Kamati ya Amani yapiga marufuku Magufuli kuitwa "Mwendazake", Wametumia sheria gani?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,080
103,308
Kamati ya Amani ya viongozi wa dini nchini imepiga marufuku, John Pombe Magufuli kuitwa "mwendazake". Mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste (CPCT), Askofu Peter Konki amesema neno "mwendazake" ni matusi makubwa kwa Magufuli na ametaka wanaotumia neno hilo washtakiwe kwani wanahatarisha amani.

Lakini kwa mujibu wa Kamusi kuu ya Kiswahili ya baraza la Kiswahili nchini (BAKITA) toleo no.2 la mwaka 2017, neno mwendazake linamaanisha "mtu aliyekufa hivi karibuni na anaelekea kuzikwa au mipango ya mazishi yake inaendelea." Mwendazake ni kisawe cha neno marehemu ama hayati.

Je, unaamini neno mwendazake ni matusi? Je wanaomuita Magufuli mwendazake washtakiwe kama alivyoshauri Askofu Konki? Je Askofu apuuzwe, au anunuliwe Kamusi ajifunze Kiswahili?

Credit Malisa GJ

Hawa wazee kazi yao ni kupiga marufuku,au kuhamaisha amani
 
Back
Top Bottom