Kamati ya Amani ya Maaskofu na Mashekhe yamuonya Askofu Gwajima

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Kamati ya Kitaifa ya pamoja kwa Maaskofu na Maashekhe ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini Tanzania imemkemea Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kutoana madai ya kusambaza kipeperushi na sauti kwa lugha ya kisukuma chenye lengo la kuhamasisha watu kuunda kikundi cha kikabila nchini.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Machi 05, 2020 na mwenyekiti wa kamati hiyo, Askofu William Mwamalanga imesema kuwa viongozi hao wa dini wanaungana na na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam lililompa askofu huyo onyo kwa kuwa ukabila ni dhambi hatari ambayo inapanda chuki ndani ya jamii na ni chukizo mbele za Mungu.

Kamati hiyo imesema kuwa kitendo hicho kinapaswa kudharauliwa na kila Mtanzania na imelipongeza jeshi la polisi kwa kumpa onyo Askofu Gwajima.

“Ndani ya jamii zetu mijini na vijijini kuna vikundi mbalimbali vya kimaendeleo vinavyoshirikisha makabila mbalimbali hutajawahi kuona polisi wanavikamata kwa kujiunga kwao bila shaka hili la Askofu Gwajima Polisi hawajakosea,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Gwajima alipewa onyo na Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam baada ya jeshi hilo kujiridhisha na kosa la kusambaza kipeperushi na sauti kwa lugha ya kisukuma zenye lengo la kuhamasisha watu kuunda kikundi cha kikabila nchini.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo limesema kabla ya Gwajima kupewa onyo walimhoji na baadaye kumuonya kuacha mara moja vitendo vya kuligawa Taifa kwa kutumia vigezo vya ukabila

Kipeperushi hicho chenye picha ya Rais John Magufuli kimesambaa kwenye mitandao ya kijamii kikiwa na maandishi yanayosomeka kwa lugha ya kisukuma.

Pamoja na kipeperushi hicho, inadaiwa Askofu Gwajima pia alitoa ujumbe wa sauti wenye ujumbe wa kumpongeza Rais Magufuli na kuhamasisha wasukuma kurejesha utamaduni wao wa zamani wa kutumia lugha yao, kusaidiana katika shida na raha.

Chanzo: Mwananchi
 
Huyu naye alikuwepo ?
1660090_FB_IMG_1514731600839.jpg
 
kwani Gwaji alikula maharagwe ya wapi wakati akiandaa haya mambo ya ukabila?
 
Wewe mpuuzi kweli,wasukuma peke yao na kwa umoja wao wanao uwezo wa kupiga kura na kumpitisha raid,eti mwisho kuwapa madaraka, poor
Wewe soma vizuri kwanini huyu askofu amefanya makosa makubwa acha kupotosha watu. Ukabila wa wasuk umesambaa kila mahali na ni hatari kwa ustawi tuliojijengea tangu awali. Ni mwisho kuchagua kutoka huko...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gwajima anatumika tu kukamilisha mpango wa jiwe.....yeye alisewa watu wa kaskazini hii sio zamu yao alafu akabomolea watu hovyo maeneo memngi lkn alipofika mwanza alisema hawa ndo walionipa kura......Unajua jiwe anamipango mingi sn mibaya kuhusu hii nchi ndo maana kila ziara ni mwanza chato...................chato chato chato.....anataka kupeleka hata mlima kilimanjaro chato
 
Back
Top Bottom