Kamati Teule ya kuchunguza Uhujumu Uchumi... Wizara ya Utalii na Maliasili, Mh PAMBA hapana! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati Teule ya kuchunguza Uhujumu Uchumi... Wizara ya Utalii na Maliasili, Mh PAMBA hapana!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mr. Clean, Nov 24, 2011.

 1. M

  Mr. Clean Senior Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 195
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jana Katibu wa bunge katangaza majina ya Kamati teule ya bunge kuchunguza uuzaji wa wanyama hai / usifisadi katika Wizara ya Maliasili na Utalii.

  Ndanimo yupo Mbunge wa mafya ccm kama mwenyekiti pia mjumbe mmojawapo ni Mh. SALEHE PAMBA mbunge wa Pangani ccm.

  Hofu yangu ni kuwa:
  kumbukumbu zangu zanaonesha ndani ya kipindi cha JK kama rais,
  Mh. Salehe Pamba alishakuwa Katibu tawala wa mkoa, pia alikuwa KATIBU MKUU wizara ya Maliasili na Utalii enzi za Waziri Zakia Mengji, sasa kuwepokwake kwenye kamati ya kuchunguza ufisadi aloufanya yeye mwenyewe ndani ya wizara hiyo TUTARAJIE NINI? USANIIIIIIIIIIIII>>>>>>in ACTION!
   
 2. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Hii taarifa ni ya kweli au? Lini hayo maazimio ya kuundwa kamati teule yalifikiwa bungeni? Hebu niweke sawa hapo kabla ya kuchangia.
   
 3. M

  Mr. Clean Senior Member

  #3
  Nov 24, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 195
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  [TABLE="class: MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD]Kamati kuchunguza ufisadi maliasili yapewa hadidu rejea
  [/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]Wednesday, 23 November 2011 20:34
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  James Magai
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  BUNGE limetoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Kamati Ndogo ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maliasili na Mazingira iliyoundwa kuchunguza tuhuma za kuwapo kwa vitendo vya ufisadi, vinavyodaiwa kufanywa katika Wizara ya Maliasili na Utalii.
  Uchunguzi unaolengwa na kamati hiyo, unahusu utoroshaji wanayamapori kwenda nje ya nchi.

  Jana, gazeti hili liliripoti kuhusu kuundwa kwa kamati hiyo yenye wajumbe watano.
  Akizungumza ofisini kwake Dar es Salaam jana, Dk Kashililah alitoa wito kwa wananchi kuisaidia kufanikisha jukumu hilo.
  "Natoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa kamati hii katika kutekeleza jukumu lake, kila aliye na taarifa zozote zitakazosaidia kamati hii awe tayari kuzitoa," alisema Dk Kashililah.

  Alisema kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Mafia (CCM), Abdulkarim Shah, imepewa hadidu za rejea tano na muda wa majuma matatu kukamilisha kazi hiyo.

  Alizitaja hadidu hizo; kupitia na kuchambua sheria, kanuni zinazosimamia biashara ya wanyamaa pori hai na nyara, kupitia mfumo mzima wa biashara ya wanyamapori hai na nyara, ili kutoa maoni na mapendekezo ya kuboresha tasnia hiyo.

  Hadidu ya pili ni kuchunguza utaratibu uliotumika kukamata na kusafirisha Twiga wawili kwa kibali kilichotolewa Aprili 29, mwaka huu na utaratibu uliotumika kukamata na kusafirisha wanyamapori hai kutoka mwaka 2009 hadi sasa.

  Pia, kuchunguza ushiriki wa watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika biashara ya wanyamapori hai; kuchunguza mchakato mzima wa utoaji na ugawaji vitalu vya uwindaji wa kitalii.

  Hadidu rejea ya tano ni kuchunguza jambo lingine lolote litakalosaidia kamati katika kutekeleza majukumu yake kuhusiana na biashara ya wanyamapori hai/nyara na ugawaji wa vitalu vya uwindaji wa kitalii.

  Wajumbe wengine wanaounda kamati hiyo ndogo ni Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Bernadeta Mushashu, Mbunge wa Pangani (CCM), Salehe Pamba na Mbunge wa Mkoani (CUF), Ali Khamis Seif.

  Dk Kashilililah alisema hiyo imeundwa baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuridhia pendekezo la Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, Novemba 15, mwaka huu kwa mujibu wa Kanuni ya 114 (18) ya Kanuni za Bunge, Toleo la 2007.

  Kuundwa kwa kamati ndogo kunafuatia ombi lililowasilishwa kwa Spika Makinda na Mwenyekiti wa Kamati ya Maliasili na Mazingira, James Lembeli, akitaka kufanyika kwa uchunguzi wa kina kutokana na kuwapo kwa taarifa za kuendelea kwa vitendo vya utoroshaji wanyama kwenda nje ya nchi.


  CHANZO CHA HABARI : GAZETI LA MWANANCHI LA LEO


  Sorry, editing imenikaa kando kwa hapa!

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 4. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Ogopa sana maneno haya mchakato, tume, kamati, upembuzi yakinifu, kikosi kazi n.k. Hii ni kesi ya polisi si ya kuundiwa tume au kamati.
   
Loading...