Kamati ya bunge "yakataa" ardhi ya Tanzania kutumika kwa manufaa ya EAC. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati ya bunge "yakataa" ardhi ya Tanzania kutumika kwa manufaa ya EAC.

Discussion in 'International Forum' started by Ngongo, Jan 20, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Kamati ya bunge ya mambo ya nje,ulinzi na usalama umeitaka serekali kukataa muundo wowote wa ushirikiano wa Afrika mashariki utakaoruhusu ardhi ya Tanzania kutumika kwa manufaa ya shirikisho.
  Kamati ya bunge imeitaka serekali kuwa makini na suala la ardhi kwani ni rasilimali adimu na urithi pekeewa wananchi wa Tanzania.
  Kamati ya bunge iliwasilisha rasmi mapendekezo yake kwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa mheshimiwa B Membe.
   
 2. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Wadau

  Kwa hili naomba niipongeze kamati ya Bunge kwa Kazi nzuri iliyoifanya kwani wangeruhusu hardhi yetu itumike kwa manufaaa ya EAC, basi kesho nyake ungeona majiranizutu wa EAC wangevamia kila sehemu ili wapate ardhi. Mfano angalia Kenya wanapigana mpaka leo kwa sababu ya ardhi, the same to Rwanda na Burundi.

  Walikuwa wanavizia tukubali ardhi itumike eti kwa manufaa ya EAC. NANI ANATAKA UPUMBAVU HUO. Yaani wanatuona sisi WA TZ ni Mafalaaaaaaaaaaaaa kumbe wao ndio mafalaaaaaaaaaaaa tena wakutupa
   
 3. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kamati ya Bunge wanastahili pongezi kwa hili kwani kumekuwa na tetesi kwamba Wakenya wanataka kutumia mgongo wa Jumuia ya Afrika Mashariki kununua Ardhi ya TZ kwa kuwa wana uwezo kifedha.Tena ni vema kutumia fursa hii kuchunguza Wakenya waliojitwalia Ardhi kinyemela na kuirudisha kwa wananchi.
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Hakuna mtanzania halisi atakayepingana na kamati ya bunge ya mambo nje,ulinzi na usalama.Tatizo langu mpaka sasa watanzania bado tumeshikilia ardhi tu bila kuangalia mambo mengine muhimu kama free movement nadhani nalo ni hatari sana hasa katika sector ya utalii na usalama wetu.Miaka ya nyuma wakenya waliidanganya dunia kuwa mlima Kilimanjaro uko Kenya sasa kama free movememnt nayo isipoangaliwa vizuri tutarudi kulekule tulikotoka.
  Sector ya utalii inatoa mchango mkubwa katika kukuza pato la taifa hakuna asiyejua wenzetu wamepiga hatua kubwa katika sector ya utalii tusipo angalia makampuni makubwa yaliyopo Tanzania yanaweza kutoweka kabisa.
   
 5. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu Ngogo, huu ni msimamo saafi kabisa na ni a true reflection ya maoni ya wa TZ wengi.Ushirikiano ambao jirani yako anainsist kulala nyumbani kwako lazima uwe suspect.
  Ushirikiano uanzie katika kuratify tarriffs za kodi,viwango vya bidhaa na huduma nk
  Hatimae kuainisha sera za kidemokrasia katika nchi zetu kuzuia migogoro ya kisiasa.
  Tusipofanya hivyo tutakaribisha madudu ya nchi nyingine.
   
 6. R

  Rodelite JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2009
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 320
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu hapo umesema kweli kabisa. Katika miaka ya 80s Kenya Airways ilikuwa inaitwa "The Pride of Kilimanjaro" ...sijui kama wamwbadilisha. Wakati ule ndio watalii walitua Kenya na kulala kwenye mahoteli yao halafu walikuwa wanavushwa kupitia Namanga kwenda kuuona au kuupanda mlima kwa bei "chee".
   
 7. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Kichwa cha mada ni kibovu. Kamati ya Bunge haiwezi kukataa "ardhi ya Tanzania kutumika kwa manufaa ya EAC". Mbona tayari ardhi ya Tanzania inatumika vizuri tu kwa manufaa ya EAC? Makao makuu ya EAC yapo kwenye ardhi ya Tanzania, na tungependa watumie ardhi yetu kuweka taasisi za EAC zaidi.

  There must be give and take. We must win some and lose some. Ni ajabu kuona nchi yenye makao makuu ya EAC inakuwa mstari wa mbele kupinga mipango ya EAC.

  Ukitaka cha mvunguni sharti uiname. Tukitaka umoja sharti tukubali kuuchangia kwa hali na mali.
   
 8. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  Excellent A. Mushi.
   
Loading...