Kamati ya Amani yapiga marufuku Magufuli kuitwa "Mwendazake", Wametumia sheria gani?

Kamati ya amani ya viongozi wa dini nchini imepiga marufuku, John Pombe Magufuli kuitwa "mwendazake". Mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste (CPCT), Askofu Peter Konki amesema neno "mwendazake" ni matusi makubwa kwa Magufuli na ametaka wanaotumia neno hilo washtakiwe kwani wanahatarisha aman...
Vyeo ni dhamana ,wengine wanadhani kutokana na nyanyifa zao basi wakitoa matamka yanakuwa ni sheria 'wanahitaji kurudi shule'
 
Kama kuna watu wamepigwa na njaa hizi siku 100 za kwanza za Mother ni viongozi wa dini feki, wasanii feki, wamiliki wa vyombo vya habari vya hovyo (Musiba na wenzake) na watoto pendwa wa jpm wasiokuwa na maadili (Sabaya and co). Kwa sasa wataropoka lolote ili nao waonekane, but the good thing is Mama hana shobo na wanafiki na waganga njaa. Jana kuna msanii kamsifu mother then kamwambia Mama simama watu wakuone akamgomea tena kwa kutikisa kichwa
Alifikiri Mama ni Mwendazake,eti amchezeshe singeli
 
Huyo atabaki kuwa Mwendazake tu,tusipangiane,tunajua kwamba hao ndio walikuwa waimba mapambio wake wakati watu wakiteswa na kuuawa sasa wanatafuta pa kutokea
 
Kamati ya amani ya viongozi wa dini nchini imepiga marufuku, John Pombe Magufuli kuitwa "mwendazake". Mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste (CPCT), Askofu Peter Konki amesema neno "mwendazake" ni matusi makubwa kwa Magufuli na ametaka wanaotumia neno hilo washtakiwe kwani wanahatarisha amani...
Kwanini Kamati haijadili HAKI ? Watu wanateseka bila HAKI Kamati IPO kimya
 
kwani wanahatarisha amani.
sheed.png

Tanzania ni Burdani
 
Ni vibaya kuwasema viongozi wa kiroho lakini kwa aina ya viongozi ya viongozi wasiojoelewa kama hawa hakuna namna kuwakosoa na kuwasema ya kwamba wasione aibu kuchutama ili tusiwaone utupu wao
 
47 Reactions
Reply
Back
Top Bottom