Uchaguzi 2020 Kamati ya amani yaazimia kuwe na siku tatu za kufunga ili kuombea uchaguzi upite kwa amani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,864
Kamati ya amani na dini mbalimbali Mkoa wa Singida inayojumuisha viongozi wa madhehebu na dini zote imetoa tamko lenye maazimio saba kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu huku ikiwaomba waumini wao kumtanguliza Mungu na Serikali kusimamia amani na utulivu ili kuwapata viongozi bora watakaoingoza nchi katika miaka mitano ijayo 2020 hadi 2025.

Akisoma maazimio hayo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Shehe, Hamis Muhamed Kisuke amesema miongoni mwa maazimio hayo ni kuwaomba waumini wao kutenga siku tatu kuanzia Ijumaa hadi Jumapili ya juma hili kwa ajili ya kufunga na kuomba ili kuombea uchaguzi upite kwa amani na usalama.

Maazimio mengine yaliyofikiwa kwenye kikao hicho ni pamoja na viongozi wa dini katika kipindi hiki kudumisha Amani, kutotumika kwenye majukwaani ya siasa kushabikia viongozi wa vyama vya siasa, kuhubiri Amani, kuhimiza waumini wao kushiriki kupiga kura na kuhimiza kufuata na kutii sheria za nchi ambapo pia wamesisitiza kuviacha vyombo halali vilivyopewa dhamana ya kusimamia uchaguzi huo vifanye kazi yake.

Mwakilishi wa dini ya Kiislam (Baraza la Kiislam Tanzania) katika Mkoa wa Singida Shehe, Issa Nassor amesema Amani ikitoweka watakaoumia zaidi ni watoto, wanawake, wajawazito, wazee na watu wenye mahitaji maalum kwa kuwa hawana uwezo wa kukimbia na kujitetea.

Aidha, wamewataka wazazi na walezi wa kila familia kuwaasa vijana kujiepusha na kushawishiwa na watu wanaoitakia mabaya nchi ya Tanzania ambapo ameongeza kwamba baada ya kupiga kura vijana warejee nyumbani kwa kuwa tayari Serikali imeshaweka vyombo maalum kwa ajili kuhesabu na kutangaza matokeo hayo.

“Historia inaonyesha kuwa nchi zote duniani zilizopoteza amani ni nchi ambazo walilewa amani, vilevile tukumbuke kupata amani ni mchakao wakati kuvunja amani ni jambo rahisi kabisa. Nawaomba watanzania wenzangu kutumia vipande vyetu vya kupigia kura kuwachagua Viongozi bora.” aliongeza Shehe, Nassor

Mwakilishi kwa upande wa wakristo, Askofu wa Kanisa la TAG mkoani Singida, Gasper Mdimi amesema amani ya nchi ni jambo nyeti ambalo linatakiwa kuchukuliwa kwa uangalifu mkubwa kwa kuwa lina athari pana kuanzia kwenye ngazi ya kaya hadi taifa kwa ujumla na kwamba Bibilia imefafanua kuwa chanzo cha Amani ni Mungu mwenyewe, Haki na Watu wanaomcha Mungu.

Amefafanua kuwa vitabu vyote vitakatifu vinasisitiza kutafuta kuwa na amani na watu wote ambapo na kwamba watanzania wanatakiwa kupendana katika kipindi hiki bila kuangalia vyama vyao vya Siasa na kuiombea nchi yao ipate viongozi ambao watailinda amani.

Pia amesema wakati wananchi wanakwenda katika siku za mwisho wa kuhitimisha zoezi la kuwachagua viongozi ni muhimu kuzingatia kuacha kuongea maneno ambayo yatasababisha machafuko na uvunjifu wa amani.

Mwakilishi wa Mhashamu Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Singida, Padre Padri Elia Mnyakanka amesema Uongozi Bora ni tunu na zao la amani na kwamba ili kuwa na maendeleo na ustawi kuanzia ngazi ya familia na taifa ni muhimu kwa wananchi kutafakari kwa kina na kuwachagua viongozi wanaoweza kuilinda amani.

Akitoa mfano amesema katika taifa la Israel uongozi bora ulikuwa ni nyenzo ya kuwafikisha kwenye nchi ya ahadi kupitia manabii mbalimbali ambapo kwa kufanya hivyo amani ilipatikana.

Amesema viongozi wa dini wanapaswa kuwapa elimu ya uraia waumini wao ili kuwapa uwezo wa kuwachagua wagombea makini kupitia ilani zao ambapo amesisitiza kwamba uchaguzi wa haki na amani ndiyo njia pekee ya kujitawala na kuleta amani katika nchi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike amesema kwenye kipindi hiki cha uchaguzi majukumu yao ni pamoja na kutunza na kudumisha Amani, kusimamia utekelezaji wa sheria, kuzuia na kubaini makosa ya jinai, kuwakamata wahalifu wanaohatarisha amani na kuwafikisha katika vyombo vya sheria, kulinda mali za raia, kutoa ulinzi kwa maafisa na vituo, pia kuhakikisha hakuna mtu anaye watishia wapiga kura na kuhakikisha usalama wa vifaa vya kupigia kura.

Mkuu wa Mkoa Singida Dkt.Rehema Nchimbi amewashukuru viongozi hao kwa kuandaa mkutano huu ambao umelenga kudumisha amani na kuwahimiza wananchi washiriki kikamilifu kupiga kura ili kuwa chagua viongozi bora.

Aidha Dkt.Nchimbi amewataka Viongozi wa Dini kutotumika kuharibu amani na mshikamano ambao upo kwa kipindi kirefu sasa hapa nchini kutokana na kazi nzuri ya kusimamia amani hiyo iliyofanywa na Serikali.
 
Watanzania kwa kutafuta kiki hatujambo atakaevunja amani ni nani hadi wakae waiombee?!?!...wao waombee haki itendeke ili amani isivunjwe,unaombeaje outcome badala ya tatizo,na nyie viongozi wa dini ndio mmejaa unafiki kweli awamu hii!

OMBEENI HAKI SIO AMANI!
 
Sisi tuko kwenye mfungo wa siku 15 uliotangazwa na Mwalimu Mwakasege na tumeanza juzi 21 October kwa ajili ya kuombea uchaguzi!
 
It's very simple. Ukiona watu wanaongelea sana amani amani na hawataji haki ujue hao sio watumishi wa Mungu ila ni wachumia tumbo tu.

Wao wanataka amani iwepo lakini bila haki maana yake hicho ndicho mlipaji wao ccm alichowambia waseme.
 
Hii ni mikusanyiko ya majitu majinga tu, makhanisi tu. They never, NEVER, NEVER talk about HAKI, HAKI HAKI. Yanaongelea Amani wakati amani ni PRODUCT YA HAKI. Kama kuna HAKI huna hata haja ya kuomba. nan atafanya fujo wakati haki imetendeka? HUWEZI KUPATA MIMBA BILA FERTILIZATION.
 
Tumefika hapa kutokana na watu waliopewa kuongoza wakageuka watawala sasa wawaambie warudi kwenye uongozi sio utawala mambo yatarudi kama zamani
 
Ni mambumbumbu!Amani itapatikana kupitia uchaguzi wa huru na haki.Sasa unapiga watu mabomu,unaweka vituo bubu/hewa vya kupigia kura kila mahali kwenye nchi hii, unatumia TISS kuchakachua kura, unajaza majina hewa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura,unakataa kuapisha mawakala e.t.c halafu unaombea amani?!Hiyo ni akili au ni matope?Mungu gani atasikiliza maombi ya kifala kama hayo?
 
Hivi hizi sijui kamati mara mabaraza mara majukwaa mara makanisa mara misikiti nk wanasema kuombea uchaguzi wa amani ni katika misingi ipi hasa.

Wawezaje kuombea wasafiri safari njema huku unashughudia magurudumu ya chombo chao cha usafiri yenye vipara au yenye nati za hapa na pale tu?

Huyo unaye muomba amani hakuoni kituko?
 
Hao mashetani wakaombee familia zao watuache Mungu wa mbinguni pekee ndio atasimama na watz hao wanafiki waombee familia zao
 
Ahsante kamati ya amani. Nitaungana pamoja nanyi. Mim siku hizo tatu nitasoma zaburi 109. Siku zake anayepanga kuiba kura, kuchakachua matokeo, kuongeza vituo hewa na wapiga kura hewa na mambo yasiyo ya haki, SIKU ZAKE ZIWE CHACHE. Naomba na wapenda amani wote waungane pamoja nami na pamoja na kamati hiyo. Sisi tusome zaburi 109
 
Watanzania nadhani kuja haja ya kusali pamoja na viongozi wetu na tukumbuke kuna maisha baada ya uchaguzi
 
Back
Top Bottom