Kamati NEC yashauri Chadema ienguliwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati NEC yashauri Chadema ienguliwe

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Geza Ulole, Oct 26, 2010.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,064
  Likes Received: 3,986
  Trophy Points: 280
  26th October 10
  Kamati NEC yashauri Chadema ienguliwe

  Waandishi Wetu

  Chama Cha Demokrasia na Maedeleo (Chadema) kiko hatarini wagombea wake wa ubunge na udiwani kuenguliwa katika Jimbo la Maswa Magharibi katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumapili kutokana na kuhusishwa na vurugu zilizotokea wiki iliyopita na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
  Tishio la wagombea wa Chadema kuenguliwa linatokana na Kamati ya Maadili ya Uchaguzi ya Jimbo la Maswa Magharibi kupendekeza wagombea wa Chadema waenguliwe kwa madai ya kuwa chanzo cha vurugu hizo.
  Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Maswa, Magharibi Elizabeth Kitundu, alisema jana kuwa kamati hiyo ilikutana Jumamosi iliyopita kujadili hoja ya kuwaengua wagombea wa Chadema kushiriki katika uchaguzi.
  Kitundu alisema kuwa tume hiyo imepeleka mapendekezo hayo kwa Kamati ya Maadili ya Uchaguzi ya Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC).
  Aliongeza kuwa Chadema nao tayari wamepeleka barua ya kujitetea kupinga kuenguliwa katika uchaguzi huo. Hatua ya kamati hiyo inadaiwa kuchukuliwa kufuatia vurugu zilizotokea Oktoba 21 na kusababisha kifo cha mfuasi mmoja wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Kwilasa, ambaye alipigwa jiwe na kuchomwa na kitu chenye ncha kali na kufariki papo hapo katika vurugu zilizotokea katika kijiji cha Kizungu wakati mgombea ubunge wa Jimbo la Maswa Magharibi kupitia Chadema, John Shibuda, alipokuwa akijinadi mbele ya wananchi wa kijiji hicho.
  Mwenyekiti wa NEC, Jaji Lewis Makame, alipoulizwa kama NEC imepokea mapendekezo ya kuwaengua wagombea wa Chadema, alisema kuwa asingeweza kulizungumzia suala hilo kwa kuwa alikuwa katika kikao.
  SHIBUDA AACHIWA
  Katika hatua nyingine, Jeshi la polisi limemwachia Shibuda aliyekuwa anashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na vurugu zilizosababisha kifo cha mfuasi wa CCM.
  Shibuda aliwekwa mahabusu tangu Oktoba 21, baada ya kutokea vurugu baina ya wafuasi wa Chadema na CCM iliyotokea katika kijiji cha Kizungu Kata ya Buchambi wilaya ya Maswa.
  Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, alisema upelelezi wa kina uliofanywa na jeshi hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama nchini umebaini kuwa Shibuda hakuhusika na tukio hilo.
  Alisema kwa mujibu wa upelelezi huo wakati tukio hilo likitokea, Shibuda alikuwa akifanya mkutano wa hadhara umbali wa mita 200 kutoka eneo la tukio na kuwa upelelezi huo pia hauonyeshi kuhusika kwake namna yoyote ya uchochezi wa vurugu hizo.
  Manumba aliwaambia waandishi wa habari mjini Maswa kuwa Shibuda aliachiwa huru juzi majira ya saa 1:45 usiku ili aendelee na kampeni.
  Hata hivyo Kamishna Manumba alisema kuwa upelelezi unaendelea na iwapo utapatikana ushahidi wa kutosha kwamba alihusika, atapaswa kuunganishwa katika tuhuma za mauaji hayo inayowakabili watu 11 ambao ni wafuasi wa Chadema.
  "Kwa kuwa upelelezi haufanyiki kwa kipindi kifupi na kwisha yawezekana baadaye Shibuda pia akakamatwa na kuunganishwa kwenye kesi hiyo ya tuhuma ya mauaji, lakini kwa sasa tumejiridhisha kabisa kuwa hana kosa na ndiyo maana tumemwachia huru," alisema.
  Kuhusu tuhuma za mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Robert Kisenha, kumpiga Mkuu wa Polisi Wilaya ya Maswa, Peter Ndunguru, DCI Manumba alisema mtuhumiwa huyo tayari amekamatwa lakini kwa sasa yuko nje kwa dhamana.
  "Pamoja na kuwa mtuhumiwa huyu wa kumshambulia OCD yuko nje kwa dhamana, tuhuma zake tunazipeleleza kujua kama kweli alifanya hivyo na tukipata ushahidi wa kutosha basi sheria itafuata mkondo wake," alisema Manumba.
  Kutokana na tukio hilo, watuhumiwa hao 11 jana walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Maswa na kusomewa shitaka la mauaji ambapo hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
  Watuhumiwa hao walisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu mkazi wa wilaya hiyo, Thomson Mtani, ambapo kesi hiyo imepangwa kutajwa tena Novemba 8, mwaka huu. Watuhumiwa wa kesi hiyo ya mauaji ni pamoja na Mohammed Juma (30), Constantine Zengo (20), Raphael Deusi (20), Juvent William (30), Frank Gogadi (22) na Emmanuel Bundala (22).
  Wengine ni Omary Idd (26), Waziri Peter (40), Stephen Makondo (26), Emmanuel Edward (25) na Paschal Damian (19) wote wakazi wa Maswa.
  Imeandikwa na Anceth Nyahore, Mohab Dominic na Stephen Wang'anyi (Maswa).

  NIPASHE

  Kamati NEC yashauri Chadema ienguliwe

  MY TAKE
  Hawa wanajitafutia visababu kwa mwenendo huu si shangai NEC kuwa kuwadi wa CCM maana kule Upinzani unaposhambuliwa haswa CHADEMA wanakaa kimya mbali na kupewa malalamiko! Uvumilivu umewashinda wananchi wameamua kufanya fujo, tunaona NEC wakitaka kumuengua Mh. Chibuda! Hii si haki nathani EU Observers wanaona hili....jinsi demokrasia inavyonyongwa!
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwanza hii kamati ya NEC huteuliwa na nani? Sidhani kama ni NEC yenyewe kwa maana ya Makame na taasisi yake, kwani huyu ameonyesha hana meno kabisa. Makame hukenua meno tu pale wale anaodai/anaofikiria ni wasimamizi wake wa uchaguzi katika majimbo wanahamishwa kwa agizo la mgombea wa CCM (kupitia waziri wake husika) wakati kamp[eni zinaendelea.

  Kwa hiyo Wasimamizi wote wa uchaguzi hawana loyalty kwa Makame na timu yake, bali kwa serikali ya CCM iliyowateua katika nyadhifa ambazo hatimaye wanakuwa wasimamizi wa uchaguzi. Maamuzi yao yanukuwa pro-CCM tu! Inawezekana kamati hiyo ya NEC ilipata agizo kutoka kwa Makamba kufanya hivyo.

  Kama tungeshuhudia Makame analalamika kuhamishwa ghafla kwa watu wake katikati ya kampeni, hapo tungekubali kweli anatetea haki katika usimamizi wa mchakato wa uchaguzi. Anamdanganya nani?
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Umenena Mkuu:

  Lakini habari nilizopata, yaani zilizovuja kutoka sehemu hiyo ni kwamba kamati hiyo ya NEC iligawanyika, yaani haikuwa unanymous katika pendekezo hilo. habari zinasema baadhi ya wajumbe walinunuliwa kwa fedha zilizotoka kwa mfanyabiashara mmoja maarufu wa sehemu hiyo ya nchi na ambaye amekuwa anabebea tuhuma nzito za ufisadi.

  Mtoa habari wangu anasema mfanyabiashara huyo alitoa msukumo kwa kamati hiyo ya NEC kukaa haraka haraka baada ya kuona Shibuda ataachiliwa na polisi kwa sababu kwamba hana kosa.
   
Loading...