Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 612
Kamati kuuchunguza mkataba wa Buzwagi
NA MWANDISHI WETU
Dar es Salaam
.Kuanza vikao vyake wiki ijayo Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Kamati ya kuangalia upya mikataba ya uchimbaji madini, Jaji Mark Bomani, amesema kamati yake itapitia mikataba yote ukiwamo ule wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, na kuweka bayana watakachobaini.
Akizungumza kwa simu na KULIKONI jana, Jaji Bomani alisema kamati yake itahakikisha inatimiza wajibu wake kwa kuangalia kila eneo linalohusu mikataba ya madini na kulitolea maelezo kama ilivyoanishwa katika hadidu za rejea.
Aliulizwa kama kamati yake itaangalia mkataba wa Buzwagi na kuzungumza na wahusika wakuu wa mkataba huo, alisema, Sisi tutaangalia yote na iliyona dosari tutasema na isiyo na tatizo pia tutasema. Tumepewa jukumu la kukutana na Chamber of Mining na wadau wengine kwa hiyo wote hao tutakutana nao.
Kauli hiyo ya Jaji Bomani imekuja huku kukiwa na wasiwasi kwamba baadhi ya wajumbe wana mahusiano ya karibu na wahusika wakuu wa mikataba ya madini wakimtaja na Peter Machunde wa Soko la Hisa la Dar es Salaam ambaye anatajwa kuwa na mahusiano ya kibiashara na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi.
Wajumbe wengine wa kamati hiyo walitajwa kuwa ni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, kupitia Chadema, Zitto Kabwe na Mbunge wa Bariadi Mashariki, UDP, John Cheyo, Dk. Harrison Mwakyembe (Kyela-CCM), Ezekiel Maige (Msalala-CCM) na Waziri wa zamani wa Biashara na Viwanda, Iddi Mohamed Simba.
Wajumbe wengine wametajwa kuwa ni pamoja David Tarimo wa PriceWater Coopers na Maria Kejo wa Wizara ya Sheria na Katiba, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Mugisha Kamugisha kutoka Wizara ya Fedha na Edward Kihundwa, ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Makazi, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
Kuhusishwa kwa Machunde na Karamagi ambaye ndiye hasa chimbuko la kupamba moto kwa mjadala wa madini kutokana na kusaini mkataba wa Buzwagi kimya kimya akiwa safarini London, kulijenga hisia za uwezekano wa kulindana lakini Jaji Bomani aanaondoa hofu hiyo kwa kusema hakuna mkataba utakaoachwa.
Jaji Bomani alisema maandalizi ya kuanza kwa vikao vya kamati yamo katika hatua za mwisho ikiwa ni pamoja na kuteuliwa kwa watendaji ambao wataunda sekretarieti ya kamati hiyo pamoja na kuwapelekea barua rasmi wajumbe wote ambao wameteuliwa.
Rais Jakaya Kikwete, alitimiza ahadi yake ya kuteua kamati ya kupitia mikataba ya madini, ahadi aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma hivi karibuni. Rais aliahidi kuingiza na wanasiasa kutoka upinzani.
Uteuzi wa wabunge wa upinzani umeibua mjadala mkubwa hususan kwa upande wa CHADEMA ambako baadhi ya viongozi wake wameonekana kutofurahishwa na uteuzi wa Zitto katika kamati hiyo na kutoa kauli za kukinzana katika siku za hivi karibuni.
Tayari Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ameitisha kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kujadili suala hilo ambalo linaashiria uwezekano wa kuwapo mgawanyiko mkubwa ndani ya chama hicho kilichoanza kupata wafuasi wengi katika siku za karibuni.
Hii ni mara ya pili kwa Zitto kuteuliwa na Rais, mara ya kwanza ikiwa ni katika kamati ya kupokea maoni ya uundwaji wa Shirikisho la Afrika Mashariki, uteuzi ambao ulipata baraka zote za Chadema na haukuwahi kupigiwa kelele.
Pamoja na baadhi ya watu kudai kwamba kamati hiyo haina hadidu za rejea, taarifa ya uteuzi wa kamati iliyosainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, ilizitaja kuwa ni pamoja na;
Kupitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zinazohusu migodi mikubwa, kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta ya madini, kupitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchumbaji mkubwa unaofanywa na serikali, kuchambua na kuanisha haki na wajibu wa wekezaji na mwenye rasilimali (serikali), kukutana na chamber of mines na wadau wengine na kutoa taarifa yenye mapendekezo.
Jaji Bomani alisema kati hiyo iliyopewa miezi mitatu kukamilisha kazi yake, inatarajiwa kuanza vikao vyake Dar es Salaam wiki ijayo baada ya wajumbe wote kupata barua kwa maelezo kwamba baadhi wako nje ya nchi na wengine mikoani.
Kulikoni: Jumatano, Novemba 21, 2007