Kamati ndogo ya kamati ndogo ya Kamati Kuu ya Chadema inaundwa na akina nani? Wanaohama wanailalamikia

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Ndugu zangu,

Wengi ambao hawaridhishwi na uongozi Chadema pamoja na mengine lakinin wamekuwa wakisema kuwa kuna kamati ambayo Mbowe kaiunda kinyume na katiba inaitwa ''kamati ndogo ya kamati ndogo ya kamati kuu ya Chadema'' yaani kamati kuu ina kamati ndogo kisha hiyo kamati ndogo ya Kamati Kuu imetengenezewa kamati ndogo ili kuhakikisha ajenda ya Mbowe inachujwa.

Yaani kwa kifupi yanayotangazwa na Makene huanzia kwa Mbowe, kisha kamati ndogo ya kamati ndogo ya kamati kuu, kisha hupelekwa kamati kuu. Zaidi, Katibu Mkuu wa Chadema yeye hushiriki kikao cha kamati kuu tu ila sio zile kamati ndogo mbili.

Ukimuondoa Mbowe na Lema nani mwingine ni mjumbe wa kamati ndogo ya kamati ndogo ya kamati kuu? Je, kamati hii ipo kwa mujibu wa katiba ya chama? Ni rasmi?

Hili jambo limenikumbusha maneno ya Mch. Mtikila (R.I.P) aliyewahi kubainisha kuwa Chadema ina matabaka yaani ''kuna Chadema sebuleni na Chadema chumbani'' ni nani hawa wajumbe wa kamati ndogo ya kamati ndogo ya kamati kuu?

Tujadili bila fujo.
 
Kuna wakati ukiwasikiliza wanao hama maneno yanatofautiana na sura zao

Ukweli inawezekana kabisa chadema wakawa na makosa ila wanao wapokea wakawa na makosa mara mbili
 
Mtahangaika sana na CDM!Inawakosesha usingizi yaani kila kukicha mnachadema kichwani kwenu!CDM inatamkwa sana kulicho chama chochote nchi hii,hii ni dalili nzuri!
 
Back
Top Bottom