushwa hauwezi kuwa wa hivi hivi kama angelikuwa ni mtu basi asingeliwatetea wahusika bali angeomba uchunguzi rasmi ndio uwatete wahusika kwa kuwaclear
  na siyo yeye kusimama na kutetea vitu ambavyo hata ukimwambia mtoto mdogo anaelewa kuwa kuna rushwa imeliwa.
   
 5. k

  kayumba JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hata kama sababu za kutajana kwa wale waliokula rushwa itakuwa ni chuki za kisiasa lakini jamii itafaidika na chuki hizo. Ikumbukwe na EPA walitajana baada ya chuki zao binafsi nasi tukajua kilichokuwa kinaendelea.

  Kama ninavyosema siku zote, Hakuna mbunge wa CCM anayepinga Ufisadi kutoka rohoni. Ukiona mwanaCCM anapinga ufisadi ujue kakosa mgao au anayenufaika na mgao ni mbaya wake katika siasa zao za makundi. Nitaendelea kuamini hivyo mpaka pale watakapobadilika!
   
 6. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wabunge ambao wako kwenye hizi kamati 98% ni wala rushwa so sio wanamkamata mmoja mmoja wakamate wote hizo kamati zote zivunjwe kama baraza la mawaziri linabadilishwa kwann hizo kamati zisibadilishwe?
   
 7. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 737
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kilango alikuwa mpiga kelele sana mpaka akapata tuzo ya USA ya Mwanamke JASIRI. Leo Anna Kilango siye yule wa mwanzo amekuwa hana msimamo na mtetezi wa wezi. Hatujui kama kavuta mshiko lakini tunapata picha kuwa YAWEZEKANA:
   
 8. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #8
  Aug 13, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Huyo mama si inasemekana hata pesa za fungate lake yeye na baba yake le mutuz walipewa na fisadi wa EPA? Anaitwa nani kumbe yule jamaa aliye tajwa na Sofia mnyama pale bungeni?
   
 9. ugolo wa bibi

  ugolo wa bibi JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 1,226
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Anne kilango,Olesendeka..walikuwa ni wapiga kelele sana.......teh teh teh teh
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  jaman me hata simuon msafi wa kumkagua mwenzie hapo,,,,woote wachafu na ndio maana hawataki live show pale dodoma
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  si malaika yule,ukumbuke kuwa aliwah kutajwa siku za nyuma kwa biashara ya unga kinondoni
   
 12. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  ni uchafu na uchochezi wa gazeti la mtanzania kwa kutumiwa na sophia simba ili kumharibia anne kilango sioni stori hapa zaidi ya ukanjanja
   
 13. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Wajumbe woooote, ila Chiligati!? Sijui!
   
 14. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 15. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #15
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  mazee kajengo ketu pale moroco kanaleta problemae, bado pale karibu na mnzi. la sivyo chi chi em itageuzwa limited coy
   
 16. t

  tenende JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135

  jitu tapeli au?
   
 17. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #17
  Aug 13, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Gutter Politics
   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Siasa zimefika mahali pake...kazi ipo
   
 19. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #19
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  Bahati mbaya mamaangu Anne hana watu humu maana tukianza action zetu za utotoni nani atasimama. Mbinu za UWT hizi maana imekuwa issue ili aonekana hafai. Basi kati ya waovu hutu aweza kutibu na kubadilika na kuwa mwema.
   
 20. Edmond

  Edmond JF-Expert Member

  #20
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Duh pesa sabuni ya roho bana, hata ninyi wote wachangiaji humu mkidakishwa hizi kelele mnazopiga hapa jukwaani mtatulizana mwenyewe, nani asiyependa hela bana?
   
Loading...