Kamati ya Amani yapiga marufuku Magufuli kuitwa "Mwendazake", Wametumia sheria gani?

Yawezekana aliwaulia ndugu zao. Kwani hujui kuna waliokufa au kupotea kwenye kipindi chake na hakutoa ushirikiano?
So walokufa wote ulitaka magufuli aulize kwa nini fulani kafa? Hivi mnajua kuongoza linchi kilibwa hivi lenye majizi, majambazi hivi ni kazi?

Wengine hata familia hamuwezi iongoza leo eti magufuli aache kufatilia miradi ya nchi aanze kufatilia nani kafa.

Jamani kuwa rais wa nchi sio kama mnavyoshinda vijiweni mnakunywa kahawa.
 
Kamati ya Amani ya viongozi wa dini nchini imepiga marufuku, John Pombe Magufuli kuitwa "mwendazake". Mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste (CPCT), Askofu Peter Konki amesema neno "mwendazake" ni matusi makubwa kwa Magufuli na ametaka wanaotumia neno hilo washtakiwe kwani wanahatarisha amani.

Lakini kwa mujibu wa Kamusi kuu ya Kiswahili ya baraza la Kiswahili nchini (BAKITA) toleo no.2 la mwaka 2017, neno mwendazake linamaanisha "mtu aliyekufa hivi karibuni na anaelekea kuzikwa au mipango ya mazishi yake inaendelea." Mwendazake ni kisawe cha neno marehemu ama hayati.

Je, unaamini neno mwendazake ni matusi? Je wanaomuita Magufuli mwendazake washtakiwe kama alivyoshauri Askofu Konki? Je Askofu apuuzwe, au anunuliwe Kamusi ajifunze Kiswahili?

Credit Malisa GJ

Hawa wazee kazi yao ni kupiga marufuku,au kuhamaisha amani
Waulizeni hao wanaopiga marufuku kwani mwendazake bado yupo?
 
Kumbe hata hujui maana ya marehemu, na hayati!!!!
Ila wako sahihi 'mwendazake' ni matusi, toka kuzaliwa sijawahi sikia hiyo lugha ikitumika kwa waliotangulia, kama neno lipo kwenye kamusi basi kuna wa lakini mahala, eidha kiswahili hicho ni cha nchi ya jirani na sio tanzania ama waloweka neno kwenye kamusi walikuwa wamekengeuka
Hivi unajua "Luninga" ni nini? Unajua hili nalo lilianzia nchi ya jirani? Maneno kuanzia Tanzania au nchi nyingine si hoja, kikubwa ni kupokelewa na kukubalika katika kamusi na yakatumika na jamii. Luninga liko kwenye kamusi na linatumika na jamii.
 
Mi nafikiri tumeiga kimakosa kiswahili cha kenya. Ni vyema tutumie neno marehemu. Hilo ndio neno tunatumiaga kwa kiswahili chetu.
Na Luninga unajua limetokea wapi? Sijui kwa nini neno "mwendazake" limeonekana kuwa shida. Kitendo cha kutumika kwa JPM imekua ni tatizo, huko Kenya linatumika sana tu.
 
Mwendazake ni sawa na kusema mfu au kumrejelea mtu aliyekufa. Na hili neno halijaanza kutumika baada ya kifo cha mpendwa wetu JPM. Lilikuwepo tangu zamani sana. Kukaza kulitumia ni sawa na kufikiria kulifuta kwenye kamusi ya kiswahili.
 
Kiswahili hakiongozwi na kamati kama Kifaransa.

Na hata kama kingekuwa kinaongozwa na kamati, kamati hiyo si maaskofu.
 
Locus stand wanaitioa wapi hao wafia dini
Hivi huyu malasusa na ile skendo yake na yule mama mchungaji pale Luther house imeishia wapi
 
Kamati ya Amani ya viongozi wa dini nchini imepiga marufuku, John Pombe Magufuli kuitwa "mwendazake". Mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste (CPCT), Askofu Peter Konki amesema neno "mwendazake" ni matusi makubwa kwa Magufuli na ametaka wanaotumia neno hilo washtakiwe kwani wanahatarisha amani.

Lakini kwa mujibu wa Kamusi kuu ya Kiswahili ya baraza la Kiswahili nchini (BAKITA) toleo no.2 la mwaka 2017, neno mwendazake linamaanisha "mtu aliyekufa hivi karibuni na anaelekea kuzikwa au mipango ya mazishi yake inaendelea." Mwendazake ni kisawe cha neno marehemu ama hayati.

Je, unaamini neno mwendazake ni matusi? Je wanaomuita Magufuli mwendazake washtakiwe kama alivyoshauri Askofu Konki? Je Askofu apuuzwe, au anunuliwe Kamusi ajifunze Kiswahili?

Credit Malisa GJ

Hawa wazee kazi yao ni kupiga marufuku,au kuhamaisha amani
Siamini kuwa neno mwendazake ni matusi.Pia hiyo maana ya neno hilo kutoka kwenye kamusi uliyoitaja haikidhi Magufuli kuitwa mwendazake.Hajafariki hivi karibuni(ni tangu mwezi march) ,haelekei kuzikwa(alishazikwa) na mipango ya mazishi yake haiendelei.Kwahiyo ni sahihi kusema kuwa kumuita Magufuli mwendazake ni upotofu.Pia Sio sahihi kusema neno mwendazake ni tusi....

Haya....
 
Kamati ya Amani ya viongozi wa dini nchini imepiga marufuku, John Pombe Magufuli kuitwa "mwendazake". Mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste (CPCT), Askofu Peter Konki amesema neno "mwendazake" ni matusi makubwa kwa Magufuli na ametaka wanaotumia neno hilo washtakiwe kwani wanahatarisha amani.

Lakini kwa mujibu wa Kamusi kuu ya Kiswahili ya baraza la Kiswahili nchini (BAKITA) toleo no.2 la mwaka 2017, neno mwendazake linamaanisha "mtu aliyekufa hivi karibuni na anaelekea kuzikwa au mipango ya mazishi yake inaendelea." Mwendazake ni kisawe cha neno marehemu ama hayati.

Je, unaamini neno mwendazake ni matusi? Je wanaomuita Magufuli mwendazake washtakiwe kama alivyoshauri Askofu Konki? Je Askofu apuuzwe, au anunuliwe Kamusi ajifunze Kiswahili?

Credit Malisa GJ

Hawa wazee kazi yao ni kupiga marufuku,au kuhamaisha amani
Mbona tafsiri ya kamusi inabainisha wazi kuwa 'mwenda zake' ni mtu aliyefariki karibuni na mipango yake ya maziko inafanyika.
Sasa ameshazikwa kitambo kuna haja gani ya kuendelea kutumia neno hilo 'mwenda zake?' kama si kumkejeli marehemu, jambo ambalo si uungwana kwa mujibu wa mila za kiafrika na mfundisho ya dini zetu, ambazo zinatuhimiza tuwataje kwa mambo mazuri marehemu wetu.
 
Back
Top Bottom