Kamati ya Bashe UVCCM kupasua jipu leo Dodoma, ripoti yasakwa ihujumiwe... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati ya Bashe UVCCM kupasua jipu leo Dodoma, ripoti yasakwa ihujumiwe...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, Jun 3, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Vigogo CCM wahaha kupata Ripoti Kamati ya Bashe

  BAADHI ya vigogo wa CCM na wale wa Umoja wa Vijana wa chama hicho, (UVCCM) jana walikuwa wakihaha kupata ripoti ya kamati iliyoundwa Machi mwaka jana kutathmini namna ya kuuhuisha umoja huo inayotarajiwa kuwasilishwa leo katika kikao cha Baraza Kuu la UVCCM.

  Taarifa kutoka ndani ya kikao ambazo zilithibitishwa na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo maarufu kama ‘Kamati ya Bashe', zilieleza kuwa vijana na vigogo wa chama hicho walikuwa na shauku ya kuiona ripoti hiyo ambayo inasemekana imesheheni mambo mazito kabla haijawasilishwa ili wajue namna ya kuizuia au kujipanga kwa kutoa maoni yao.

  Vyanzo vya habari kutoka ndani ya kikao hicho vililidokeza Mwananchi Jumapili kuwa ripoti hiyo inatarajiwa kuja na mageuzi makubwa ndani ya Jumuiya ya Vijana pamoja na CCM kwa ujumla na kwamba kutovuja kwa kilichopendekezwa humo, kumeibua maswali mengi kwa wajumbe.

  Hata hivyo, chanzo chetu kutoka ndani ya chama hicho kimedokeza kuwa moja ya mapendekezo ya kamati hiyo ni pamoja na kuutaka Umoja huo kujisimamia na kuondokana na kuwa ‘Jumuiya ya kuimba Iyena iyena.'
  Mengine ni pamoja na kuwa katika mageuzi makubwa ambapo wanataka Jumuiya ambayo italeta mabadiliko ya kiuchumi pamoja na mikakati na misimamo ya ndani ya chama ambayo kwa sehemu inawagusa vigogo.

  Pia kamati hiyo inapendekeza uchumi wa nchi kumilikiwa na wazawa yaani wananchi washiriki katika kumiliki raslimali na kwamba kazi hiyo isiachwe kwa wawekezaji wa kigeni pekee.

  Kwa mujibu wa msemaji wetu, hadi jana mchana kulikuwa na mgawanyiko wa makundi matatu katika Baraza hilo.
  Kundi moja liliongozwa na mtoto wa kigogo ambaye ni mjumbe kutoka Mkoa wa Pwani huku kundi lingine likiwa ni vijana waliotumwa na uongozi kwa ajili ya kuhakikisha wanaunasa waraka huo kabla ya kuingizwa mkutanoni leo hii.
  Kundi la tatu ni lile linalojiita ‘Wapenda haki' ambalo ndilo linalojua nini kilichopendekezwa na Kamati ya Bashe na ndilo hasa lililoonekana kuwa na furaha kubwa huku likiapa kutotolewa taarifa hiyo hadi itakapowasilishwa leo ukumbini.

  "Tumeapa na tuko tayari kuifia imani yetu, hawa jamaa hawawezi kuiona ripoti hiyo maana kuna ujanja wanataka kuufanya na kurubuni wajumbe, hivyo lazima tuwe makini na mambo hayo,'' alisema mmoja wa wajumbe.

  Kauli ya msemaji huyo haikuwa na tofauti na kauli ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bashe ambaye jana alisema kuwa hakuwa na la kusema, lakini akakiri kuwa kuna usiri mkubwa katika kamati yake.

  "Kimsingi sisi tutaiwasilisha kesho (leo) saa 9 alasiri, kwa hiyo naomba msubiri wala msiwe na haraka, ndiyo maana unaona wajumbe wa kamati yangu hawaonekani sana pale ukumbini,'' alisema Bashe.

  Bila ya kutaja nini kilichomo ndani ya ripoti yao, alisema kuwa wanaCCM na vijana watarajie kuona mambo makubwa ambayo kimsingi yatakuwa na lengo kamili la kuujenga UVCCM pamoja na CCM kwa jumla.

  MY TAKE:
  Tusubiri mpasuko mwingine UVCCM baada ya NEC yao kupasuka pia
   
 2. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #2
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Malisa amesema kuwa sasa UVCCM itaanza kujibu mapigo yote ya wapinzani maana wamechoka kuvumilia matusi ya wapinzani.
   
 3. F

  FIDO DIDO Member

  #3
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  malisa hana jeur hiyo na kund laki kujibu mapigo mkuu, watabak tu kupeawa hela na EL, alafu ujue kama viongoz wa kitaifa weng wa uvmagamba hawajui politics hata kidogo alafu n vilaza mno
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  akapake poda huko...
   
 5. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hakuna jipya. Like father like son!
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Ndio kwanza namsikia huyo malisa ataanzia wapi? Badala ya kutekeleza yale maisha bora walio ahidi wananchi yeye anasubiri kujibu mapingo kweli CCM inafuga vichaa
   
 7. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Huyo Malissa kweli fikra na akili zake ni sawa na za wengi ya wana c.c.m walivyo,hv wapinzani wanatukana au wanatoa hoja ambazo zinawagusa moja kwa moja wananchi hasa kutokana na hali halisi ya nchi ilivyo?kama ni matusi basi c.c.m wangeshnda kwa kishindo Arumeru!maisha ni magumu sana,na wananchi are feeling the pinch,inflation inatisha,rasilimali zinaporwa na kugawiwa bure tu,kwa nini wananchi wasiwaamini wapinzani kwa kuona wanawapa mwanga wa matumaini japo hawajashka dola??wananchi hawana mpango wa kusikiliza matusi na porojo,kama U.v.c.c.m wanawaza hivyo kwa nini wasianzishe kundi la taarabu tu?
   
 8. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Hawa wasipojipanga wataishia kuwa waimba kwaya wa NEC na CC kwa ujumla!!mwanzo wa mwisho wao unakaribia......hayo mapendekezo kama hawatakubalioana kuungana na kuacha tofauti zao...wana magwanda watawaapasua vichwa hadi 2015 wakiingia ikulu ndio kabisa UVnYnYM itajifia usingizini bila shida
   
 9. Jallen

  Jallen JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 497
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Mpaka ifike 2015 hakika tutaona mengi ndani ya Magamba
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kaaazi kweli kweli,,,kumbe vijana kazi yao ni ndio mzeeeee......
  Huyo mtoto wa kigogo ni nani????kutoka pwani????riz-1 nini????
  Yaani na sisiem kuna wapigania haki????na walio tayar kufa????nani asojua kuwa rasilimali not 4 us????tume kibao zimeundwa hakuna jipya hapo,,,,
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  xactly mdau
   
 12. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  'Iyena iyena'
   
 13. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #13
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  wameshasema mtoto wa kigogo na mjumbe toka mkoa wa pwani, wameshindwa nini kumalizia na jina tu maana kila kitu wameshakisema.
   
 14. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Vp wakuu hiyo report inasemaje sasa,mwenye nakala atuwekee hapa
   
 15. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  uvccm ni kama kurugenzi ndani ya wizara flani,sasa kuna kurugenzi inaweza kutoa taarifa kwa vyombo vya habari bila mtendaji mkuu wa wizara kujua?unajua maana ya kuhaha?wakiitaka taarifa wanaipata tu,asikudanganye mtu!
   
 16. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu hapo Bashe bado ana uchungu wa kuumbuliwa uraia.
   
 17. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,090
  Likes Received: 602
  Trophy Points: 280
  maneno ya kutoa tamko kila siku tumewazoea! hata ambao hatuna vyama tumezidi kujidhatiti na misimamo yetu! HATUNA VYAMA aaa SINA CHAMA NA SITAKI
   
 18. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Vipi hakuna update yoyote?
   
 19. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #19
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  yaani nazifuatilia updates bila mafanikio
   
Loading...