Kamati ya bunge yaibana Serikali; Yagomea bajeti Wizara ya Miundombinu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati ya bunge yaibana Serikali; Yagomea bajeti Wizara ya Miundombinu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 31, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  *Yagomea bajeti Wizara ya Miundombinu
  *Yadai imeshindwa kufufua TRL, ATCL


  Na Dunstan Bahai

  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imetishia kutoipitisha bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa madai kuwa wizara hiyo imeshindwa kuwekeza kwenye mashirika nyeti ambayo ni mhimili wa nchi.

  Mashirika hayo ni Shirika la Reli Tanzania (TRL), Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) na Bandari.


  Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya majadiliano ya asubuhi ya kamati hiyo, Mwenyekiti wa kamati, Bw. Peter Serukamba alisema serikali imekuwa na matumizi mengi yasiyo ya lazima lakini imeshindwa kuwekeza katika mashirika hayo na kusababisha kuelekea kufa.


  "Serikali na wizara kwa ujumla inatakiwa kuweka kipaumbele kwanza kwa mashirika haya. Haya mashirika ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa nchi, ukisema unawekeza kwenye kilimo kwanza, huwezi kufanikiwa kama huna miundombinu bora," alisema.


  Alitoa mfano kuwa ATCL ili iweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi inahitaji sh. bilioni 23 tu wakati serikali imelaumiwa kwa kushindwa kuilipia gharama za matengenezo ndege moja iliyopo Afrika Kusini ya shirika hilo, deni la sh. bilioni moja tu.


  Aidha TRL nayo inahitaji sh. bilioni 241 kulifufua shirika hilo.


  "Wanaosema serikali haina fedha siwaelewi, imekuwa na matumizi yasiyo ya lazima na kushindwa kutoa fedha kwenye maeneo ambayo yanachangia uchumi wa nchi. Lazima mashirika haya yapewe fedha vinginevyo hatuipitishi bajeti hii," alisema.


  Kwa mujibu wa Bw. Serukamba, Wizara ya Uchukuzi kwenye bajeti yake kwa fedha za ndani ilikuwa sh. bilioni 95 lakini ambazo wizara imepewa ni sh. bilioni 45 tu wakati za wahisani zilikuwa ni sh. bilioni 65, lakini zilizopatikana ni sh. bilioni mbili tu.


  Kutokana na mazingira hayo, alisema wizara haiwezi kutekeleza majukumu yake ipasavyo.


  Mjumbe wa kamati hiyo ambaye ni Mbunge wa Tunduru (CCM) Bw. Mtutura Mtutura alisema serikali inachokosea haitengi vitu ambavyo ni vya kipaumbele.


  Alisema kwa wakati uliopo sasa bandari ndogondogo sizitiliwe umuhimu kwani hazichangii uchumi wa nchi kwa kiasi
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Is that the reason Mr. Mattaka of ATC has to retire from public work?
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mbona mkuu wa kaya anaahidi Meli mpya ziwa victoria pesa za kuinunua zinatoka wapi wakati kweney wizara hakuna fungu lake
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Nadhani amesema pesa za meli sio bajeti hii ni bajeti ya 2012-2013
   
 5. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu kama hata bajeti ya mwaka jana wafadhili wametoa asilimia mbili ya kile walichopaswa kutoa hiyo ya mwaka huo au hata ya mwaka huu zitakuwepo kweli
  Kama serikali inashindwa kutoa bil moja kuifanyia matengenezo ndege ya ATCL kuna ulazima kweli au kuna uhakika na ahadi hiyo
  Kama hata serikali inashindwa kutoa kile ambacho wizara inakihitaji kuna uhakika wa kuwa na vile vilivyoahidiwa maana mkuu hiyo ni ahadi juu ya ahadi
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Wow tutaona hizo ahadi; labda atachaji makampuni ya madini ushuru more than 3%
   
 7. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  HTML:
  "Serikali na wizara kwa ujumla inatakiwa kuweka kipaumbele kwanza kwa mashirika haya. Haya mashirika ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa nchi, ukisema unawekeza kwenye kilimo kwanza, huwezi kufanikiwa kama huna miundombinu bora," alisema.
  
  Alitoa mfano kuwa ATCL ili iweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi inahitaji sh. bilioni 23 tu wakati serikali imelaumiwa kwa kushindwa kuilipia gharama za matengenezo ndege moja iliyopo Afrika Kusini ya shirika hilo, deni la sh. bilioni moja tu.
  
  Aidha TRL nayo inahitaji sh. bilioni 241 kulifufua shirika hilo.
  
  "Wanaosema serikali haina fedha siwaelewi, imekuwa na matumizi yasiyo ya lazima na kushindwa kutoa fedha kwenye maeneo ambayo yanachangia uchumi wa nchi. Lazima mashirika haya yapewe fedha vinginevyo hatuipitishi bajeti hii," alisema.
  
  Kwa mujibu wa Bw. Serukamba, Wizara ya Uchukuzi kwenye bajeti yake kwa fedha za ndani ilikuwa sh. bilioni 95 lakini ambazo wizara imepewa ni sh. bilioni 45 tu wakati za wahisani zilikuwa ni sh. bilioni 65, lakini zilizopatikana ni sh. bilioni mbili tu.
  
  Kutokana na mazingira hayo, alisema wizara haiwezi kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
  Haya sasa si tunaona kumbe tuna watu wanaojua mambo ya uchumi wamewekwa kwenye kamati badala ya mstari wa mbele huyu Mkullo is useless na chanzo cha matatizo mengi madogo madogo.

  Mtu gani anaeshindwa kusema serikali aiwezi kuendekeza mishahara ya wabunge kuwa mikubwa na marupurupu yao wakati nchi inaangamia na yenye miundo mbinu mibovu. Ni wakati wa wabunge kusema ukweli tu huyu bwana hawana imani nae tena.
   
 8. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama ana ubavu huo maana najeti tayari ishaandaliwa na wigo huo ulipaswa ujulikane mapema sio kwenda kumshtua mtu
   
 9. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  SOMA HAPA CHINI INAONYESHA NI BAJETI YA 2012-2013 AS PER IKULU

  JK: MCHAKATO WA KUNUNUA MELI MPYA UMEANZA

  [​IMG]
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa mchakato wa kununua meli mpya kwa ajili ya kusafirisha abiria katika Ziwa Victoria umeanza kwa ajili ya ununuzi wa meli hiyo.
  Rais Kikwete amesema kuwa kwa sasa wataalamu washauri wa kupatikana kwa meli hiyo, yaani Kampuni ya OSK-Ship Tech ya Denmark, tayari wamekamilisha upembuzi yakinifu juu ya aina ya meli inayofaa kwa matumizi katika Ziwa Victoria.
  Rais Kikwete amesema kuwa fedha za ununuzi wa meli hiyo zitatengwa katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/2013 baada ya kuwa maandalizi yote ya ununuzi wa meli hiyo kuwa yamekamilika.
  Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa kazi ya tathmini ya kuzikarabati meli za Mv Victoria, Mv Umoja na Mv Sengerema ambazo zote zinatoa huduma ya usafiri wa abiria na mizigo katika Ziwa Victoria umefanywa na sasa fedha zinatafutwa kwa ajili ya kuanza kazi yenyewe ya ukarabati.
  Rais Kikwete ametangaza hayo leo, Jumatatu, Mei 30, 2011, wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa eneo la Usagara, Bukumbi, Wilaya ya Misungwi, Mkoa wa Mwanza, kabla ya kuzindua rasmi barabara ya lami ya kilomita 90 kutoka Usagara hadi Geita.
  Amewaambia wananchi hao, "Kwa upande wa usafiri katika Ziwa Victoria, ninafurahi kuwafahamisha kwamba mchakato wa kununua meli mpya umeanza. Hivi sasa wataalam washauri, yaani Kampuni ya OSK-Ship Tech ya Denmark, wamekwishakamilisha upembuzi yakinifu juu ya aina ya meli itakayofaa katika Ziwa Victoria."
  Ununuzi wa meli hiyo utakuwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mheshimiwa Rais Kikwete wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana wakati alipowaahidi wananchi wa mikoa ya Ziwa kuwa Serikali yake ingenunua meli ya kusafirisha abiria ndani ya Ziwa hilo kuchukua nafasi ya Mv Bukoba iliyozama miaka 1996.
  Tokea kuzama meli hiyo miaka 15 iliyopita ambako watu wanaokadiriwa kufikia 1,000 pia walipoteza maisha, Serikali haijapata kununua meli nyingine kwa ajili ya usafiri wa abiria katika Ziwa hilo na wasafiri wameendelea kutumia meli ndogo zaidi.
  Mbali na Ziwa Victoria, Rais Kikwete pia aliahidi kununua meli ya abiria katika Ziwa Nyasa kuchukua nafasi ya Mv Mbeya iliyozama katika Ziwa hilo. Aidha, aliahidi kununua meli kwa ajili ya usafiri wa abiria katika Ziwa Tanganyika ambako meli inayosafirisha abiria ya Mv Liemba imekuwa inatumika kwa miaka 100 na imechoka na kuchakaa.
  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.
  30 Mei, 2011
  Filed under: Uncategorized | No Comments
   
 10. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Asante sana Mkuu kwa taarifa nimeiona ni ya mwaka 2012/2013
  Tatizo sio matarakimu ya miaka mkuu tatizo ni upatikanaji wa pesa
  ukisoma taarifa ya hapo juu ya Kamati inaonekana wafadhili wamegoma kutoa fungu lao na wametoa asilimia mbili sasa mkuu hizo za kununua meli mpya zitatoka wapi kama bajeti yenyewe fedha zilizopatikana ni ndogo
   
 11. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Oh yeah nimeona wafadhili wamegoma na aliahidi sio meli moja aliahidi L. Tanganyika na L. Nyasa as well na wafadhili wengi wemejiondoa

  Hii itaisumbua sana serikali ya CCM
   
 12. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #12
  May 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Si umeona mkuu mpaka serikali nayo fungu ililoahidi limepigwa panga pia hii imekaa vibaya sana na unakuta fungu lililopigwa panga ni la maendeleo sio la mishahara
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Good... & No Foreigh AID; well what will the ruling government do if their coffers are empty? Printing More Money? Selling Land to nations such as Bangladesh, South Korea n.k? OR Get ride of Shangingi's...

  “The world itself is pregnant with failure, is the perfect manifestation of imperfection, of the consciousness of failure.
   
Loading...