KAMATI ya Baraza la Wawakilishi ya Hesabu za Umma (PAC), imegundua matumizi mabaya ya Serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KAMATI ya Baraza la Wawakilishi ya Hesabu za Umma (PAC), imegundua matumizi mabaya ya Serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BabuK, Apr 19, 2012.

 1. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  KAMATI ya Baraza la Wawakilishi ya Hesabu za Umma (PAC), imegundua matumizi mabaya ya Serikali yasiyozingatia Sheria ya Fedha pamoja na Manunuzi ya Mwaka 2005 ikiwemo miradi mikubwa ya ujenzi kushindwa kufuata taratibu za fedha.

  Akiwasilisha taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu katika Baraza la Wawakilishi, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Omar Ali Shehe wa Jimbo la Chake Chake (CUF), alisema ukiukwaji huo wa sheria ya fedha pamoja na manunuzi kwa kiasi kikubwa unaitia hasara kubwa Serikali na kutoa mwanya kwa wajanja kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

  Alisema katika taasisi nyingi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hakuna daftari la kuhifadhi kumbukumbu ya mali na hivyo kujenga mazingira mabaya ya wajanja kutumia mwanya huo.

  Aidha, alisema wamegundua kuwapo kwa miradi mingi ya Serikali inayotekelezwa sasa ambayo haikufuata sheria za fedha na manunuzi na hivyo kuwapo kwa wasiwasi mkubwa wa matumizi mabaya ya fedha za umma.

  Aliitaja baadhi ya miradi hiyo ukiwamo mradi wa ushirikiano kati ya Serikali ya Misri pamoja na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) wa kilimo cha mboga ambao tayari umetumia mabilioni ya fedha huku matokeo yake yakionesha wazi wazi kutoleta tija.

  Aidha, aliitaja miradi mingine ikiwemo ujenzi wa nyumba za viongozi wakuu wa kitaifa ambao umetengewa fedha Sh 2,470,000,000,ambao kwa sasa tayari umetumia Sh 631,576,765 huku ukikiuka taratibu za fedha za manunuzi pamoja na nyumba hizo kushindwa kutumiwa licha ya kufanywa matengenezo yake.

  Miradi mingine mikubwa inayotekelezwa na SMZ ambayo Kamati imeitilia wasiwasi mkubwa ni mradi wa ujenzi wa Hospitali ya KMKM Kibweni na mradi wa ujenzi wa Makao Makuu ya JKU.

  Aidha, alielezea masikitiko yake makubwa kwa taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kushindwa kufunga hesabu zake kwa wakati hadi sasa ikiwemo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) pamoja na Benki ya Watu wa Zanzibar na Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB)
   
Loading...