Kamati ya Bunge yaijia juu serikali kuhusu kampuni ya mizigo
Andrew Msechu na Glory Kimathi
KAMATI ya Bunge ya Miundombinu imeitaka serikali kusitisha mara moja mkataba na Kampuni inayosimamia Kitengo cha Makontena katika Bandari ya Dar es Salaam (TICTS) ulioongezwa kabla ya kumalizika kwa mkataba wa kwanza wa miaka kumi utakaomalizika mwaka 2010.
Wajumbe wa kamti hiyo ambao ni wabunge pia wameitaka serikali kuweka wazi wamiliki wa na kujitetea iwapo haihusiki na kuongezwa kwa mkataba wa kampuni hiyo kinyume cha utaratibu.
Katika kikao cha kamati hiyo na viongozi wa Wizara ya Miundombinu na TICTS kilichofanyika Ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam jana, wabunge hao walitaka mkataba wa miaka 15 ulioongezwa kabla ya kumalizika kwa mkataba wa awali na kwamba wapewe maelezo ya kina kabla hawajaamua kupeleka hoja binafsi bungeni kuhusu utata wa mkataba huo.
Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango alisema mkataba huo uliolazimishwa kuongezewa muda wakati chama chake kikiwa katika harakati za kampeni za uchaguzi mwaka 2005 unaonyesha kukiukwa kwa taratibu na kuleta mashaka juu ya walioamua kusimamia kuongeza muda wa mkataba huo.
Alisema mkataba wa awali uliosainiwa mwaka 2000 ulishaonekana kuwa na matatizo makubwa ya kiutendaji hata kabla ya kumaliza nusu ya muda wake wa awali, uliongezwa kwa muda wa miaka mingine 15 kinyume na utaratibu na kuufanya ufikie miaka 25.
"Suala ninalogundua hapa ni ubovu wa mkataba huu, leo tuko hapa utendaji wake hauridhishi, kinachoniuma zaidi na hatua ya PSRC kutueleza wazi hapa kuwa si wao walioongeza muda wa mkataba huo kabla ya wakati, bali ni amri iliyotoka juu. Tunataka serikali iuangalie upya mkataba huu na iondoe miaka15 iliyoongezwa," aliema Kilango.
Aliongeza kuwa hadaa nyingine iliyowekwa katika mkataba huo ni hatua ya kuitaka TICTS kuendelea kuendesha kitengo hicho cha makasha hadi watakapohakikisha kuwa kinakuwa na uwezo wa kupitisha makontena 600,000 ndipo makampuni mengine yaweze kuruhusiwa kuingia kwenye ushindani.
"Tunaitegemea bandari hasa ya Dar es Salaam kuwa chanzo kikuu cha mapato ya nchi, lakini katika kipindi hiki cha utandawazi, tunaona wazi kuwa makampuni mengine yanabanwa kwa makusudi na TICTS imepewa nafasi ya kuhodhi shughuli hizi kwa kipindi kisichojulikana na zaidi kuna mianya wa mapato ya ziada, kila kontena linatozwa dola 80 za kimarekani kwa siku 19, lakini serikali hapa inapata dola 15 tu" alisema Kilango.
Mbunge wa Rorya Profesa Philemon Sarungi aliungana na Kilango akidai kuwa TICTS imepuuza kauli ya Waziri Mkuu kutaka kuondolewa kwa msongamano wa makontena kwa kufanya kazi kwa masaa 24 kwa siku zote saba za wiki, lakini pamoja na Wizara kueleza kuwa zoezi hilo limeshindikana bado wananchi hawajaelezwa.
"Sisi tunajua kuwa kauli yoyote ya kiongozi ni amri inayotakiwa kuingia kwenye utekelezaji, lakini suala la muhimu hapa tukubalaiane, tuelezwe kuwa ni lini serikali inatarajia kuupitia na kuuboresha mkataba huu wa TICTS," alisema Sarungi.
Mbunge wa Mbozi Mashariki Godfrey Zambi alisema kufuatia mazingira ya kuharakishwa kuongezwa kwa mkataba huo, mazingira yanayonyesha kuwa ni mradi wa wakubwa fulani walioamua kuhakikisha kuwa wanafanya kila linalowezekana ili uendelee kuwepo kwa muda huo, hasa baada ya kuhisi kuwa huenda wasiendelee kuwepo serikalini baada ya mwaka 2005.
"Iwapo hatutapewa maelezo mazuri na wizara hii, mimi nitakuwa wa kwanza kuikataa bajeti yake, lakini suala la msingi ni kuondolewa kwa miaka hii 15 iliyoongezwa kinyemela na tupitie upya utendaji wa TICTS, kama unaturidhisha si tutaongeza tu mkataba wana wasiwasi gani?" alisema.
Katika kikao hicho chini ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, mbunge wa Singida Kusini Mohamed Misanga, Mbunge wa Ruangwa Gogfrid Ng'itu alibainisha kuwa mkataba huo wa TICTS ni moja ya mikataba yenye utata mkubwa na kuitaka wizara kukiri kupokea barua ya kuongeza mkataba huo.
"Mkataba huu ni Richmond na Buzwagi nyingine, hili liko wazi, tumetaka sana kama wabunge tuonyeshwe mkataba huu lakini tunaambiwa kwua tutakuwa tumeingia jikoni, sasa tusipouona sisi wawakilishi wa wananchi wanataka wauone akina nani, hapo ndipo uoza unapoanzia hivyo ni lazima mikataba ya aina hii iwe wazi na sisi wabunge tuweze kuipitia na kuithibitisha katika hatua za mwanzo," alisisitiza.
Awali, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Batholomew Lufunjo aliwaeleza wabunge hao kuwa pamoja na seriali kuamua kuiongezea kampuni hiyo mkataba huo bado ipo kwenye mchakato wa namna ya kuboresha mkataba huo wa TICTS ili uwe na vigezo vingi zaidi vya utendaji ili kuongeza ufanisi.
Alipotakiwa kujibu hoja hizo alisema dhumuni la kuongeza muda huo lilitokana na utendaji mzuri wa TICTS, jibu ambalo lililopingwa na wabunge hao wakidai kuwa hakukuwa na sababu ya kuharakisha utekelezaji wa suala hilo.
Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu huyo alisema yeye hana majibu ya uhakika atakayowaridhisha wabunge hao, na kudai kuwa Waziri wa Miundombinu ndiye anayeweza kuwapa majibu sahihi.
Mkataba huo ulioanza mwaka 2000 ulitakiwa kumalizika mwaka 2010 lakini uliongezewa miaka 15 mwaka 2005, hivyo kuufanya umalizike mwaka 2025, pia kuongezewa sehemu ya kuhifadhi makontena pamoja na kupewa yadi Ubungo.
Source: Mwananchi