Kamati ya bunge ya Nishati na Madini; January Makamba atakwepaje uwajibikaji?

Na huyu malima sijui kwanini anaendelea kupeta wakati alikuwamo kwenye gemu tangu 2005. Migao ya mezani kashiriki. Ndio maana alilizwa kule moro
 
Naona January yeye hazungumziwi kabisa katika hili, so far he is walking around unscathed! Ningependa kujua yeye kama Mwenyekiti alifanya nini kuzuia au kufacilitate ubadhirifu huu?
 
Nimekuwa nikifuatilia hili kasheshe la mlungula unayoihusu kamati ya nishati na madini, lakini kitu kinachonishangaza mwenyekiti wake, January Makamba, ajaguswa kabisa. Ni dhahiri ya kuwa kama yale yanayosemwa ni ya kweli, basi Mwenyekiti naye ni guilt kwani vitu vyote vilitokea chini ya uongozi wake.

Kinachonishangaza ni kwa nini huyu mtu aguswi kabisa na vyombo vya habari? Na jee media wamepewa nini au wanaexpect nini toka kwa huyu mheshimiwa.

Itakuwa vyema kama wananchi tutaambiwa in detail ni role gani mwenyekiti aliplay katika hili sakata.
 
Naona kwenye twitter page ya January amesema kama angekuwepo bungeni hiyo kamati isingevunjwa. Ningependa kujua hii kashfa ilitokea kipindi gani? Na kama yeye angekuwepo angefanya nini haswa? It seems the guy is full of himself!
 
Ameandikwa kule twitter kwamba... "Ningekuwepo kule bungeni kamati la nishati na Madini Lisingevunjwa"

Huyu jamaa is full of himself. Mwenyekiti wa sasa hajamaliza miezi miwili, atuelzee haya madudu yake yalianza lini
 
Ngojeni Selemani (Curtis wa YA) aje humu. Huwa ana jazba jazba hivi as if ngumi anaziweza. Left hook yangu moja tu and it's lights out for him.
 
Januari hajui machungu ya maisha halisi ya vijana wa Kitanzania....
Amekuwa kwenye bahari ya maisha bora tangu akiwa mtoto, ndio maana kila kitu kwake anaona ni cha kufanyia utani tu!
Kwani yeye ni nani hadi isingevunjwa?
 
Januari hajui machungu ya maisha halisi ya vijana wa Kitanzania....
Amekuwa kwenye bahari ya maisha bora tangu akiwa mtoto, ndio maana kila kitu kwake anaona ni cha kufanyia utani tu!
Kwani yeye ni nani hadi isingevunjwa?

unajua zitto ni mtu wa kuropoka sana, alishasemaga kwamba wao wawili lazima waingie magogoni. pengine ndio maana wanajikweza sana hawa kaka zangu
 
Nyani,

Hakuna cha Selemani wala nini. Jamaa needs to explain to the public why his Kamati failed miserably to live-up to Wananchi's expectations.
 
Ningekuwa mimi ni Zitto ningetumia reaction ya tuhuma hizi iliyoonyeshwa na Wabunge siku ile, kuwa somo kwangu.

Actually, that way is a replica of how the situation will be siku atakapoharibu kwenye hizi mbio na papara zake za urais. Zitto ,the world turns against you at an angle of 180' just in a "1 millimeter" diversion from what is believed to be the social truth!

Zitto umejaliwa kipaji cha akili na upambanuzi wa masuala ya kijamii, angalia upya hizi mbio zako kinyume na taratibu za kichama!
 
Tusitegemee lolote toka ndani ya Bunge hili chafu. Kila mbunge kwenye nafasi yake, amefanya madudu, hata yule tuliyeamini kuwa msafi, naye pia kachafuka. Kila mmoja ana dhambi, hakuna aliye msafi. Nchi haina mwenyewe, sina tena Imani na mtu. Si nyinyiemu, si upinzani, wanatafuta kututafuna. hakuna cha m4c wala nini, lengo lao ni kutufanya mtaji. Nchi hii, anayependa afanye kazi, anayependa kugoma, agome, hatona dola tena.
 
naomba kama inawezekana ujibu hapahapa jf kwani itatusaidia kukuelewa vizuri.
wewe ulikuwa mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya nishati na madini kama sijakosea,sasa imejulikana mgao wa umeme ulikuwa wa kutengeneza.
sasa tutete.
1.je ulijua kama mgao wa umeme tanzania kwa miaka yote ulikuwa ni wa kutengeneza?
2.kama hukujua je unatuambiaje ili tukuelewe?

nakutakia kazi njema za ujenzi wa taifa.
 
3.Na kama alijua je alichukua hatua gani yeye kama kiongozi makini.
4. Na kama alijua hilo kwanini alikubali kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo na wakati alijua hana uwezo wa kufuatilia utendaji wa wizara hiyo?
 
Alikuwa anautafuta Uwaziri,kaupata ndio kwanza ametulia.Kazi kweli kweli!
 
Tanzania ina kazi sana kuendelea, ukitafakari kwa makini kila mtu utamuona yupo kwa maslahi yake. Na hii sio kwa wale wakubwa sana hata sisi wa chini kila mtu anawadhulumu wenzake. Anzia serikali za mitaa, njoo kwenye individual business, njoo kwenye miradi ya wafadhili malizia na serikalini. Wanapiga kelele wale ambao hawajafikiwa na ndio maana kuna kipindi ilikuwa ukipiga kelele wanakuletea data zako na wewe.
 
Mkuu Ringo endelea kupiga round huwa awajibu na wakijibu ni shutuma au kauli nyepesi nyepesi......Wacha wajipimie mwenye size ya kamba.
 
Pundamilia wote wanafanana, kasoro mistari tu. Hakuna cha chama wala upinzani, wote ni wala rushwa. ukweli utadhihirika baada ya taarifa ya tume.
 
Mimi binasfsi ninaamini kabisa kama wabunge wengi wameupata ubunge kwa rushwa ni vigumu kwao kuwajibika yao ni serikali isiyowajibika. Just imagine the hypocrisy that surrounds the whole thing. Most knew the injustice they were doing to Tanzanians but for selfish reasons they couldn't care less! Hasara zote na usumbufu wote unaosababishwa na adha ya kukosa umeme bila sababu za msingi. Waheshimiwa wabunge wetu wametufikisha hapa hakika watalaaniwa tu.

Kama wale wa CHADEMA nao walishiriki kashfa hii wafukuzwe kwenye chama mara moja ili iwe fundisho kwa wanachama wote kuwa rushwa ndani ya CDM ni MWIKO!!!. CCM waendelee na unafiki wao, dawa yao iko jikoni wananchi watawanywesha kilainiiii kwenye sanduku la kupiga kura.
 
3.Na kama alijua je alichukua hatua gani yeye kama kiongozi makini.
4. Na kama alijua hilo kwanini alikubali kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo na wakati alijua hana uwezo wa kufuatilia utendaji wa wizara hiyo?

Hiyo ndiyo CCM unafiki mtupu. Umesahau ule msemo eti chukua chako mapema?
 
Back
Top Bottom