Kamati ya Bunge yaitwisha Serikali mzigo wa Dowans

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imeibebesha Serikali mzigo wa deni la kampuni ya kufua umeme ya Dowans ikisema ndiyo iliyohusika na mkataba wake.

Serikali imekuwa ikidai kwamba Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), ndilo linalopaswa kulipa deni hilo.

Agizo hilo la POAC lilitolewa jana katika kikao cha pamoja baina ya Kamati hiyo na makatibu wakuu wa Wizara za Fedha na Uchumi na Nishati na Madini na watendaji wa Tanesco.

Juzi, Kamati hiyo ilishindwa kuthibitisha deni hilo la zaidi ya Sh96 bilioni kutokana na kukosekana kwa ufafanuzi wa uhalali wake na nani anastahili kuilipa kati ya Serikali na Tanesco.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho cha juzi zililidokeza gazeti hili kuwa tangu kutolewa kwa hukumu iliyotaka Dowans ilipwe fidia kutokana na mkataba wake wa kuzalisha umeme kuvunjwa kiholela, Serikali na Tanesco wamekuwa wakitupiana mpira wa nani anayepaswa kulipa deni hilo.

"Kamati imeshindwa kuthibitisha uhalali wa deni hili na tumewataka makatibu wakuu kufika kesho (Jumatano) ili waweze kutupa ufafanuzi kabla ya kutoa uamuzi," aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Murtaza Mangungu, aliwaambia waandishi wa habari.


Baada ya mahojiano ya muda baina ya viongozi hao wa Serikali na Tanesco, Kamati hiyo iliitaka Serikali kuilipa Dowans ikiwa mahakama itatoa hukumu ya deni hilo kulipwa.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe alisema jana kuwa kwa mujibu wa vitabu vilivyotolewa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), deni la Dowans lilitakiwa kuingizwa kwenye vitabu vya Serikali na si Tanesco.


"... Kwa sababu wao (Serikali) ndiyo walioingia mkataba na kampuni hiyo (Dowans) ya kuwalipa gharama za ununuzi wa umeme," alisema Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema).

Zitto alisema Serikali ilipinga suala hilo na Katibu Mkuu (Hazina) alimwandikia CAG, Februari 9, mwaka huu kuwa Tanesco inapaswa kulipa deni hilo. Tanesco nayo iliandika barua ya kupinga kulipa deni hilo jambo ambalo lilisababisha CAG kukataa kusaini vitabu hivyo.


"Ripoti ya CAG iliyotolewa kwenye kamati hii imeonyesha kuwa deni hili linapaswa kuonekana kwenye vitabu vya Serikali na si Tanesco kwa sababu wao (Serikali), ndiyo walioingia mkataba na kampuni hiyo kwa ajili ya kuzalisha umeme. Hivyo deni lake halipaswi kulipwa na Tanesco. Utata huo ulimfanya CAG aombe mwongozo," alieleza Zitto jana.


Kwa mujibu wa Zitto, baada ya malumbano hayo, POAC iliomba kukutana na makatibu wakuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi; na Nishati na Madini ili wajadili suala hilo na kufikia muafaka.

"Muafaka ni kuwa deni hilo linapaswa kuonekana kwenye vitabu vya Serikali hivyo wao ndiyo wenye jukumu la kulipa deni hilo ikiwa mahakama itatoa hukumu ya kulipwa," alisema Zitto.


Alisema Tanesco haiwezi kulipa deni hilo kwa sababu wao siyo walioingia mkataba na Dowans... "Tanesco haiwezi kubebeshwa mzigo usiowahusu, badala yake Serikali itawajibika yenyewe katika suala hilo ikiwa hukumu yake itatoka."

Zitto alisema Tanesco linajiendesha kwa hasara kila mwaka na hiyo inatokana na wadaiwa kushindwa kulipa madeni yao ipasavyo, hivyo kulibebesha mzigo wa kulipa deni kubwa kama la Dowans ni sawa na kulifilisi au kuliua kabisa.


"Mwaka jana, Tanesco lilipata hasara ya Sh5 bilioni. Hii inatokana na sababu mbalimbali, ikiwamo ya wadaiwa wao kushindwa kulipa madeni yao. Jambo hilo limesababisha shirika lijiendeshe kwa hasara na kutokana na hali hiyo, hawawezi kubebeshwa mzigo huo wa Dowans," aliongeza.

Sakata la malipo kwa kampuni ya Dowans limeibua mjadala mkubwa miongoni mwa jamii hasa ya wasomi, wanasiasa na watu mbalimbali baadhi yao kupinga na wengine kukubaliana nayo.


Mjadala ulipamba moto baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema kueleza kuwa Serikali haina pingamizi na malipo hayo na kwamba tayari imewaagiza wahusika kutekeleza mara moja. Kauli hiyo ya Werema na ile iliyotolewa na Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani kuunga mkono malipo hayo ziliwafanya wanaharakati wa haki za binadamu kufungua kesi mahakamani kupinga malipo hayo.


Source: Mwananchi
 
Duh! Hii Serikali ya kisanii imesaini mkataba na fisadi Rostam alias Richmond/Dowans halafu wawatupie TANESCO uozo wao ili shirika hilo ndiyo lilipe deni hilo! Kweli tuna Serikali makini!
 
Kamati ya Bunge yaitwisha Serikali mzigo wa Dowans Wednesday, 30 March 2011 21:29

Patricia Kimelemeta
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imeibebesha Serikali mzigo wa deni la kampuni ya kufua umeme ya Dowans ikisema ndiyo iliyohusika na mkataba wake. Serikali imekuwa ikidai kwamba Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), ndilo linalopaswa kulipa deni hilo.Agizo hilo la POAC lilitolewa jana katika kikao cha pamoja baina ya Kamati hiyo na makatibu wakuu wa Wizara za Fedha na Uchumi na Nishati na Madini na watendaji wa Tanesco.

Juzi, Kamati hiyo ilishindwa kuthibitisha deni hilo la zaidi ya Sh96 bilioni kutokana na kukosekana kwa ufafanuzi wa uhalali wake na nani anastahili kuilipa kati ya Serikali na Tanesco.Habari kutoka ndani ya kikao hicho cha juzi zililidokeza gazeti hili kuwa tangu kutolewa kwa hukumu iliyotaka Dowans ilipwe fidia kutokana na mkataba wake wa kuzalisha umeme kuvunjwa kiholela, Serikali na Tanesco wamekuwa wakitupiana mpira wa nani anayepaswa kulipa deni hilo.

"Kamati imeshindwa kuthibitisha uhalali wa deni hili na tumewataka makatibu wakuu kufika kesho (Jumatano) ili waweze kutupa ufafanuzi kabla ya kutoa uamuzi," aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Murtaza Mangungu, aliwaambia waandishi wa habari.

Baada ya mahojiano ya muda baina ya viongozi hao wa Serikali na Tanesco, Kamati hiyo iliitaka Serikali kuilipa Dowans ikiwa mahakama itatoa hukumu ya deni hilo kulipwa.Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe alisema jana kuwa kwa mujibu wa vitabu vilivyotolewa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), deni la Dowans lilitakiwa kuingizwa kwenye vitabu vya Serikali na si Tanesco.

"... Kwa sababu wao (Serikali) ndiyo walioingia mkataba na kampuni hiyo (Dowans) ya kuwalipa gharama za ununuzi wa umeme," alisema Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema). Zitto alisema Serikali ilipinga suala hilo na Katibu Mkuu (Hazina) alimwandikia CAG, Februari 9, mwaka huu kuwa Tanesco inapaswa kulipa deni hilo. Tanesco nayo iliandika barua ya kupinga kulipa deni hilo jambo ambalo lilisababisha CAG kukataa kusaini vitabu hivyo.

"Ripoti ya CAG iliyotolewa kwenye kamati hii imeonyesha kuwa deni hili linapaswa kuonekana kwenye vitabu vya Serikali na si Tanesco kwa sababu wao (Serikali), ndiyo walioingia mkataba na kampuni hiyo kwa ajili ya kuzalisha umeme. Hivyo deni lake halipaswi kulipwa na Tanesco. Utata huo ulimfanya CAG aombe mwongozo," alieleza Zitto jana.

Kwa mujibu wa Zitto, baada ya malumbano hayo, POAC iliomba kukutana na makatibu wakuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi; na Nishati na Madini ili wajadili suala hilo na kufikia muafaka."Muafaka ni kuwa deni hilo linapaswa kuonekana kwenye vitabu vya Serikali hivyo wao ndiyo wenye jukumu la kulipa deni hilo ikiwa mahakama itatoa hukumu ya kulipwa," alisema Zitto.

Alisema Tanesco haiwezi kulipa deni hilo kwa sababu wao siyo walioingia mkataba na Dowans... "Tanesco haiwezi kubebeshwa mzigo usiowahusu, badala yake Serikali itawajibika yenyewe katika suala hilo ikiwa hukumu yake itatoka."Zitto alisema Tanesco linajiendesha kwa hasara kila mwaka na hiyo inatokana na wadaiwa kushindwa kulipa madeni yao ipasavyo, hivyo kulibebesha mzigo wa kulipa deni kubwa kama la Dowans ni sawa na kulifilisi au kuliua kabisa.

"Mwaka jana, Tanesco lilipata hasara ya Sh5 bilioni. Hii inatokana na sababu mbalimbali, ikiwamo ya wadaiwa wao kushindwa kulipa madeni yao. Jambo hilo limesababisha shirika lijiendeshe kwa hasara na kutokana na hali hiyo, hawawezi kubebeshwa mzigo huo wa Dowans," aliongeza.

Sakata la malipo kwa kampuni ya Dowans limeibua mjadala mkubwa miongoni mwa jamii hasa ya wasomi, wanasiasa na watu mbalimbali baadhi yao kupinga na wengine kukubaliana nayo.

Mjadala ulipamba moto baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema kueleza kuwa Serikali haina pingamizi na malipo hayo na kwamba tayari imewaagiza wahusika kutekeleza mara moja.

Kauli hiyo ya Werema na ile iliyotolewa na Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani kuunga mkono malipo hayo ziliwafanya wanaharakati wa haki za binadamu kufungua kesi mahakamani kupinga malipo hayo.

Source:Mwananchi
 
Taifa ni kama bahari huwa alibebi uchafu so akakadowans katatusumbua lakin one day katajikuta ufukweni.
 
Tunachozungumzia kila siku ktk Dowans ni Kwamba haipaswi kulipwa na Institution yoyote inayopata pato lake kutokana na kodi za watanzania...iwe TRA,HAZINA,PPF,LOCAL GOVT,BUNGE AU HATA SERIKALI KUU na tulihitaji misimamo ya kamati inayofanana na hiyo.
 
Sasa mambo hadharani, ndio maana baadhi ya wana ccm wameona hayo kwa kusema uozo wa ccm serikali inajitwisha na ule wa serikali ccm inajitwisha
 
Dowans, Richmond zainyonga Serikali


Na Beatrice Shayo
31st March 2011

headline_bullet.jpg
Kamati ya bunge yatwika zigo

Poac.jpg

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe (wa 2 kulia) na Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, baada ya mkutano kati ya kamati na katibu mkuu huyo jana, kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam jana.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imeliokoa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kwa kuiagiza serikali kujiandaa kuilipa kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans Tanzania Limited Sh. bilioni 94 ikiwa mahakama itaidhinisha malipo hayo.

Agizo hilo, limetolewa na POAC siku nne baada ya kuibuka mvutano mkubwa kati ya Tanesco na Wizara ya Fedha na Uchumi kuhusu nani kati yao anayepaswa kubeba mzigo wa kuilipa Dowans fedha hizo.

Fedha hizo, Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC) iliiamuru Tanesco kuilipa Kampuni ya Dowans Tanzania Limited kwa kosa la kuvunjiwa mkataba wake.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taratibu, Dowans haiwezi kulipwa fedha hizo hadi hapo Mahakama Kuu ya Tanzania itakaposajili hukumu ya ICC.

Tayari Dowans imekwisha kuwasilisha maombi Mahakama Kuu kutaka hukumu hiyo isajiliwe ili ilipwe fedha hizo, lakini Tanesco kwa upande mmoja na mashirika 17 ya wanaharakati kwa upande mwingine, wamewasilisha pingamizi mahakamani hapo kupinga hukumu kusajiliwa.

Agizo la POAC kwa serikali lilitangazwa na Mwenyekiti wake, Zitto Kabwe, alipozungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam jana.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alisema baada ya kamati yake kupitia hesabu za Tanesco, walilazimika kuwaita Makatibu Wakuu wa Wizara ya Fedha na wa Nishati na Madini.

Alisema lengo la kuwaita makatibu wakuu hao, lilikuwa kuona namna serikali itakavyolipa fedha hizo kwa kuwa ndiyo iliyoingia mkataba na Dowans.

Zitto alisema baada ya kuzungumza nao, kamati imefikia uamuzi huo kwa kuwa mchakato mzima wa kukodi kampuni hiyo, kuanzia kampuni ya Richmond, ambayo Dowans walirithi mkataba wake na Tanesco, ulisimamiwa kwa karibu na serikali.

Alisema Tanesco iliingia mkataba huo na Dowans kwa maelekezo na usimamizi wa serikali.

"
Hivyo, basi vitabu vya Tanesco vinatakiwa visiwe na deni la Dowans kutokana na kwamba, maelekezo yote yaliyofanywa yalikuwa yanatoka serikalini na sio maamuzi yao wenyewe," alisema Zitto.

Kwa agizo hilo la POAC, malipo ya Dowans yatalipwa na serikali kuu na sio Tanesco.

CHANZO: NIPASHE

My note:Huyu Dogo yeye ameahidiwa asilimia ngapi na RA??
 
Kwa hali hii mambo bado kabisa

Serikali yachakachua Mswada wa Katiba Mpya - Kumpa Rais mamlaka ya kuunda tume
KAMA vile imeshindwa kusoma alama za nyakati, serikali imeamua kuchakachua mchakato wa marekebisho ya katiba mpya kwa kuandaa muswada ambao unapinga yote yanayopendekezwa na wananchi.

Badala yake, serikali inarejesha yote yanayokataliwa na wadau, hali ambayo inaweza kuhatarisha amani ya nchi na hatimaye kusababisha mchakato mzima kurudiwa huko mbele.

Mabadiliko ya katiba ni madai ya msingi na matakwa ya lazima kama nchi hii inataka kujenga na kudumisha amani ya kweli na kuleta maendeleo kwa watu wake.

Katika mazingira ambamo wananchi wamekuwa wanalalamikia mamlaka yaliyopitiliza ya rais, kama kikwazo cha maendeleo na badiliko la msingi katika katiba, muswada wa sasa unaoletwa na serikali, unalenga kuendelea kusimika mamlaka hayo.

Uchambuzi uliofanywa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), ambaye awali ndiye alidhamiria kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusu mchakato wa katiba mpya, unaonyesha kuwa muswada huo uliochapwa katika gazeti la serikali toleo No. 1 Vol. 92 la tarehe 11, Machi 2011, unataka kumpa rais mamlaka ya kuunda tume ya kuongoza mchakato mzima wa katiba bila kuhusisha Bunge ama wadau wengine wa msingi.

Wakati wanaharakati na wananchi kwa ujumla wamekuwa wanasisitiza wananchi wawe na mamlaka ya mwisho katika kuamua hatima ya katiba yao, muswada huu wa serikali unarejesha mamlaka hayo kwa rais.

Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011 unatarajiwa kuwasilishwa bungeni hivi karibuni, na CCM kwa kutumia wingi wa wabunge wao, wanaoiunga mkono serikali hata kwa masuala wasiyokubaliana nayo, wanatarajiwa kuunga mkono muswada huo, kuhujumu mabadiliko makubwa ambayo taifa lingefanya baada ya miaka 50 ya uhuru.

Nawasilisha

Rejea thread ya Serikali yachakachua mswada wa Katiba mpya kumpa rais mamlaka ya kuunda Katiba mpya
 
Muanzisha mada napata shida kujua pointi yako. Japo unataka kujenga dhana kuwa Zitto ametoa ushawishi kuwa deni la TANESCO liahmie serikalini na lilipwe. This is too low!! kama kweli ndio ufahamu wako...na jibu rahisi simply ni vita vianavyoendeshwa dhidi ya kijana huyu...ila yoote haya ni pale alipotaka kugombea Uenyekiti.

Inaudhi sana....Kwenye kipindi cha Jambo Tanzania cha tarehe 31.3.2011 Mh! huyu alikuwepo studio na akaulizwa kuhusu hii kadhia..alichokieleza ndicho kinachoonekana kwenye barua ya mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali akimuandikia katibu mkuu Hazina. Na infact alichokieleza Zitto kwa ufasaha ni the so called ''liability contingency'' and that hizo TZS 94b zionekane kwenye vitabu vya serikali na si vya TANESCO. Sababu ni kama alivyoeleza Mdhibiti...Government was highly invloved on the signing of this Agreement btn TANESCO and RICHMOND.

Sasa jitu kuja na kuanza kuandika utumbo hapa kutaka kumtia ubaya kijana wa watu ni absolutely out of order...sh$$>>%##$*<<&^^.... Sikawaida yangu kutoa kauli hizi lakini this is too much sasa.

Shkh Yahya,
Magomeni.
 
Back
Top Bottom