Kamati Teule ya Richmond ilitumia sh 400 milioni?!!

Niliposoma kichwa cha Post hii nilidhani hizi Tsh 400 milioni zilipewa Mwakyembe na fisadi mmoja ili asiandike kwa ukali sana ripoti yake. Kumbe hizi Tsh 400 milioni ni fedha Kamati ya Mwakyembe ilizotumia kukamilisha Ripoti.

Hii Kamati si ilikwenda mpaka Merikani kuthibitisha non-existence ya Richmond?

Naweza kushauri wanaJF, kama Waziri wa Fedha mstaafu aliyependa kubana sana matumizi ya fedha za walipa kodi, kwamba kwa viwango vya sasa, Kamati ya Mwakyembe haikufuja fedha. Tujadili mambo muhimu zaidi.

- Mzee heshima ikufikie popote ulipo, maneno yako ni mazito sana na ubarikiwe.

Respect.

FMEs!
 
Niliposoma kichwa cha Post hii nilidhani hizi Tsh 400 milioni zilipewa Mwakyembe na fisadi mmoja ili asiandike kwa ukali sana ripoti yake. Kumbe hizi Tsh 400 milioni ni fedha Kamati ya Mwakyembe ilizotumia kukamilisha Ripoti.

Hii Kamati si ilikwenda mpaka Merikani kuthibitisha non-existence ya Richmond?

Naweza kushauri wanaJF, kama Waziri wa Fedha mstaafu aliyependa kubana sana matumizi ya fedha za walipa kodi, kwamba kwa viwango vya sasa, Kamati ya Mwakyembe haikufuja fedha. Tujadili mambo muhimu zaidi.

Mh. Edwin Mtei
Tunashukuru sana kwa ushauri.......kwa walio na macho na wasome waelewe........
 
Niliposoma kichwa cha Post hii nilidhani hizi Tsh 400 milioni zilipewa Mwakyembe na fisadi mmoja ili asiandike kwa ukali sana ripoti yake. Kumbe hizi Tsh 400 milioni ni fedha Kamati ya Mwakyembe ilizotumia kukamilisha Ripoti.

Hii Kamati si ilikwenda mpaka Merikani kuthibitisha non-existence ya Richmond?

Naweza kushauri wanaJF, kama Waziri wa Fedha mstaafu aliyependa kubana sana matumizi ya fedha za walipa kodi, kwamba kwa viwango vya sasa, Kamati ya Mwakyembe haikufuja fedha. Tujadili mambo muhimu zaidi.

Kwa maneno haya....nadhani sifai kuwa Waziri wa Fedha. Maana nilivyo mbahili wa pesa za Umma, hiyo million 400 wangeharisha kwanza kabla ya kuipata...hahahaha
 
Naona wote mmechangia kuhusu milioni 400 - kama zilikuwa na tij au la.

Swali muhimu ni kwamba,kwanini walificha vielelezo wakati ule, jambo ambalo lingerahisisha maamuzi yakichukuliwa kwa wakati mmoja na ya uhakika. Issue ni kwamba walitumia pesa za umma and then wakaficha vielelezo vingine ambayo ilikuwa so unprofessional.

Wazalendo halis,

Kwa kifupi,

"vielelezo vyote na taarifa yote ya Richmond ni copy right ya Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."

Yeyote anayetumia vielelezo hivyo kwa maslahi yake, ya ndugu yake, jamaa yake, chama chake, serikali yake nk. Anavunja sheria ya Interlectual Property kwenye kipengele cha Copy Right.
 
Niliposoma kichwa cha Post hii nilidhani hizi Tsh 400 milioni zilipewa Mwakyembe na fisadi mmoja ili asiandike kwa ukali sana ripoti yake. Kumbe hizi Tsh 400 milioni ni fedha Kamati ya Mwakyembe ilizotumia kukamilisha Ripoti.

Hii Kamati si ilikwenda mpaka Merikani kuthibitisha non-existence ya Richmond?

Naweza kushauri wanaJF, kama Waziri wa Fedha mstaafu aliyependa kubana sana matumizi ya fedha za walipa kodi, kwamba kwa viwango vya sasa, Kamati ya Mwakyembe haikufuja fedha. Tujadili mambo muhimu zaidi.
Kumradhi wakuu, naona mods waliiunganisha hii na zile nyingine ambazo ni related na mgongano wa Mwakyembe na TAKUKURU bila kujua hii ni over Richmond (another move anyway)...

Mzee wangu Mtei, karibu tena jamvini kutupa busara zako, kumradhi kuwa fonts zangu muda mwingi ni ndogo lakini naamini miwani inatosha kusoma ninachoandika.

Wakuu, nasikia kama nilivyosema jana ndivyo alivyokuja kiongozi wa Upinzani Bungeni kwa kushauri kuwa hii move sasa iende mbele zaidi, safari za JK na gharama zake kwa serikali yetu sasa vianze kuhojiwa na viwekwe bayana, gharama zote wanazotumia mawaziri wote wa serikali ziainishwe ili tujue kuwa wako wasafi.

Na nasikia hata mbunge mwingine wa CCM kasisitiza kuwa kabla ya kuanza kuvurumshana na wabunge washughulikiwe wa Kagoda, Deep Green Finance na Meremeta kisha tukabiliane na wabunge...!

Nice move anyway...
 
Wazo la kutoa ziiiiiiiiii as opposed to thanx lianzie kwenye hii thread, inaonyesha chuki binafsi kuanzia kwenye title. Ile ilikuwa kamati maalumu ya bunge why pick on an individual. Kwa wote wanaoona hii thread inastahili ziiiiiii waanze kusema hapa.
 
Tanzania ni Nchi na sio NGO

Kamati ya bunge ya kuchunguza kampuni ya kufua umeme, Richmond, ilitumia kiasi cha shillingi za Tanzania zisizopungua millioni 400.

Vyanzo vya uhakika kutoka hazina vimethibitisha kuwa, kiasi hicho kikubwa cha pesa za wakipa kodi zilitumika kwa kusudi la kuwezesha uchunguzi makini na kamilifu ili haki iweze kutendeka.

Baadhi ya maofisa wa serikali wamesema wanashangazwa sana na habari kuwa, baada ya kutumia pesa hizo zote, kamati hiyo ilishindwa kukabidhi vithibitisho kamili kwa wakati mmoja na badala yake, wanasema leo kuwa walificha vielelezo ambavyo wameanza kutoa katika vyombo vya habari.

Wataalamu wanasema, hatua hii ni kinyume cha sheria kwa sababu vithibitisho vyote ni mali ya bunge iliyoagiza uchunguzi huo, na kwa wanakamati kutokabidhi nyaraka zote ni ishara kuwa walishindwa kukamilisha kazi waliopewa.

Pia, hatua hizi zinaonyesha kuwa, wanakamati walikuwa na agenda binafsi kwa kuchagua kipi cha kuorodhesha na kipi cha kuficha.

"Duniani sehemu zote, ukikabidhiwa kazi ya uchunguzi wowote na kilipwa kwa kazi hiyo, unatakiwa kukabidhi yote uliyoyathibitisha. Kushikilia vielelezo kadhaa ili uje kuyatoa kwa sababu zako binafsi ni kosa kubwa na kamwe haiwezi kuhalalishwa kwa kigezo cha maslahi ya umma," alieleza mtaalamu na kuongeza kuwa, kama maslahi ya umma yangezingatiwa, basi ripoti kamili ingetolewa wakati huwo wa kuwasilisha ili maamuzi kamili yachukuliwe.

Malumbano ambayo hayana tija kuhusu suala la Richmond na ambayo yanaendelea kupoteza wakati na akili za watanzania leo yamekithiri katika vyombo vya habari. Wakati nchi inaelekea uchaguzi, badala ya kuweka kipaumbele kuzungumzia habari zinazowasumbua wananchi kama huduma za elimu, afya n.k, vyombo vya habari vinaendeleza poroja za wanakamati wa Richmond.

Wanakamati hao wanatakiwa kushtakiwa kwa kushindwa kukabidhi vielelezo vyote vya uchunguzi walioufanya kwa pesa za wananchi. Kwanza, hawakuwatendea haki wananchi kwa kutumia hela hizo zote na kutokamilisha ripoti yao. Pia, eti walishikilia vielelezo hivyo ili waje watoe baadae. Je sababu ni nini? Ili kuwasaidia kisiasa? Hapo hawajawatendea haki wananchi.

Pia, kuzitoa habari walizopata kwa kutumia pesa za umma kwa vyombo binanfsi vya habari ni kosa la jinai.

Wasomi wanasema milioni hizo 400 zingeweza kununua genereta na wananchi wasingeendelea kuwa gizani leo. Kwa uzembe wa kamati hiyo, wananchi wako gizani kwa kutokuwa na umeme leo, na pia wako gizani kwa kutojua ukweli kamili wa waliyojia katika ufatiliaje kamili wa Richmond.

"Ni upumbavu mtupu,hatuitaji maelezo mengine tunachoitaji ni waliousika na richmond wawajibishwe basi.Suala la mil.400 hatutaki kulisikia,hata angepewa bilion 1, tunaitaji kujua muhafaka wa richmond.
 
Huyumtoa mada kwanza atwambie yeye kapewa milioni ngapi ili aje hapa JF abandike upumbafu wake hapa. kama ni lowasa amekutuma....... hapo umechemka (nanukuu mama sofia simba).
 
Kwani kamati ya jaji bomani ilitumia shs ngapi?? hawa mafisadi na makuwadi wao wana tapatapa sasa
 
Tanzania ni Nchi na sio NGO

Kamati ya bunge ya kuchunguza kampuni ya kufua umeme, Richmond, ilitumia kiasi cha shillingi za Tanzania zisizopungua millioni 400.

Vyanzo vya uhakika kutoka hazina vimethibitisha kuwa, kiasi hicho kikubwa cha pesa za wakipa kodi zilitumika kwa kusudi la kuwezesha uchunguzi makini na kamilifu ili haki iweze kutendeka.

Baadhi ya maofisa wa serikali wamesema wanashangazwa sana na habari kuwa, baada ya kutumia pesa hizo zote, kamati hiyo ilishindwa kukabidhi vithibitisho kamili kwa wakati mmoja na badala yake, wanasema leo kuwa walificha vielelezo ambavyo wameanza kutoa katika vyombo vya habari.

Wataalamu wanasema, hatua hii ni kinyume cha sheria kwa sababu vithibitisho vyote ni mali ya bunge iliyoagiza uchunguzi huo, na kwa wanakamati kutokabidhi nyaraka zote ni ishara kuwa walishindwa kukamilisha kazi waliopewa.

Pia, hatua hizi zinaonyesha kuwa, wanakamati walikuwa na agenda binafsi kwa kuchagua kipi cha kuorodhesha na kipi cha kuficha.

"Duniani sehemu zote, ukikabidhiwa kazi ya uchunguzi wowote na kilipwa kwa kazi hiyo, unatakiwa kukabidhi yote uliyoyathibitisha. Kushikilia vielelezo kadhaa ili uje kuyatoa kwa sababu zako binafsi ni kosa kubwa na kamwe haiwezi kuhalalishwa kwa kigezo cha maslahi ya umma," alieleza mtaalamu na kuongeza kuwa, kama maslahi ya umma yangezingatiwa, basi ripoti kamili ingetolewa wakati huwo wa kuwasilisha ili maamuzi kamili yachukuliwe.

Malumbano ambayo hayana tija kuhusu suala la Richmond na ambayo yanaendelea kupoteza wakati na akili za watanzania leo yamekithiri katika vyombo vya habari. Wakati nchi inaelekea uchaguzi, badala ya kuweka kipaumbele kuzungumzia habari zinazowasumbua wananchi kama huduma za elimu, afya n.k, vyombo vya habari vinaendeleza poroja za wanakamati wa Richmond.

Wanakamati hao wanatakiwa kushtakiwa kwa kushindwa kukabidhi vielelezo vyote vya uchunguzi walioufanya kwa pesa za wananchi. Kwanza, hawakuwatendea haki wananchi kwa kutumia hela hizo zote na kutokamilisha ripoti yao. Pia, eti walishikilia vielelezo hivyo ili waje watoe baadae. Je sababu ni nini? Ili kuwasaidia kisiasa? Hapo hawajawatendea haki wananchi.

Pia, kuzitoa habari walizopata kwa kutumia pesa za umma kwa vyombo binanfsi vya habari ni kosa la jinai.

Wasomi wanasema milioni hizo 400 zingeweza kununua genereta na wananchi wasingeendelea kuwa gizani leo. Kwa uzembe wa kamati hiyo, wananchi wako gizani kwa kutokuwa na umeme leo, na pia wako gizani kwa kutojua ukweli kamili wa waliyojia katika ufatiliaje kamili wa Richmond.

ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
- Mkulu joka, hapa sasa tupo pamoja sana tuichukulie hii ishu kama changamoto ya kuangalia madudu ya matumizi ya hela zetu serikalini, hiyo Ngurudoto yenyewe ni suspect pia maana inajengwa chapu chapu mara moja na inaanza kuchukua tenda zote za serikali za mikutano, hivi kweli unafikiri hakuna mikono mizito hapo?

Respect.

FMEs!

Ngurdoto = JK + Lowasa
 
Hivi zile semina za ngurdoto, kwenye mawizara zimeleta matunda gani????
 
Wazalendo halis
Junior Member
red_left.png
red_right.png
green_left.png
green.png
green_right.png
Join Date: Fri Oct 2009
Posts: 3
Thanks: 0
Thanked 3 Times in 1 Post

Hii inaonyesha huyu jamaa ni pandikizi humu JF tafadhali mods delete huyu mtu.
 
kama mil 400 kwa kazi waliyofanya ni nyingi, je ni kiasi gani kingetumika?
wakati unataja ufikirie hivi vitu;
idadi ya watu kwenye tume na mda tume iliyotumia
nauli
kukaa hoteli
kuwahoji watu
ku obtain information (watu wengine hawakupi info bure)
vikwazo walivyokutana navyo.

note: mil 400 imesababisha lowasa, msabaha, karamagi kuondolewa
 
Lakini mkuu milioni 400 ni lundo la hela, kwa kazi gani hasa walioifanya? Wakati mwingine hawa vinara wetu wa vita dhidi ya ufisadi wanajipiga bao mwenyewe. Milioni 400, posho mbilmbili, ebo!

Alishatuasa Katibu Mkuu wetu Dk Slaa kuwa hii vita dhidi ya ufisadi inahitaji sifa moja kubwa, nayo ni: unyoofu. Sasa hawa wenzetu kila siku wanapoteza sifa za kuwa majemadari wa vita hii. Tutayajua mengi huko tuendako!

Kitila mie kila kona hapa utaona nilikataa upambanaji wa akina Mwakyembe . Majina yao daima ni tata , wapambanaji , Chama cha Mapinduzi , ukiuliza mlimpindua nani hakuna kitu . Hawa wote ni kapu la wajanja wana ajenda ya kuutaka uongozi tu hakuna zaidi .
 
pamoja na hayo mkuu Lunyungu, bado tume ya akina mwakyembe na wenzake kuhusu richmonduli ilifanya kazi nzuri hivyo wanastahili kupongezwa na pesa waliyotumia ni halali na haki yao.

ingekuwa serikali imetekeleza ilicho agizwa na bunge tunge sema ni halali kwa hayo yanayoendelea ya kuwahoji lakini kwa nini serikali imeshindwa kutekeleza maagizo ya bunge na inageukia wabunge wale wale wanaoisulubu bungeni??
 
So what?...
Ama kweli Mafisadi huja na mbinu za kila aina...

Hili Sakata la Richmond bado ni ngoma nzito sana. Tusubiri Mwakyembe naye aibuke na yale ambayo hakuyaweka kwenye ripoti ile kwa kudai yalikuwa mazito zaidi. Kweli nchi yetu imeshikwa na mafisadi na wameing'ang'ania vya kutosha ili kuendeleza ufisadi wao...Duh! hii inatisha sana!
 
sawa milioni 400 zaweza kuwa si nyingi kwa kazi kamati iliyofanya, lakini tusiifumbie macho, kamati haikutekeleza kazi iliyotakiwa kufanya

haikutwambia richmond ni nani,
 
Back
Top Bottom