Kamati kuuchunguza mkataba wa Buzwagi

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Kamati kuuchunguza mkataba wa Buzwagi

NA MWANDISHI WETU
Dar es Salaam
.Kuanza vikao vyake wiki ijayo Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Kamati ya kuangalia upya mikataba ya uchimbaji madini, Jaji Mark Bomani, amesema kamati yake itapitia mikataba yote ukiwamo ule wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, na kuweka bayana watakachobaini.

Akizungumza kwa simu na KULIKONI jana, Jaji Bomani alisema kamati yake itahakikisha inatimiza wajibu wake kwa kuangalia kila eneo linalohusu mikataba ya madini na kulitolea maelezo kama ilivyoanishwa katika hadidu za rejea.

Aliulizwa kama kamati yake itaangalia mkataba wa Buzwagi na kuzungumza na wahusika wakuu wa mkataba huo, alisema, “Sisi tutaangalia yote na iliyona dosari tutasema na isiyo na tatizo pia tutasema. Tumepewa jukumu la kukutana na “Chamber of Mining” na wadau wengine kwa hiyo wote hao tutakutana nao.”

Kauli hiyo ya Jaji Bomani imekuja huku kukiwa na wasiwasi kwamba baadhi ya wajumbe wana mahusiano ya karibu na wahusika wakuu wa mikataba ya madini wakimtaja na Peter Machunde wa Soko la Hisa la Dar es Salaam ambaye anatajwa kuwa na mahusiano ya kibiashara na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi.

Wajumbe wengine wa kamati hiyo walitajwa kuwa ni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, kupitia Chadema, Zitto Kabwe na Mbunge wa Bariadi Mashariki, UDP, John Cheyo, Dk. Harrison Mwakyembe (Kyela-CCM), Ezekiel Maige (Msalala-CCM) na Waziri wa zamani wa Biashara na Viwanda, Iddi Mohamed Simba.

Wajumbe wengine wametajwa kuwa ni pamoja David Tarimo wa PriceWater Coopers na Maria Kejo wa Wizara ya Sheria na Katiba, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Mugisha Kamugisha kutoka Wizara ya Fedha na Edward Kihundwa, ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Makazi, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.

Kuhusishwa kwa Machunde na Karamagi ambaye ndiye hasa chimbuko la kupamba moto kwa mjadala wa madini kutokana na kusaini mkataba wa Buzwagi kimya kimya akiwa safarini London, kulijenga hisia za uwezekano wa kulindana lakini Jaji Bomani aanaondoa hofu hiyo kwa kusema hakuna mkataba utakaoachwa.

Jaji Bomani alisema maandalizi ya kuanza kwa vikao vya kamati yamo katika hatua za mwisho ikiwa ni pamoja na kuteuliwa kwa watendaji ambao wataunda sekretarieti ya kamati hiyo pamoja na kuwapelekea barua rasmi wajumbe wote ambao wameteuliwa.


Rais Jakaya Kikwete, alitimiza ahadi yake ya kuteua kamati ya kupitia mikataba ya madini, ahadi aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma hivi karibuni. Rais aliahidi kuingiza na wanasiasa kutoka upinzani.

Uteuzi wa wabunge wa upinzani umeibua mjadala mkubwa hususan kwa upande wa CHADEMA ambako baadhi ya viongozi wake wameonekana kutofurahishwa na uteuzi wa Zitto katika kamati hiyo na kutoa kauli za kukinzana katika siku za hivi karibuni.

Tayari Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ameitisha kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kujadili suala hilo ambalo linaashiria uwezekano wa kuwapo mgawanyiko mkubwa ndani ya chama hicho kilichoanza kupata wafuasi wengi katika siku za karibuni.

Hii ni mara ya pili kwa Zitto kuteuliwa na Rais, mara ya kwanza ikiwa ni katika kamati ya kupokea maoni ya uundwaji wa Shirikisho la Afrika Mashariki, uteuzi ambao ulipata baraka zote za Chadema na haukuwahi kupigiwa kelele.

Pamoja na baadhi ya watu kudai kwamba kamati hiyo haina hadidu za rejea, taarifa ya uteuzi wa kamati iliyosainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, ilizitaja kuwa ni pamoja na;

“Kupitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zinazohusu migodi mikubwa, kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta ya madini, kupitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchumbaji mkubwa unaofanywa na serikali, kuchambua na kuanisha haki na wajibu wa wekezaji na mwenye rasilimali (serikali), kukutana na chamber of mines na wadau wengine na kutoa taarifa yenye mapendekezo.”

Jaji Bomani alisema kati hiyo iliyopewa miezi mitatu kukamilisha kazi yake, inatarajiwa kuanza vikao vyake Dar es Salaam wiki ijayo baada ya wajumbe wote kupata barua kwa maelezo kwamba baadhi wako nje ya nchi na wengine mikoani.

Kulikoni: Jumatano, Novemba 21, 2007
 
Kamati kuuchunguza mkataba wa Buzwagi

NA MWANDISHI WETU
Dar es Salaam
.Kuanza vikao vyake wiki ijayo Dar es Salaam

........

"Kupitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zinazohusu migodi mikubwa, kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta ya madini, kupitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchumbaji mkubwa unaofanywa na serikali, kuchambua na kuanisha haki na wajibu wa wekezaji na mwenye rasilimali (serikali), kukutana na chamber of mines na wadau wengine na kutoa taarifa yenye mapendekezo."
......

Kulikoni: Jumatano, Novemba 21, 2007

Hivi ni mimi tu au ni kwamba haya ni maneno ya ikulu kuhusu kile hii tume/kamati/? itafanya?

...kupitia mikataba ya madini?
...kuchambua mfumo wa kodi?
...kukutana na chamber of mines?

Haya si ndio exactly yalifanywa na tume ya kwanza na nyingine kibao zilizopita?! Mhhhhh....

Miezi mitatu sio mingi, yangu macho na masikio
 
“Kupitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zinazohusu migodi mikubwa, kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta ya madini, kupitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchumbaji mkubwa unaofanywa na serikali, kuchambua na kuanisha haki na wajibu wa wekezaji na mwenye rasilimali (serikali), kukutana na chamber of mines na wadau wengine na kutoa taarifa yenye mapendekezo.”

hapa ndipo tatizo lilipo. Sasa wale watakaokwepa hiyo kamati wanavunja sheria gani? Je kamati ina nguvu gani ya kuita mashahidi, vielelezo na kupata ushahidi wa kweli? Je kamati ina uwezo wa kuwaapisha wale watakozungumza nayo (wao wenyewe hawaapishwi) ili waseme ukweli wakitishiwa na kosa la kuongopea chombo cha haki (perjury)? Vinginevyo, wangeweza kuomba wataalamu toka vyuo vikuu kufanya hilo hilo bila kuundwa Kamati isiyo na meno!
 
Hivi ni mimi tu au ni kwamba haya ni maneno ya ikulu kuhusu kile hii tume/kamati/? itafanya?

...kupitia mikataba ya madini?
...kuchambua mfumo wa kodi?
...kukutana na chamber of mines?

Haya si ndio exactly yalifanywa na tume ya kwanza na nyingine kibao zilizopita?! Mhhhhh....

Miezi mitatu sio mingi, yangu macho na masikio

Uko sahihi Mwafrika wa Kike, kila mtu anajiuliza, kamati zote zimepeleka wapi ripoti zake? JK analijua hilo na sasa ameweka wapinzani mmoja wao ni mwenzetu tena kijana ambaye akiichezea hii nafasi ataharibu maisha yake yote ya baadaye kwa hiyo atatusaidia kujua hicho kilichofanya ripoti za kamati zilizopita zisiwekwe hadharani na zisiwe na manufaa wala kutekelezeka.. HEBU TUMUONE ZITTO kama kweli atashinda ama kufichua nguvu kubwa ya makampuni ya madini na mbinu zao za KIMAFIA, ambazo kina "CHACHA WANGWE" wameshindwa kuzing'amua tokea waanza kumtumia kule Tarime, katika maeneo ya mgodi wa North Mara.
 
Hivi endapo Zitto asingekuwa kwenye hiyo Kamati na kama kusingekuwa na mpinzani, je angeiunga mkono kuwa ndicho alichokitaka Bungeni?
 
Uko sahihi Mwafrika wa Kike, kila mtu anajiuliza, kamati zote zimepeleka wapi ripoti zake? JK analijua hilo na sasa ameweka wapinzani mmoja wao ni mwenzetu tena kijana ambaye akiichezea hii nafasi ataharibu maisha yake yote ya baadaye kwa hiyo atatusaidia kujua hicho kilichofanya ripoti za kamati zilizopita zisiwekwe hadharani na zisiwe na manufaa wala kutekelezeka.. HEBU TUMUONE ZITTO kama kweli atashinda ama kufichua nguvu kubwa ya makampuni ya madini na mbinu zao za KIMAFIA, ambazo kina "CHACHA WANGWE" wameshindwa kuzing'amua tokea waanza kumtumia kule Tarime, katika maeneo ya mgodi wa North Mara.

Halisi,

Mimi nakubaliana nawewe hapa kuwa maslahi ya Taifa yawe mbele na kuwa Zitto apewe nafasi ili kufanya hivyo. Sidhani pia kama kuna ugomvi au tatizo kati ya chacha wangwe na zitto au viongozi wa CHADEMA.

Mgongano na debate kali ndani ya CHADEMA ni kitu ambacho hata kimewashangaza wana CCM wengi ambao wengi wao bado wana sera za ndio mzee kwa kila viongozi wao wanachosema. Kinachoendelea hapa ni CHADEMA kuonyesha kuwa bila kujali nani ni nani ndani au nje ya chama, maslahi muhimu ya Taifa lazima yapitishwe baada ya mjadala mkubwa na sauti zote hata za upinzani kusikiwa.

Miezi mitatu sio mingi, Kama Zitto ameamua kuingia huko ndani na kama alivyosema kwenye makala ya raia mwema kuwa hatatereka na atakuwa imara, basi hakuna haja ya kumwamulia cha kufanya maana yeye ni mtu huru kabisa wa kuamua cha kufanya kwa manufaa yake na ya Taifa zima.

Thanks!
 
Hizi kamati zilikuwa zikipiga hela... Bila kuja na majibu yanayo ridhisha shitt...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom