Kamati ya bunge - hadidu rejea issue ya Jairo

Mp Kalix2

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
5,940
3,041
Up dates:
Makinda alisema kamati hiyo itafanya kazi kwa kuongozwa na hadidu tano za rejea ambazo ni kuchunguza utaratibu uliobainika wa kukusanya fedha kwa ajili ya kukamilishwa kwa uwasilishaji wa Hotuba za bajeti za wizara bungeni na kwamba, hadidu hiyo ya kwanza itakuwa na vipengele vitatu.
Vipengele hivyo ni pamoja na kuchunguza uhalali wa utaratibu huo kisheria na kwa mujibu wa kanuni, iwapo fedha hizo huwa zinakasimiwa katika bajeti husika pamoja na matumizi halisi ya fedha zilizokusanywa.
"Hadidu rejea ya pili ni kupitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu uchunguzi alioufanya kuhusiana na agizo la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kwa ajili ya kufanikisha uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni," alisema Makinda na kuongeza:
"Hadidu rejea ya tatu ni kuchunguza mfumo wa Serikali kujibu hoja zinazotolewa bungeni na taratibu za kuarifu Bunge matokeo ya utekelezaji wa hoja hizo".
Makinda alisema hadidu rejea hiyo ya tatu ina vipengele viwili ambavyo ni kuchunguzwa kwa usahihi wa utaratibu uliotumiwa na Katibu Mkuu Kiongozi kwa suala la Jairo na kubaini iwapo utaratibu huo umeathiri dhana ya haki na madaraka ya Bunge.
Aliitaja hadidu ya rejea ya nne kuwa ni kuangalia nafasi ya Mamlaka ya Uteuzi kwa ngazi za Makatibu Wakuu katika kushughulikia masuala ya nidhamu ya anaowateua na ya mwisho inawaelekeza wajumbe wa Kamati hiyo kuangalia mambo mengine yoyote yenye uhusiano na uchunguzi huo.
Source:Raia mwema.

Nafikiri hapa ni kitovu cha fikra za maendeleo. Yawezekana kuna suala ulitaka kulisema, lakini umeshindwa kuliweka vizuri. NAKUSHAURI u-revise thread yako kuanzia kwe TITLE mpaka CONTENTS.

Sio wazo lolote linalokujia kichwani una-post hapa jamvini, fikiri kwanza

Huyo David Jairo asikae bure wkt analipwa mshahara bure, NASHAURI APEWE VIPINDI VYA HESABU KATIKA SHULE MOJA YA SEKONDARI AFUNDISHE!

sasa kama kamati inayoundwa majina yanatoka ikulu tutarajie nini hata kama watapitia michango ya humu JF?

Nafikiri hapa ni kitovu cha fikra za maendeleo. Yawezekana kuna suala ulitaka kulisema, lakini umeshindwa kuliweka vizuri. NAKUSHAURI u-revise thread yako kuanzia kwe TITLE mpaka CONTENTS.

Sio wazo lolote linalokujia kichwani una-post hapa jamvini, fikiri kwanza
Uhuru wa kutoa maoni au mawazo unao,lakini ungeonyesha wapi pana mapungufu ungeonekana wa maana na kunipa imani kuwa hilo unalo amini kuwa hapa ni Kitovu cha fikra za maendeleo na kuwa hoja ninayotaka kuijenga haina Mantiki.

Akafundishe wakati ana stress? Atawachangisha pesa wanafunzi ili watoe rushwa kufaulu mitihani. Mtoa mada rekebisha title. Lakn PM hana hoja hapo. Wakuhojiwa ni
1.Jairo
2.Luhanjo
3.Ngeleja
4.Ludovick Utou(CAG)
5.Wafanyakaz wote waliosukuma gari lake jairo.
6.Edward Hosea(PCCB)

Suala la Kamati kufanya mahojiana live mbele ya Umma itaijengea Imani kubwa Kamati na Bunge kwa ujumla wake kama wawakilishi wa kweli wa wananchi,kuliko kufanya shughuli za kuwa hoji walioshiki kwenye issue hii ya Wizara ya Madini na Nishati nyuma ya pazia, mwisho watakuja na taarifa fupi "Mengine tumeamua kuyaweka Kapuni iliwenzetu wasi Umbuke"

kazi kubwa ya kamati ni kuweka uwazi iliiaminiwe na suala la kuhoji watuhumiwa/ mashahidi hadharani ndiyo utakuwa msingi wa kuanika ukweli. Hata mahakama zinztumia utaratibu huo wa kuendesha kesi labda kuwe na sababu maalum. kwahiyo si jambo geni kwenye ufuatiliaji /utafutaji wa haki.

cdhani kama kamati hiyo itapata kitu kilicho sahihi na kutupatia

huyo david jairo asikae bure wkt analipwa mshahara bure, nashauri apewe vipindi vya hesabu katika shule moja ya sekondari afundishe!

hivi ni mtaalamu wa geometry na aljebra kumbe? Asije akawafundisha watoto 2+2=5 bure akatuharibia watoto. Akili yake imeshabobea kwenye hesabu za kifisadi.

Wacha kamati ifanye kazi yao. Tuondolee pumba hapa. Kwa hayo uliyoyaandika ndio umeona umeandika ya maana sana?

Pale bungeni kuna watu tuliowachagua na tunawaamini.

Nchi hii usishangae huku nyuma Naibu katibu mkuu wa Nishati na Madini anachangisha milioni 20 kila idara kwa ajili ya kufanya lobbying kwa kamati ya kumchunguza Jairo. Nchi hii ndivyo ilivyo. JK alishasema "Ukitaka kula shurti uliwe"

Wacha kamati ifanye kazi yao. Tuondolee pumba hapa. Kwa hayo uliyoyaandika ndio umeona umeandika ya maana sana?

Pale bungeni kuna watu tuliowachagua na tunawaamini.
Zomba bwana! kila nisomapo maandishi yako unaniacha hoi kweli kweli. Waambie mkuu, wapo watu makini na tunaowaamini mle mjengoni kama vile; Mhe John Komba, Maji Marefu (Profesa huyo), Livingstone Lusinde, Lameck Airo nk nk, maana ni wengi tuu bila kutaja vile viti spesheli.

Nawatakia kheri wanakamati wote walioteuliwa wawe wazi na wakweli Mungu awatangulie!

Huyo David Jairo asikae bure wkt analipwa mshahara bure, NASHAURI APEWE VIPINDI VYA HESABU KATIKA SHULE MOJA YA SEKONDARI AFUNDISHE!

naunga mkono hoja, ingawa utarishi ndio saizi yake.

Wacha kamati ifanye kazi yao. Tuondolee pumba hapa. Kwa hayo uliyoyaandika ndio umeona umeandika ya maana sana?

Pale bungeni kuna watu tuliowachagua na tunawaamini.

wewe zoba unajivunia mdunge kama lukuvi! eti tumewachagua! anayeweza kusema hivyo ni kiravu na hakimu makame ambao wanaandamwa na laana kama ya shetani, hata wakitubu hawasamehewi!!!!!!

"Aliitaja hadidu ya rejea ya nne kuwa ni kuangalia nafasi ya Mamlaka ya Uteuzi kwa ngazi za Makatibu Wakuu katika kushughulikia masuala ya nidhamu ya anaowateua na ya mwisho inawaelekeza wajumbe wa Kamati hiyo kuangalia mambo mengine yoyote yenye uhusiano na uchunguzi huo."Source Raia Mwema.
Kwa Mtazamo wangu hapa ndipo kwenye Shughuli kubwa ambayo kamati inatakiwa kuifanyia kazi ili pesa za walipa Kodi iweimetuka vilivyo;Tunataraji waheshimiwa hawa watazingatia na kuitumia nafasi hii adimu na muhimu waliyopewa kuimarisha Muhimili wa Bunge na Kuonyesha kuwa hii Ndiyo Taasisi yenye kusema na kuamua na Kusimamia Serikali kwa Niaba ya Watanzania kufanya hivyo itatuondolea madudu kama haya ya Kagoda,Kiwira,Radar etc.
Katika kufanya hivyo tunategemea Kamati itakuja na mapendekezo muhimu ya namna Taasisi ya Rais(Ikulu)inavyotakiwa kusimamiwa na Bunge.
Katikati kufanya hivyo tunataraji Kamati kufanya yafuatavyo;
-kuwa uteuzi wa Katibu Mkuu Kiongozi lazima uridhiwe na Bunge kama ilivyo wa Waziri Mkuu.
-kuwa uteuzi wa Wakurugenzi wote wa Taasisi ya Umma lazima uridhiwe na Bunge.Mfano PCCB,TANAPA,TRA,CAG,Jaji Mkuu,Mkuu wa Majeshi,UWT,DPP;etc
-Kuwa Utumishi wa Wateule hawa Lazima uwe wa ukomo wa Miaka Minne na Kama Bado wanahitajika taratibu za mwazo inazingatiwa upya
-Kuwa Bunge linakuwa na Mamlaka ya kupiga kura ya kutokuwa na imani dhidi ya Mteule yeyote wa taasisi ya Uraisi na kura yoyote inayozidi nusu ya Wabunge wa Majimbo inaheshimiwa .
Nawasilisha.

Back
Top Bottom