Kamati ya Bunge yaijia juu serikali kuhusu kampuni ya mizigo

Morani75

JF-Expert Member
Mar 1, 2007
619
0
Duh si mchezo manake haya ndiyo yale yaliyoongelewa kule http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=8939 na sasa wameanza kukwangua hivyo nadhani hii kamati ikiwa makini itaweza angalia madudu yote yakiwamo ya mizigo kuchelewa kutolewa bandarini...... Nadhani sasa waheshimiwa kule Bungeni wameanza kuamka na "my take" ni kwamba moto lazima utawaka katika kikao kijacho cha bunge pale mjini Dom (nadhani kuanzia wiki ijayo kama sijakosea)!!!
 
Rwabugiri

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
2,777
1,195

Morani huenda uko sahihi..
Zomea zomea, na jinsi walivo ipatapata kutokana na issue ya kumfungia Zitto, nadhani wamepata somo, siamini kama tena mzee wa kasungura atawambia wafyate tena!! Huenda bunge likawa bunge tena badala ya kijiwe cha mafisadi!
 
Augustine Moshi

JF-Expert Member
Apr 22, 2006
2,390
2,000
Kuingilia jikoni: Wawakilishi wa wananchi, yaani wabunge, wamekuwa wakiambiwa kwamba hawawezi kuona na kukubali au kukataa mikataba kati ya serikali na wawekezaji kwa madai kwamba wakifanya hivyo watakuwa "wameingilia jikoni". Kuna kuuza maslahi ya taifa huko jikoni. Serikali "inalinda" kwa nguvu kabisa hali hii ya viongozi wake kuwa na mwanya wa kuuza nchi kwa maslahi binafsi.

Mkataba "umeboreshwa" kwa kuwekwa kipengele tata sana, kama wanavyosema wabunge. Nanukuu:

"……. hadaa nyingine iliyowekwa katika mkataba huo ni hatua ya kuitaka TICTS kuendelea kuendesha kitengo hicho cha makasha hadi watakapohakikisha kuwa kinakuwa na uwezo wa kupitisha makontena 600,000 ndipo makampuni mengine yaweze kuruhusiwa kuingia kwenye ushindani.

Hatujaambiwa ni makontena laki sita kwa mwezi au vipi. TICTS itahakikisha uwezo wa kupitisha hiyo idadi ya makontena haufikiwi. Wamejiwekea kipengele kitakachowaruhusu wawe na huo mkataba mpaka watakapopenda wenyewe. Na naamini watakuwa wameweka kipengele kingine kisemacho mahakama za Tanzania hazina ubavu wa kuamua lolote la kuhusu mkataba wao.

Iweje kontena lilipiwe $80 na sisi tuambulie $15 tu? Kuna mtu kasema wajinga ndio waliwao. Serikali ya CCM imetufanya tuwe wajinga waliwao na kila mgeni?
 
Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214

Mwalimu,

Kwanza naomba uelewe kwamba hiyo si Kampuni ya Kigeni ni hao hao walio serikalini na kwenye NEC ndiyo wenye hiyo Kampuni.

TICTS wamegoma kufanya kazi masaa 24 kwa kuwa wakifanya hivyo idadi ya makontena itazidi laki sita na hivyo wataingia kwenye biashara ya ushindani na wao hawataki ushindani.

Mkataba ni wa miaka 10 na sasa miaka 25, kwanini wasinunue malori ya kubeba makontena kutoka bandarini kupeleka Ubungo ambapo pia wamepewa kwa ajili ya shughuli hiyo? Hao ndio wawekezaji ambao utendaji wao umeonekana ni mzuri sana kiasi cha kuongezewa miaka 15 hata kabla miaka 5 ya mwanzo haijaisha? Hiyo review ya utendaji wa TICTS ilifanyika lini na walitumia vigezo gani???

Si waseme tu ukweli kwamba TICTS walichangia kampeni ya mgombea urais wa CCM na wakapewa nyongeza ya mkataba na kuwapa monopoly zaidi ili waendelee kuvuna hela za bure!
 
Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
12,667
2,000
Mwalimu,

Kwanza naomba uelewe kwamba hiyo si Kampuni ya Kigeni ni hao hao walio serikalini na kwenye NEC ndiyo wenye hiyo Kampuni.TICTS wamegoma kufanya kazi masaa 24 kwa kuwa wakifanya hivyo idadi ya makontena itazidi laki sita na hivyo wataingia kwenye biashara ya ushindani na wao hawataki ushindani.

Mkataba ni wa miaka 10 na sasa miaka 25, kwanini wasinunue malori ya kubeba makontena kutoka bandarini kupeleka Ubungo ambapo pia wamepewa kwa ajili ya shughuli hiyo? Hao ndio wawekezaji ambao utendaji wao umeonekana ni mzuri sana kiasi cha kuongezewa miaka 15 hata kabla miaka 5 ya mwanzo haijaisha? Hiyo review ya utendaji wa TICTS ilifanyika lini na walitumia vigezo gani???

Si waseme tu ukweli kwamba TICTS walichangia kampeni ya mgombea urais wa CCM na wakapewa nyongeza ya mkataba na kuwapa monopoly zaidi ili waendelee kuvuna hela za bure!
Kwa kutotafuna maneno ni kwamba, TICTS ni ya Nazir Karamagi na wenzake! Uchemfu wake ulianzia huku TICTS, kabla hajaingia katika madini!
 
Morani75

JF-Expert Member
Mar 1, 2007
619
0
Keil, chukua tano ndugu yangu.... Ina maan TICTS wamekataa kufanya kazi 24hrs na leo wanasema wanataka kuongeza ufanisi??? Kaazi kweli kweli hapo.... Lakini kama ulivyosema hapo juu ndugu yangu %$&#@** wamo ndani so wembe ni ule ule waliosema kwenye JF "Tunga sheria, pitisha sheria, simamia sheria, adhibu sheria" sasa umeona wapi mwalimu akajichapa mwenyewe kwa kufeli mtihani?? Mwalimu/mkubwa is always right, taka usitake lakini Yana mwisho hayaaaaaaaa..........
 
Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,699
1,225
Msiwe na Wasiwasi Saa ya Ukombozi Inakuja!!!

We are so far in the righ track!!!

Kateni issue tu!
 
mwewe

Senior Member
Jul 17, 2007
125
0
Kuna haja ya mikataba yote yenye muda mrefu ipitiwe upya. Ihusishe mambo yote yaliyopitishwa na PSRC, LART, Mashirika ya Umma na hata Wizara za Serikali.

Kuna madai kuwa mapato iliyokuwa inapata serikali kupitia Mamlaka ya Bandari wakati huo ni makubwa kuliko ka-mgao inakopewa na TICTS. Hii ni licha ya kuongezeka kwa productivity pamoja na idadi ya makonteina yanayokuwa handled. Malalamiko ya wafanyakazi wa TICTS kuhusu mishahara yao kuwa midogo kulinganisha na wale wenzao waliowaacha THA yapo na hayafanyiwi kazi.
 
Shukurani

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
253
0
Kigeugeu ni mwanachama. ni hivi huyu Mama Kilango ni mzungumzaji mzuri sana wa masuala muhimu ya nchi. Nakumbuka wakati wa mjadala wa bajeti ya wizara ya nishati na madini,aliongea kwa uchungu sana kuhusu mikataba ya madini,but lilipokuja suala la Zitto kutaka iundwe kamati ya uchunguzi na siku ile Zitto anahukumiwa bungeni,nilitegemea atasisima kidete kukutetea hoja, mbona sikuona ujasiri wake pale bungeni?kisa,masalahi ya chama. Katika hili tunahitaji kujua ni nani ambaye ametoa ruhusa ya kuongeza huo mkataba? au ni PM,maana hyu naye kwa usanii hajambo,hatujasahau ziara zake zile za kihuni pale bandarini kwenye hicho kitengo.
 
Mitomingi

Senior Member
Jan 15, 2008
130
0
Huyu baada ya kura za kijinga kwanza alisimama na kutoka nje . Spika alisema wa ndiyo waseme CCM wakasema ndiyooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo na hapana wapinzani wakasema Hapaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa lakini hawakusikika ila yeye on te spot alitoka nje
 
Augustine Moshi

JF-Expert Member
Apr 22, 2006
2,390
2,000
Noamba nionyeshe kwamba kwenye maswala ya mikataba, serikali inakiuka katiba ya Tanzania. Kwa wale wanaohitaji, katiba nzima inapatikana hapa: http://www.tanzania.go.tz/constitutionf.html

Kwanza, tuelezee kwamba Bunge la Tanzania lina sehemu mbili, kama isemavyo Ibara ya 62 ya Katiba. Nanukuu:

62.-(1) Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo
litakuwa na sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge.

Tuweke hilo maanani. Sehemu ya kwanza ni Rais, na sehemu ya pili ni wabunge. Nanukuu sasa Ibara ya 63. Nimeweka msisitizo kwenye vipengele vifuatavyo: 63.2, 63.3 (c) na 63.3 (e)

63.-(1) Rais kama sehemu moja ya Bunge atatekeleza madaraka yote aliyokabidhiwa na Katiba hii kwa ajili hiyo.

(2) Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha
Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa
niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri
ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa
majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.

(3) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge
laweza-

(a) kumuuliza Waziri yeyoyote swali lo lote kuhusu
mambo ya umma katika Jamhuri ya Muungano
ambayo yako katika wajibu wake;

(b) kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano
wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti;

(c) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda
mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa
katika Jamhuri ya Muungano, na kutunga sheria ya
kusimamia utekelezaji wa mpango huo;

(d) kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji
kuwapo sheria;

(e) kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri
ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji
kuridhiwa.

Katiba inasema wazi kwamba Bunge litasimamia serikali, na litajadili na kuridhia mikataba inayohusu Jamhuri ya Muungano. Ni wazi kwamba mikataba mikubwa ya uwekezaji inahitaji kuridhiwa. Bunge linapotaja kwamba linahitaji kupewa mkataba liujadili linapashwa lipewe mara moja, kwani kwa katiba yetu, Bunge ni msimamizi wa serikali. Serikali inavunja katiba inapokataa kufanya hivyo.
 
Morani75

JF-Expert Member
Mar 1, 2007
619
0
Kwa vile sisi ni wageni humu, na kwa vile nimeona unakuwa addressed kama "Mwalimu", naomba nifuate ada kwa kukuita "Mwalimu".

Mwalimu, hapo hiyo post yako hapo juu umefungua macho na maswali meengi sana kulingana na Bunge letu tukufu la Tanzania. Kwa vile katiba imesema, naomba niweke yafuatayo kwa wahusika kuona na ikiwezekana kutekeleza:
1. Mhe Zitto alifungiwa kwa kuhoji mikataba, hii ni kupinga haki yake ya Ibara ys 63 - yeye ni Mbunge na hivyo ni Bunge lenyewe!!

2. Mhe Slaa naye ni hivyo hivyo.

3. Kuna wakati Spika alisema kwamba kuna "issues" ambazo ni siri za serikali na sio ada kwa Wabunge kuzihoji.

Sasa kwa hayo matatu hapo juu, ni hivi:
1. Spika atumie muda katika kikao kijacho kuwaomba msamaha Wah Slaa na Zitto kwa kuwashutumu na kuwashitaki bila kutafuta ukweli halisi. Hii lazima iwe public ili wananchi na Wabunge wengine wone ili kurudisha "HONOR" (ambayo imeongelewa kwenye thread ingine huko mbele na Mkuu IDIMI) vile vile kurudisha ari ya utendaji kazi wa Wabunge wetu na kusaidia kuondoa "WOGA" ambao kwa kweli ndiyo ada ya Bunge letu la sasa!!!

2. Ile tuliombiwa na Spika na wakuu wengine kwamba kuna baadahi ya masuala ya kiserikali hayatakiwi kuwa discussed/questioned..... Sasa hapa pia Spika na Bunge ni lazima watuwekee wazi (kwani ni kupinga sheria ya kuhoji haki na mikataba as per the constituion) ni mikataba na masuala yapi hayatakiwi kuhojiwa na ni kwa sababu zipi??

Long Live JF!!
 
Augustine Moshi

JF-Expert Member
Apr 22, 2006
2,390
2,000
Kuna wakati najuiliza kama Spika na hata baadhi ya wabunge wanasoma katiba au wanaizungumzia tu hivi hivi.

Nina sababu za kudhani hata Waziri wa Sheria na Katiba hajawahi kusoma katiba yetu.
 
Nyangumi

JF-Expert Member
Jan 4, 2007
508
0
Kuna wakati najuiliza kama Spika na hata baadhi ya wabunge wanasoma katiba au wanaizungumzia tu hivi hivi.

Nina sababu za kudhani hata Waziri wa Sheria na Katiba hajawahi kusoma katiba yetu
.

Hata wabunge wenyewe hawajawahi kusoma hiyo katiba kiasi kwamba hawatambui haki zao na wajibu wao kama wabunge.Ndio sababu wanapoambiwa kuwa mikataba ni siri na si haki yao kuiona wanakaa kimya.Hawajua kuwa mwenye haki zao si EL au Spika bali ni katiba.
 
Dua

JF-Expert Member
Nov 14, 2006
3,187
2,000
Kuna wakati najuiliza kama Spika na hata baadhi ya wabunge wanasoma katiba au wanaizungumzia tu hivi hivi.

Nina sababu za kudhani hata Waziri wa Sheria na Katiba hajawahi kusoma katiba yetu.
Hapa ndipo hiki chama cha majambazi wapya wametufikisha.
 
Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,699
1,225
Kuna wakati najuiliza kama Spika na hata baadhi ya wabunge wanasoma katiba au wanaizungumzia tu hivi hivi.

Nina sababu za kudhani hata Waziri wa Sheria na Katiba hajawahi kusoma katiba yetu.
Jamii iliyoparanganyikiwa, internet forums nyingi za udaku kuliko/siasa kuliko zile za uchumi, inazaa viongozi wabovu, upinzani, uchwara, wawakilishi mbumbu, wasomi wanaohemea travel/seminar allowance, serikali dhalimu, taifa lilijengwa juu ya msingi wenye mawe kama uyoga!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom