Kamati ya bunge ya Nishati na Madini; January Makamba atakwepaje uwajibikaji? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati ya bunge ya Nishati na Madini; January Makamba atakwepaje uwajibikaji?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makame, Jul 29, 2012.

 1. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana Jamvi

  Ninasikitika sana na madudu ya TANESCO; kwa kweli Wabunge waliomuunga Mkono Waziri wa Nishati na Madini nawapa pongezi. Wabunge hawa walitoka kwenye vyama vyote; na walisimamia maslahi ya Tanzania.

  Aidha; wale waliokula fedha za wauza mafuta na kupinga hatua za Waziri wa Nishati na Madini ni wa vyama vyote. Ikumbukwe kwamba ni Waziri wa Serikali ya JK ndio aliotekeleza wajibu wa kufichua haya kwa ToRs alizopewa na Bosi wake.

  Haya ni madudu ya muda mrefu; tangu zama za Mheshimiwa William Maganga Ngeleja (Mb) akiwa Waziri wa Nishati na Madini na Mheshimiwa January Yussuf Makamba (Mb) akiwa Mwenyekiti wa Kamati. Aidha Mhe Adam Kighoma Malima (Mb) akiwa Naibu Waziri wa Ngeleja wakati huo na Bwana Davidi Kitundu Jayro akiwa Katibu Mkuu wa Hio Wizara. Hawa naamini wanapaswa kuwapatia watanzania maelezo ya kina. Aidha, ikumbukwe kwamba Mheshimiwa Amos Gabriel Makala (Mb) alikuwa Mjumbe wa kamati ya Nishati na Madini kabla ya kupewa dhamana na Mheshimiwa Rais.

  Waheshimiwa Wabunge ambao ni wajumbe Wa Kamati hio ni kama ifuatavyo:-


  1. Selemani Jummanne Zedi -----------------CCM
  2. Diana Mkumbo Chilolo ---------------------CCM
  3. Shaffin Ahmedali Sumar -------------------CCM
  4. Lucy Thomas Mayenga -------------------CCM
  5. Josephine Tabitha Changula ....................CCM
  6. Aeshi Khalfani Hillary .............................CCM
  7. Mwanamrisho Taratibu Maalim Abama ...... CHADEMA
  8. Profesa Kulikoyela Kanalwanda Kahigi ...... CHADEMA
  9. DAVID Ernest Sinde .............................CHADEMA
  10. Yusufu haji Hamisi ...............................CUF
  11. Suleiman Masoud Nchambis Suleiman .......CCM
  12. Catherine Violet Magige .........................CCM
  13. Kisyeri Werema Chambiri ........................CCM
  14. Munde Abdallah Tambwe .........................CCM
  15. Anthony Gervase Mbassa .........................CHADEMA
  16. Vicky Paschal Kamata ............................CCM
  17. Abia Nyabakari Muhama .........................CCM
  18. Mbaruku Salumu Ali .............................CUF
  19. Charles John Paul Mwijage ....................CCM
  20. Sara Msafiri Ali ...................................CCM
  21. Yusufu Abdala Nasir ............................CCM
  22. Dkt Festus Bulugu Limbu ..................... CCM ----------------Wanajamvi; huyu aliwahi kukumbwa na kashfa wakati wa Mkapa Wizara ya Fedha.
  23. Grace Sindati Kiwelu ...........................CHADEMA
  24. Mussa Hamis Silima ............................CCM
  25. Christopher olonyoike Ole Sendeka ........CCM
  26. Mariamu nasoro Kisangi .....................CCM

  Kamati ni kubwa na inajumuisha wabunge wengi. Hivi haya madudu yote yakitokea wanakamati hawana habari???
  Washazoea kwenda kula fedha za umma kwenye mashirika kwa tamaa zao; Ubunge ni kutumikia umma sio kuufisidi.

  SPIKA hana nguvu za kisheria; sana sana atavunja kamati tu.

  Hawa walaji wataendelea kupeta, tena wataendelea kuwa ndani ya Bunge letu tukufu. Refer to maneno aliyotoa Mheshimiwa John Momose Cheyo; alisikitishwa sana na hii hali.

  SOMETHING RIGHT NEEDS TO BE DONE
   
 2. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  La msingi kabisa ni kutenganisha U-CCM ; U-CHADEMA or what na maslahi ya TAIFA.

  Sera za CCM ni nzuri sana; tatizo kuna wana ccm wanaharibu image ya ccm

  Likewise CHADEMA sera zao ni nzuri lakini ...same as CCm
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kati ya hao waliochukua mlungula ni akina nani?
   
 4. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna ushahidi wa dhati kusema ni nani kachukua au nani hajachukua kwa sasa. Ila wanajulikana.

  Niseme tu

  Uanakamati goes beyond kuchukua posho.

  Tena kwa Shirika kama TANESCO, ambalo linaumuhimu na linalalamikiwa.

  Wabunge wote hao kubaini kinachoendelea wameshindwa mpaka wamsubiri Maswi?

  NA JANUARY ALIKUWA MWENYEKITI!
   
 5. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,770
  Likes Received: 6,094
  Trophy Points: 280
  Hao wa upinzani tafadhali sana watoe. Wabunge wa CCM kwenye kamati wanao wajibu wa kutuambia ilikuwaje hadi hayo yakatokea. Usishangae hata kwenye Kamati baadhi ya wabunge hasa wale wa CHADEMA walikuwa wanafichwa baadhi ya mambo. Tutasikia mengi.
   
 6. malema 1989

  malema 1989 JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 848
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  du, mie napita tu lakini hili dola linakatisha tamaa.
   
 7. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Wametajwa kuwa Ni Ole sendaka na Ruth Msafiri. hawa walikwenda kwa maswi kuomba rushwa ili kuwapoza wabunge.
   
 8. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  mambo waliyoshughulikia Waziri Muhongo na katibu Mkuu Maswi ni sehemu ya utekelezaji wa hotuba ya kambi ya upinzani iliyowasilishwa na Mhe John Mnyika mwaka jana. kama angekuwa ameshirikishwa hotuba yake ya mwaka huu ingekkuwa ya kishikaji kama ilivyokuwa hotuba ya Kamati ya Nishati na Madini, lakini katika hotuba ya kambi ya upinzani Mhe John Mnyika alipasua nondo kama alivyofanya mwaka jana ili watekelezaji wapate uwqanja mpana zaidi wa kufanyia kazi. Ndio maana ya upinzani. Mpinzani pekee aliyejihusisha na sakata hili kupitia vyombo vya habari ni kutoka Kamati ya Mashirika ya umma Mhe Zitto Kabwe
   
 9. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #9
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nadhani hapa broadly ni rushwa ya


  1. MATAIRI
  2. NGUZO
  3. MISUMARI
  4. MGAO
  5. MAFUTA

  Sio MASWI kupooza wabunge. Maswi hawezi kupooza wala rushwa kwa rushwa

   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Ruth Msafiri ni ccm?
   
 11. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #11
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  mh! hii ndiyo Tanzania na hao ndiyo wabunge wa Tanzania,tena watunga sheria ambazo wamekuwa na weledi wa kuweza kuzivunja sheria na kuweka tamaa mbele kwa maslahi ya matumbo yao,duh!Lakini bunge kama bunge haya yote yanatendeka uongozi ulikuwa wapi?

  Mh.David Kafulila aliwahi kusema wazi kuwa kuna baadhi ya wabunge katika kamati yao kipindi fulani walihongwa lakini Spika alimuona mzushi,ilipotokea TAKUKURU kumkamata mheshimiwa huyu ndo wakastuka lakini tayari mhimili huo ulikuwa umeshapata doa.Tulitegemea kama sheria inavyotaka,ukiwa mtumishi wa umma na una tuhumiwa na kesi ipo mahakamani kinachofuata ni kusimamishwa mpaka kesi itakapoisha lakini bunge letu limebaki kuwa bubu,hatusikii kauli yake,yaelekea tuhuma hizo zimetupwa kapuni.Kwa hali hiyo napata shida kuamini kama kweli nchi yetu inafuata utawala bora.
   
 12. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #12
  Jul 29, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  jamani kuna thread ilikuwa huku mwaka jana au juzi ilikuwa inamzungumzia mwenyekiti wa ccm mkoa wa mbeya Abdula aliyenunua kiwanda cha chai lupembe akawa anakata nguzo za umeme na kuzipeleka kusikojulikana na kurudishwa nchini zikiwa na nembo za afrika kusini.
  alikuwa anadai kuwa anakata kuni za kukaushia chai kupisha msimu wa mvua lakini malori yalipopigwa picha zilionekana ni nguzo za umeme.
  FUATILIENI MTAKUTA NI HIIHII SKENDO.
   
 13. b

  bdo JF-Expert Member

  #13
  Jul 29, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280

  hata mie natamani kujua nani ni nani? - maana naona maneno yamekuwa mengi sana, hivi mnyika hayupo hapo?
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Jul 29, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  sasa Zitto anahusikaje na kamati?
   
 15. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #15
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnyika ni Waziri kivuli; hayuko kwenye kamati.

  Ila anamkubali Professor Muhongo; na naamini akiambiwa kuwa MGOMBEA wa URAIS Ni Muhongo atampa kura yake na atampigia kampeni.\\

  Siasa ya Tanzania imekua mradi.

  Watu wanataka kula tu!

  Tupate majembe kama muhongo, magufuli, mwakyembe na maswi!

  Watu wapo

  hawapewi nafasi na mafisadi mpaka nao wawe mafisadi
   
 16. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #16
  Jul 29, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Nimegundua kumbe kuna watu humu wanatafuta namna ya kumchafua Mnyika kwa kuwa anasimamia haki.Hata Zitto sijamuona kwenye uzi huu nadhani ndiyo matokea ya kujenga namna ya kutafuta mazingira ya kuwachafua wanasimamia ukweli na ni siasa UCHWARA (Rostam)
   
 17. b

  bdo JF-Expert Member

  #17
  Jul 29, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280

  thanks, ila ni mapema kumwamini mtu kiasi hicho....
   
 18. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #18
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyota njema huonekana alfajiri mkubwa
   
 19. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #19
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Hazina uzuri wowote! ni sera zilizoshindwa kabisa. Matatizo yote ya kiuchumi na kijamii tuliyonayo sasa ni kutokana na sera mbovu kabisa za CCM. Acha kusifia uchafu!uchafu sio jambo la kujivunia.
   
 20. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #20
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nazungumzia SERA

  Nenda kaangalie alafu uziite uchafu

  au nitajie sera moja tu ambayo Chafu.

  TATIZO WASIMAMIA NA WATEKELEZA SERA

  January MAKAMBA anachonga sana akikamata issue

  kumbe katika uenyekiti wake naye alikua kama KABWE

  anakula na KULA tena

  watu wakifakamia namna ile lazima wapinge POSHO

   
Loading...