Kamati Maalum yaundwa kuwashitaki mafisadi wa EPA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati Maalum yaundwa kuwashitaki mafisadi wa EPA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MC, Jun 27, 2008.

 1. M

  MC JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2008
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kama kweli hii kamati imeundwa na watu watakuwa serious Tanzania itakuwa imekombolewa,

  Kwa kuwa huu ndio utakuwa Mwisho wa Mafisadi na serikali inayowatetea,

  Source: IPP Media

  Wapinzani kuwafikisha Kortini mafisadi wa EPA

  2008-06-27 11:06:53
  Na Simon Mhina


  Wapinzani wameunda kamati maalum itakayohakikisha kwamba watu wanaodaiwa kuchukua fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) Sh. bilioni 133 wanafikishwa mahakamani.

  Hatua hiyo imekuja kufuatia mvutano ulioibuka upya ndani ya Bunge kuhusu waliopora fedha hizo, ambapo sasa serikali inadai kuwa fedha hizo hazikuwa za umma isipokuwa za wafanyabiashara.

  Tayari wapinzani wameunda kamati maalum ya kupambana na waporaji wa nchi ijulikanayo kama Public Interest Litigation Commitee (PILCOM) kwa ajili ya kuwaburuza mahakamani waliopora fedha hizo.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo, ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha Democratic, Mchungaji Christopher Mtikila, alisema lengo la kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hao ni kulinda hadhi ya Bunge, ambayo inachezewa na kuhakikisha matrilioni ya wavuja jasho yaliyochukuliwa kijanja yanarejeshwa.

  ``Kazi ya kamati hii ni kuwafikisha mbele ya sheria watu wote walioshiriki katika wizi wa matrilioni ya mapesa ya nchi yetu katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na katika Hazina ya taifa letu, ili wazirejeshe fedha hizo pamoja na riba, gharama pamoja na zile walizoziweka nje ya nchi, ``alisema.

  Alisema wajumbe wa kamati ya PILCOM, ni pamoja na mawakili 26, wabunge wa upinzani na wale wa CCM wenye mrengo wa kuwatetea wananchi, maaskofu pamoja na masheikh.

  Hata hivyo, alisema amekubaliana na hoja zilizotolewa na wajumbe hasa wale wa dini na wabunge wa CCM kwamba kwa sasa wasitajwe kwanza.

  Alisema kilichotoa msukumo wa watu wanaoipenda nchi hii kufungua kesi hiyo, ni hatua ya kujitokeza kwa kikundi kidogo cha wabunge ambao wamediriki`kuwasafisha` mafisadi bila aibu.

  Alisema fedha zilizoporwa lazima zirudishwe, hivyo kwa vile Bunge limeanza kusuasua, lazima mahakama iingilie kati ili sheria ifuate mkondo wake.

  Kuhusu Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustapha Mkulo, Mchungaji Mtikila alisema waziri huyo amekwenda kinyume na kauli ya Rais Kikwete na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda pale aliposema fedha za EPA sio za serikali.

  ``Kwa maneno mengine Mkulo anataka kusema Kikwete alikosea kumfukuza marehemu Balali, kama fedha sio za serikali, kwanini Rais ameunda chombo cha kiserikali kuchunguza?

  Mkulo anataka kutunyamazisha au mapesa ya EPA ndiye yanazidi kutoa jeuri kwa watu kiasi hicho,``alihoji.

  Aliwataka wananchi kuiunga mkono kamati hiyo, ambaye inapambana na magenge ya mafisadi, ambayo yanaogopwa hata na serikali yenyewe.
   
 2. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Bravo Mtikila na Kamati yote, maneno matupu haya saidii, hii move ya matendo ni nzuri sana, binafsi ninaunga mkono asilimia mia kwa mia,

  Tena nashauli kamati hii iitishe hata maandamano nchi nzima tutayaunga mkono kwa nguvu zetu zote, ili ujumbe ufike vyema wajue tulivyo chukizwa nao! na kuwaamsha wengine ambao hawajui kinacho endelea waelewe kwamba kweli wanaibiwa, hawapaswi kuwa walivo,ugumu wa maisha walio nao si mapenzi ya Mungu, watambue nani mwizi wao, na pengine itatubadilisha kutumia siraha tuliyo nayo juu ya wezi wetu!


  Haiwezekani kigenge cha watu kiigeuze nchi kama ya kwao, Tanzania ni yetu wote, na kweli ikibidi pasitoshe lakini lazima wote tufaidi maziwa na asali tulivyo jaliwa na maulana katika Tanzania yetu.
   
 3. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2008
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hii itasaidia maana mategemeo toka mhimili wa bunge ndiyo yameyoyoma kufuatia kauli tata zinazoendelea kutolewa na serikali huko Dom.
  Bravo..Go PILCOM na Mungu yupo upande wa wanaopigania haki!
   
 4. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  I dont have anything against this committee ila I doubt if they will deliver what is expected of them
   
 5. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2008
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  "BRAVO PILCOM WEMBE NI ULEULE ULIOMYOA KIPANGA NA NDIO TUTAKAUTIMIA KUWANYOA HAWA MAFISADI"... tatizo mafisadi wanamuona Mtikila kama mropokaji but ukweli huwa anawaeleza ukweli na unawachoma kisawasawa "umoja ni nguvu utengano ni uzaifu WAKEREKETWA WA NCHI NA WENYE UCHUNGU NA NCHI TUKISHIRIKIANA KWA PAMOJA TUNAWEZA NA KWA NGUVU ZA MWENYEZI MUNGU TUTAWASHINDA
   
 6. kkiwango

  kkiwango Senior Member

  #6
  Jun 27, 2008
  Joined: Aug 27, 2007
  Messages: 168
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Count me inn..........
   
 7. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kumbe ndio maana!!!!!??? Kweli kuna mpangp serious unafanywa na watu serious
   
 8. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #8
  Jun 27, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  ni mapema mno kuweka matumaini yetu yote kwenye kamati hiyo ya mtikila kwa sababu mafisadi wapo katika juhudi za kuzuwia ushahidi wote.
  na hadi kesi hiyo ikifika mahakamani, nyaraza zote zitakuwa zimeshaharibiwa.
  ila tuombe mungu
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jun 27, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Inapofikia Raia wanaamua kufanya kazi ambayo ilitakiwa kufanywa na watu walioajiriwa kufanya kazi hiyo basi tunakokwenda kubaya. Kama tunavyombo vya upelelezi na uendeshaji mashtaka na vyote vimekaa kimya kuhusu EPA hadi kina Mtikila wanakuja na Kamati zao basi tuko kwenye matatizo makubwa zaidi kuliko tunavyodhania.
   
 10. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Moja ya tatizo ni kuwa, hata kama watu wa serikali wakitaka kupambana na mafisadi (hawataki by the way, wanagelesha tu) kuanzia Rais, Makamu wake mpaka Waziri Mkuu wote hawana uti wa mgongo wa kuhimili mikiki mikiki ya mafisadi.

  Huyo Waziri Mkuu ndiye kasema wazi kabisa kwamba "mafisadi wana nguvu sana, tunawaogopa". Mtu ana nguvu zote za dola anadiriki ku whine kama hivyo.

  Essentially anasema "mmemweka mtu bogus kuwa Waziri Mkuu, mimi siwezi kazi niliyotumwa ni kubwa mno kushinda uwezo wangu".
   
 11. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  atutajie na wana kamati basi....
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Jun 27, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Haya kamati nyengine hiyo , inazuka ,nafikiri kuna haja ya kuandaa maandamano Inchi nzima tukianzia Mwanza mkoa kwa mkoa na halafu Unguja na kabla ya kufikia kilele matayarisho ya kilele yataanza Pemba na hapo DSM ndio paka atafungwa kengele.
  Sasa hii kamati itupe time frame ambayo WaTanzania watahitaji kujua ni lini na matarajio ya kumalizika maana kezi za mamilioni tena ya serikali zinaweza kuchukua uhai wa mtu .atazaliwa ataishi atazeeka na bado kesi haijamalizika.ila kwa hii iwepo na maombi spesho imalizike kabla ya Uchaguzi Mkuu.
  Hapa naona kuna kitu kwa muangalio flani flani isje kuwa inatumika njia ya kuzima na kuzika ,wakati kule Bungeni kumeshaonekana mambo yameanza kukaa sawa kwa mafisadi sasa undergrounder wamebuni mbinu ambayo itaondoa mawazo na bungeni na kuyahamishia mahakamani kwenda kupigwa tarehe na tarehe.
   
 13. w

  wajinga Senior Member

  #13
  Jun 27, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii Kamati Itachukua Mwaka Kupeleka Mapendekezo Yake, Alafu Bunge Litajadili Mapendekezo Ya Kamati Miaka Ijayo Alafu Rais Atasoma Mapendekezo Hayo Wakati Wa Uchaguzi Mwaka Elfumbili Na Kumi. Mungu Ibariki Tanzania.dumisha Mafisadi Na Wakandamize Wanyonge, Amen
   
 14. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #14
  Jun 27, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Swine zao mafisadi
  Mkulo must be in the list.... Si alikuwa msaidizi wa Meghji huyu??? Basi ccm imeishiwa viongozi sasa inakopa kutoka kwa mafisadi
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Jun 27, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280
  Hii kamati itahitaji support kubwa ya hali na mali kutoka kwa Watanzania wote wanaopenda maendeleo ya nchi yetu na kuona mafisadi wote wanamalizwa kabisa. Kama kuna yeyote anayefahamu kama kamati hii inahitaji michango ili kuisadia katika shughuli zake za kila siku atufahamishe. Wakati ni huu wa kupambana na mafisadi na kuwang'oa kabisa tukipoteza nafasi hii na kuwaachia mafisadi kushinda basi hatutapata muda tena wa kupambana na mafisadi hao.
   
 16. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #16
  Jun 27, 2008
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  1. Simuamini Mtikila maana kwenye kesi zake nyingi wala sikumbuki ni ipi iliyoisaidia nchi, naomba kukumbushiwa kama ipo.


  2. Hii ina maana gani kwa wabunge wetu hasa wa upinzani, je wameshindwa kukabiliana/kuiwajibisha serikali?
   
 17. Nyangumi

  Nyangumi JF-Expert Member

  #17
  Jun 27, 2008
  Joined: Jan 4, 2007
  Messages: 508
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kauli kama hiyo inatuonyesha jinsi Tanzania tulivyo na watawala madubwana, wasiyo na kitu kichwani. Huwezi kuwa Waziri mkuu then unatuambia kuna maafisadi wanae nguvu zaidi yako, technically ni kuwa unatuambia kuwa wewe sio Waziri mkuu.


  Kushusu suala hili la kamati naliunga mkono lakini najiuliza kama watumishi wote wa mahakama wanaajiriwa na serikali ya Maafisadi ambao hawataki kuwachukulia hatua majambazi wenzao then tunategemea kupata nini huko mahakamani?
   
 18. M

  MC JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2008
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  _____ ____ ____

  Ni kweli kabisa, tutawaunga mkono kwa kila hali, Tanzania sasa inahitaji iendeshwe na Nguvu ya Umma, kwa kuwa Baadhi ya wabunge wamenikatisha tamaa sana ndio maana naunga mkono hoja hii, ila naomba Mtikila awe mkweli na Muwazi kwa kuwa wakati mwingine huyu bwana huwa ana siasa zenye utata!
   
 19. M

  MC JF-Expert Member

  #19
  Jun 28, 2008
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45

  Hata mimi huwa naamini siasa za Mtikila ni siasa zenye utata, ila kama kweli kamati hiyo iko na watu makini kama ilivyotajwa naamini wataweza kumdhibiti hata akitaka kuleta usaliti, kwa kuwa Watanzania wengi wamefurahia uamuzi huo wa kuunda kamati na wako tayari kutoa support, kwa hiyo Mtikila hapo hawezi kutudanganya bali atatakiwa afanye kazi kwelikweli
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  Jun 28, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,543
  Likes Received: 1,892
  Trophy Points: 280
  Niliwaambia GUYS kuna COALITION ISIYO JALI VYAMA,DINI WAlA ukabila...COALITION AMBAYO KAMA BUNGE LISIPOFANYA KAZI YAKE...THEN INAWEZA KUCHUKUA NCHI NA KUTELETEA MAPINDUZI BORA!
   
Loading...