Kamati Teule ya Bunge kuchunguza rushwa kwa wabunge ikishindwa ina maana gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati Teule ya Bunge kuchunguza rushwa kwa wabunge ikishindwa ina maana gani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 3, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nimeeleza kwenye ile mada nyingine kuwa haya yote ni mazingaombwe. Bado naamini hivyo. Ninaamini mazingaombwe haya ni kamili (complete illusion) kwa sababu kamati teule iliyoundwa na Spika Makinda kuchunguza tuhuma hii kimsingi imepewa jukumu lisilowezekana. Kamati hii inaongozwa na Hassan Ngwilizi (CCM) na wajumbe wake wengine wakiwa ni: John Chiligati (CCM), Said Arfi (CHADEMA), Riziki Omar Juma (CUF), na Gosbert Blandes (CCM).

  Nani aliomba rushwa na aliombaje?
  Kazi kubwa ya kuweza kuthibitisha hili inaanzia hapa. KT inapaswa kupata ushahidi usiokinzana wa kuonesha nani aliomba rushwa TANESCO na aliomba rushwa hiyo vipi. Ni rahisi - kwa kiasi - kuweza kutaja majina ya walioomba rushwa lakini kuweza kuonesha waliomba "vipi" rushwa hiyo ikawa ni kazi. Kama mbunge aliomba rushwa kwa mtendaji wa TANESCO na wakati anafanya hivyo walikuwa wawili tu ni kwa kiasi gani maneno ya mtendaji wa TANESCO yataweza kuaminika bila ya ushahidi mwingine wowote wa nje (mawasiliaoni ya simu, email, video au vimemo)?

  Kumbe haitoshi kusema tu "fulani aliomba rushwa" kwani hilo peke yake bila ushahidi wa nje wa uombaji huo ni maneno dhidi ya maneno.

  Nani alipokea rushwa?
  Sasa inawezekana kuwa ni vigumu kuonesha ni vipi rushwa iliombwa; lakini ni rahisi kwa kiasi chake kuonesha kama rushwa ilipokelewa. Kama rushwa haikutolewa na hakuna ushahidi wa kuonesha kuwa rushwa imepokelewa madai kuwa kuna mtu aliomba rushwa yanaweza kuonekana ni masimulizi tu. Kama rushwa ilipokelewa ni wazi basi kuna mtu aliitoa. Huyu aliyetoa ni nani? na kama alitoa ni kwanini alitoa bila kujaribu kuwasiliana na TAKUKURU kuwanasisha wataka rushwa hawa?

  Hili linatudokeza lile la kwangu la "mazingaombwe". Kama mtu alitoa rushwa bila kushirikisha vyombo vya usalama ili kumnasa mtoa rushwa mtu huyo naye anashtakika kwa mashtaka ya kutoa rushwa! Ikumbukwe katika sheria yetu mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wanashtakika! Ushahidi wa kuwa mtu kapokea rushwa ni pamoja na kukutwa na rushwa. Ina maana akaunti za wabunge WOTE wanaotuhumiwa kupokea rushwa (siyo kuomba tu) ni LAZIMA zipitiwe na kamati teule na pamoja na akaunti hizo ni zile za JAMAA NA NDUGU WA KARIBU na kulinganisha mtiririko (flow) ya fedha katika siku ambazo viongozi wanadaiwa kuomba rushwa.

  Uchunguzi huu hauwezi kukamilika bila kueleza wazi kuwa akaunti za wabunge watuhumiwa na jamaa zao wa karibu zilikuwa au hazikukutwa na kiasi cha fedha kinachodaiwa kutolewa. Naamini wataangalia pia 'movement' ya fedha kutoka akaunti hizo baada ya tarehe ya sakata kulipuka bungeni.

  Itakuwaje kama hakuna ushahidi wa kiforensiki wa rushwa?
  Sasa, swali hili liko katika kiini cha nani anasema kweli. Kama hakuna ushahidi wa rushwa kutolewa au kupokelewa na wala hakuna ushahidi wa rushwa kuombwa ni kwa vipi watu waliweza kusimama BUNGENI na kudai kuwa kulikuwa na rushwa? Je tunakumbuka (au tumesahau) jinsi sakata la Jairo lilivyodai kuwa kuna "rushwa" ilitolewa kwa wabunge na wengine tulipinga vile vile kwani hakukuwa na ushahidi? Na ni kweli walipochunguza "hawakukuta" rushwa hiyo? Sasa kama hakuna ushahidi wowote kuonesha kama rushwa iliombwa, ilitolewa au ilipokelewa hawa wabunge wanaosimama kudai kuna rushwa wanapata wapi taarifa hizo?

  Lakini kama wapo wabunge wanaopokea rushwa (wakiomba au wasipoomba) na wanaweza kuficha rushwa hiyo kiasi kwamba haiwezi kuonekana kwa vyombo vya usalama je hii ina maana gani? Je tuna uhakika gani kuwa kila wanapoulizwa "wale wanaokubali waseme ndiyo" wanasema ndiyo na "wale wanaokataa waseme hapana" halafu "waliosema ndio wameshinda" wanafanya hivyo wakiwa na mulungula mfukoni au kwenye vyungu vyao? Lakini, kama ni kweli wabunge wanaweza kuhongwa kwa ajili ya kufanya mambo fulani Bungeni na hakuna mtu ambaye ameweza kuwanasa ina maana kuwa tuna mfumo mbovu kabisa wa kupigana na rushwa? siyo?

  Kwamba wabunge wenyewe wanajuana nani mpokea rushwa na nani anapenda kuomba omba rushwa lakini wabunge hawa walioapa kuilinda, kuitetea na kuihifadhi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakuna hata mmoja wao ambaye ameweza kusaidia vyombo vya dala kuwanasa wenzie wala rushwa?


  Lakini swali la ugomvi ni kuwa: KAMA kweli Bungeni wala rushwa wapo, wanajuana na kulindana na wakikasirikiana wanatajana ni kwa kiasi gani tunaweza kuamini wanavyozungumza kwa jazba, kumwaga data na hata kuonekana ni wazalendo? Na kama wabunge wala rushwa hawawezi kupatikana tunaweza vipi kuliamini Bunge hili lote?

  Swali zaidi ambalo sitaki kufikiria maana yake ni kuwa ITAKUWAJE KAMA KAMATI TEULE ITAKUTA KUWA NI KWELI WAPO WABUNGE WAMEKULA RUSHWA? Ikumbukwe agizo la Spika Makinda ni kuwa wakimaliza kina Ngwilizi wamshauri nini cha kufanya! Hakuwapa agizo la kusoma ripoti yao BUNGENI. Kwanini wabunge wasimtake Spika kutaka Kamati Teule isome ripoti yake Bungeni moja kwa moja ILI BUNGE LIAMUE NINI CHA KUFANYA BADALA YA YEYE MTU MMOJA?
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Nami nakuunga mkono sana MKJJ hiyo KT ni kupoteza pesa za wavuja jasho, na kupoteza muda kabisa huwezi thibitisha moja kwa moja, ni ngumu sana sana,

  Majibu ya tume watasema kulikuwa na muonekano wa rushwa, ila kuthibitisha ndio issue,mapendekezo....ni kosa kufanya biashara kwa wajumbe wa kamati mbali mbali kwa makampuni wanayosimamia,

  Hata ujumbe wa bodi..yaani TOR ya hito tume wataitengeneza kupata majibu yanayowalinda na kumaliza hilo suala bila utata!!ila yana mwisho natamani sana ingekuwa 2015 Jan.....
   
 3. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Kamati ikisema haijathibitisha kuwa kuna mbunge aliyeomba, kupokea wala kutoa rushwa, waziri aliyesema hivyo bungeni anatakiwa kujiuzulu mara moja! Kamati ikithibitisha otherwise, wabunge tajwa wanatakiwa kukamatwa na takukuru na sheria kufuata mkondo wake. Nategemea moja kati ya hayo!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  wanaweza wasije na stori nyingine yoyote kwani wanaripoti kwa Spika na Spika atakuja na kusema baada ya kupitia hiyo ripoti ameona kuwa suala hilo limemalizika na yeye "ameridhika"!
   
 5. G

  Godwine JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ni rais sana kudhibitisha wabunge wala rushwa lakini ni ngumu kudhibitisha wamekula rushwa lini, Nyerere alikuwa na mfumo wa kikandamizi lakini ulikuwa unatoa majibu sahihi japo kwa njia hisiyo sahihi. hapa imefika wakati kujumuisha mali zote za wabunge wanaoshutumiwa kwa rushwa na kisha kila mmoja aeleze amezipata wapi na kutokana na chanzo gani na kwa njia gani. najua inaweza kuwa wengine wakajitetea kuwa hawana kumbukumbu, lakini haiwezekani umiliki mali ambazo utashindwa kueleza zimetoka katika chanzo gani.

  kwa njia hii ni rais kuwapata wara rushwa na watumia madaraka vibaya kwani akisema pesa yake imetokana na biashara basi ni wakati wa kuchunguza na ulipaji wake wa kodi wa TRA na kuona kama biashara yake inaweza kumuingizia kiasi hicho cha fedha.
   
 6. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Duh! Nachelea kusema kuwa sisi, wabunge wetu pamoja na waziri aliyetoa tuhuma tutakuwa wajinga sana kama na sisi "tutaridhika" kama yeye! Sidhani kama tutafanya hivyo. Sababu itamaanisha kwamba waziri pamoja na Lissu watageuka watuhumiwa wa kuwakashifu wenzao na watashahili adhabu maana watakuwa wameshindwa kudhibitisha!
  Kwa upande wa pili, hiyo itakuwa ni mwendelezo wa mapigo wanayoyapata ccm kuelekea anguko lao. Cdm wakiichukua hiyo kama agenda na kwenda kuwashtaki kwa wananchi ccm watapata shida sana. Sijui watatokea wapi?
   
 7. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Ina maana nao wamekula mlungula.
   
 8. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  KWA HIYO HAPA NDIO UMEANDIKA MPAKA MWISHO WA AKILI ZAKO,KWA TAARIFA YAKO HAPA HUJAANDIKA KITU JIPANGE UJE UPYA THIS IS NONSENSE,MWAMBIE ALIEKUTUMA UCHUNGUZI UTAFANYWA NA UKWELI UTAJULIKANA KWA TAARIFA YAKO KAMA MHANDO MSOMI INJINIA HANA AKILI KIASI CHA KUFUNGUA KAMPUNI KITANDANI NA MKEWA NA KUIPA TENDA TANESCO BASI WABUNGE WETU MAMBUMBUMBU HAWANA UJANJA WA KUFIKIRIA KUPITISHA HELA KWENYE ACCC ZA NDUGU ZAO KILA KITU KITAKUWA WAZI SOON NA KAMA ZITTO KAKUTUMA UMTETEE HAPA MWAMBIE UMECHELEWA WANANCHI TUMESHAZInDUKA PERIOD
   
 9. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Tatizo letu ni upeo mfupi, walioteuliwa kwenye kamati hawana utaalam wowote kuchunguza kesi za rushwa au uhalifu wa kifedha (FORENSIC AUDIT) unategemea nini hapo mkuu?
   
 10. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #10
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Serikali haiko serious na issues, ninashangaa timu ya uchunguzi imeundwa, inaongozwa na wajumbe wengi kutoka ccm ambayo kwa sehemu kubwa inatuhumiwa kupokea rushwa.
  Kwanini viongozi wetu wanakosa busara hata kuunda tume huru ya kuchunguza tuhuma dhidi ya wawakilishi wetu tujue ukweli?
   
 11. HIMO ONE

  HIMO ONE Senior Member

  #11
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwana kijiji bana yaani yuko kama housegirly wa zitto kumtetea tuu kwa kila namna
   
 12. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,502
  Likes Received: 5,613
  Trophy Points: 280
  Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya bunge kuongoza kamati ya kiuchunguzi kwa wabunge imenishangaza pia!
  hapo patakuwa na Independence kweli? Matokeo ya hapo yanaweza kuhojiwa wapi? Ngwilizi atasimama kwa kofia ipi?
  madai yalipopelekwa kwenye kamati ya Ngwilizi wametoa taarifa gani? Spika ameunda kamati based on what? taarifa ya kamati ya maadili ya Bunge au kwakuwa kuna tuhuma tu?​
   
 13. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  MKJJ,kwa system ya Tanzania ni ngumu sana ku-prove kwamba wabunge waliotuhumiwa wamepokea rushwa. Kama ulivyosema, unatakiwa ushahidi wa kiforensiki jambo ambalo kwa Tz inaniogofya kusema kwamba utaalam huo hakuna. Ndio maana hata sehemu zinazolalamikiwa kupokea rushwa kwa kiasi kikubwa,bado wahusika wameshindwa kuthibitisha hilo. Ni lazima kujua kwamba, hata anaepokea rushwa nae anatumia ujanja wa hali ya juu kuhakikisha kwamba anafuta tracks zake ili asije akakamatwa mwisho wa siku. Mh. Spika alisema km kuna mbunge mwenye taarifa za kuwahusisha wabunge tajwa ajitokeze na kutoa ushahidi. Jambo ambalo kwa mila na desturi za ki-TZ si rahisi. So, mwisho wa siku KT ina wakati mgumu kupata ushahidi usio na mashaka juu ya tuhuma hizo. Letz wait n see!
   
 14. p

  pembe JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 2,058
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mzalendo JR uko sahihi pamoja na hao waheshimiwa angekuwepo mtaalamu (wataalamu) wa nje. Huyu angewasadia kupambanua hizo tuhuma kwa kuuliza maswali ya papo kwa papo yatakayowafanya wajikute wameshasema walichokuwa hawataki kusema.
  Pamoja na hayo nilitegemea kamati ya bunge ya maadili ndio ingetoa issue hiyo au yenyewe inangojea tu haifanyi kazi?
   
 15. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  hii hoja yako ndio jibu sahihi la huu mlolongo wote lakini kwa hali ya kitaasisi tuliyo nayo sasa hivi kama alivyosema Mzee Manakijiji hawa watu hawawezi kutajana.
  Cha msingi hapa kwa wale great thinkers wa-note hili suala na tusiwe kama wale wanaosahau sahau na kuongozwa na matukio ili kuweza kufanya marejeo ya kosa na 'ujinga' wana namna hii uko mbeleni. Maana sitaki kujiaminisha kuwa Watanzania tutaendelea kufanya mambo yetu kwa kutumia akili ndogo milele!
  Chukulia mfano wa hukumu ya mgomo wa walimu inayothibitisha kuwa kumbe masaa 48 ya weekend serikali inakuwaga likizo na hizo siku haziihusu lakini wakasahau kuwa wenyewe waliwahi kupata hati ya zuio la mgomo saa nane usiku siku hizo hizo za weekend.

   
 16. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #16
  Aug 3, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Kama suala la Lema lilivyofunikwa, suala la kamati ya huduma za jamii ilivyofunikwa kuhusu mgomo wa madaktari n.k.

  Najiuliza kwanini kamati iripoti kwa Spika na si bunge. Hii ni kamati ya Spika au ya bunge?
   
 17. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Absolutely spot on mkuu! easy and straight forward then wanashikika! Serikali inafanya mambo yanakuwa magumu sana ktk kuwapata mafisadi, na hii ni kwa sababu ya mfumo mbovu wa kulindana ambao umejengwa na utawala mbovu, usio na clues, na mchafu kupita kiasi.
   
 18. W

  WildCard JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kama wanaotuhumiwa kula rushwa ni WABUNGE; wanaowatuhumu ni WABUNGE; kamati teule pia inaundwa na WABUNGE; Kamati hii imeshindwa kabla hata haijaanza kazi. Mimi nilidhani kanuni za Bunge zinaruhusu Spika kuunda kamati hii nje ya Bunge lenyewe kwa kuteua watu kama Majaji wa Mahakama Kuu/Rufaa.
  Hata hivyo Mwanakijiji, kamati nyingine zote zilizoitangulia hii nazo pia zimeshindwa kwa maana kwamba hata MAAZIMIO yaliyofikiwa hayakufanyiwa kazi. Nadhani imefika wakati sasa mhimili huu wa BUNGE ukaondolewa kinga ulizojizungushia ili pamoja na mambo mengine uache kujigeuza kufanya kazi za mihimili mingine.
   
 19. c

  chama JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Rushwa wale wao kujichunguza wajichunguze wao hiki ni kichekesho cha mwaka; bunge limejaa wasanii kama tume ya kuwachunguza iundwe tume huru vinginevyo kuliongezea gharama taifa zisizo na maana.

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 20. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwa kamati hizi za ccm usitegemee mbunge yeyote wa ccm kutiwa hatiani kwa kuomba ama kupokea rushwa. Alichofanya waziri wa nishati ni kupiga kelele ili kuinusuru bajeti yake na kunusuru nafasi yake ya uwaziri pamoja na katibu mkuu wake.
  Kutokana na mazingira ya sasa ya kisiasa usitegemee kamati hii iichome kisu ccm, kwani kuwabainisha wabunge wala rushwa ni sawa na kuichoma ccm kisu cha mgongoni. Wacha wale posho tu lakini hakuna lolote hapo.
   
Loading...