Uchaguzi 2020 Kamati kuu ya CHADEMA, tunaomba mtuletee maazimio yafuatayo

Mimi kama mwananchi wa kawaida namshauri mheshimiwa mgombea angetumia muda huu kutengeneza video zinazolenga kuongea na ma group mbalimbali.

1. Kwa mfano video ya kwanza kuongea na watumishi wa umma kuwaelezea kwanini wamchague.

2. Kuongea na vijana na kuwapa sababu za kumchagua.

3. Kuongea na kina mama kuwanadia sera zake na kuwapa sababu.

4. Kuongea na walimu nk

5. Kuongea na wanafunzi wa vyuo vya elimu za juu nk

Yaani siku 7 zikiisha anatakiwa kila siku 2 au 3 anarusha video moja mtandaoni ambayo sio ndefu ila ilaelezea sera zake kwa makundi mbalimbali. Na huku anaanza tena kampeni nadhani itamuongezea mileage. Na kinaweza kuwa kimbunga kikubwa ambacho kinatapakaa kwa whatssap na social media zingine kwa muda mfupi. Ningekuwa mimi ndio meneja wa kempeni zake ningefanya hivyo.
 
Hii ni good idea, lakini je akifanya hivyo hawatamhesabia kuwa kafanya kampeni?
 
Kwa mujibu wa Katiba Lissu ana haki ya kwenda popote nchini, ana haki ya kwenda masokoni kununua bidhaa, ana haki ya kwenda sokoni kariakoo kununua matunda, kwenda Soko la Tandale, Kisutu, Mwananyamala na kwenye shopping malls zote kubwa. Ana haki ya kwenda kwa shoe shines kung'arisha viatu vyake, ana haki ya kuchukua aina ya magari ya watalii na kuzunguuka mijini etc
Nakuelewa sana ndugu.
 
Mimi kama mwananchi wa kawaida namshauri mheshimiwa mgombea angetumia muda huu kutengeneza video zinazolenga kuongea na ma group mbalimbali.

1. Kwa mfano video ya kwanza kuongea na watumishi wa umma kuwaelezea kwanini wamchague.

2. Kuongea na vijana na kuwapa sababu za kumchagua.

3. Kuongea na kina mama kuwanadia sera zake na kuwapa sababu.

4. Kuongea na walimu nk

5. Kuongea na wanafunzi wa vyuo vya elimu za juu nk

Yaani siku 7 zikiisha anatakiwa kila siku 2 au 3 anarusha video moja mtandaoni ambayo sio ndefu ila ilaelezea sera zake kwa makundi mbalimbali. Na huku anaanza tena kampeni nadhani itamuongezea mileage. Na kinaweza kuwa kimbunga kikubwa ambacho kinatapakaa kwa whatssap na social media zingine kwa muda mfupi. Ningekuwa mimi ndio meneja wa kempeni zake ningefanya hivyo.
Bonge la idea mkuu. I wish wazo hili lingechukuliwa.
 
Leo kamati kuu ya Chadema inakaa, naamini itajadili mambo mengi ikiwemo mwenendo mzima wa kampeni kuanzia uraisi hadi madiwani nchi nzima bila kusahau suala zito la kusimamishwa kufanya kampeni kwa ndugu Tundu Lissu.

Kwa minajili hiyo mimi kama mwananchi naomba kamati kuu iazimie yafuatayo

1. Ipinge na ilaani kwa nguvu zote katazo hilo na ilitangaze kuwa ni batili

Ukangalia hilo katazo dhidi ya mh Lissu, mchakato wake mzima tangu Mahera anatangazia umma kuwa wamemwandikia Lissu barua ya wito na kuifikisha kwa mhusika wakati ni uongo, mpaka siku Nyahoza anapeleka barua ya wito kwa bodaboda siku moja mbele baada ya tangazo a Mahera, Ukiangalia namna ambavyo mtuhumiwa hakuambiwa kwa maandishi Kosa lake halisi alilolifanya ili aandae utetezi juu ya kosa hilo kwa maandishi ndani ya masaa 48 kama kanuni zinavyosema, na ukiangalia kuwa Mtuhumiwa hakupewa nafasi ya kujitetea kwa kosa ambalo kimsingi halikutajwa ni nini haswa na wala hakukabidhiwa wito yeye mwenyewe. Kwa hiyo ni dhahiri maamuzi ya Kamati ya maadili ni batili na kamati kuu iutangazie umma kuwa maamuzi hayo ni batili, ya kiuonevu na iutangazie umma kuwa katazo hilo ni kinyume cha sheria na ni uonevu wa dhahiri dhidi ya mgombea wake wa uraisi

2. Kamati kuu impongeze heshimiwa Lissu na iwashukuru wananchi.

Kiukweli kabisa, Lissu kapiga kazi nzito, kuanzia wakati wa kutafuta wadhamini, mpaka wakati wa kampeni, Kanadi ilani ya chama kwa weledi mkubwa sana, kasaidia kuhuisha uhai wa chama na anaelekea kukipatia chama ushindi mnono. Chama kitoe azimio kumpongeza ndugu Lissu na kuwashukuru Watanzania kwa mwitikio mzuri na kuonyesha kukubali sera za Chadema

3. Kamati kuu impe mapumziko ndugu Lissu au Impangie majukumu mengine ya kichama ndani ya siku hizi saba

Kamati kuu kwa kutambua kazi nzito aliyofanya mheshimiwa Lissu inaweza kuamua kumpa Likizo ya mapumziko ya siku saba au ikaamua kumpa likizo ya siku tatu na ikampangia majukumu ya kujenga chama kwa siku nne. Kwenye kujenga Chama mheshimiwa Lissu atembelee ofisi za Chama na matawi yake, abadirishane mawazo na watendaji wa ofisi hizo na matawi hayo.
Lakini chama kikipenda kinaweza kumpangia mh Lissu kazi ya kunadi wagombea udiwani na Ubunge bila kujinadi yeye mwenyewe. Kufanya hivi siyo kosa kwa sababu kwanza mheshimiwa Lissu bado ni mtanzania ana haki ya kwenda popote nchini kwa mujibu wa katiba, na pili ni kiongozi halali wa Chama ana wajibu wa kuimarisha chama chake hata kama hajipigii kampeni. Nne ana haki zote za uhuru wa maoni na uhuru wa kujumuika (Freedom of association) katika kusanyiko lolote.

4. Kamati kuu imuagize Mwenyekiti ndugu Mbowe kuzunguuka sehemu mbalimbali za nchi na kuwapigia kampeni Madiwani na wabunge

Iwapo chama kitaamua Makamu Mwenyekiti (Yaani Tundu Lissu) awe kwenye mapumziko, ni wakati muafaka sasa Mwenyekiti afanye kama anavyofanya Kassim Majaliwa, yaani azunguuke sehemu mbalimbali za nchi kunadi wabunge wake na madiwani wake. Na atumie hadhara hizo kuwaeleza wananchi kwa nini Lissu hayuko kwenye kampeni, awaeleze kuwa ni sababu za uonevu tu na kutofuata sheria kwa tume.

LISSU MWENYEWE AFANYEJE

1. Kama akiamua kukaa Likizo ya siku kadhaa, basi ni muda muafaka wa kwenda kufanya Shopping kwenye masoko makubwa

Kwa mujibu wa Katiba Lissu ana haki ya kwenda popote nchini, ana haki ya kwenda masokoni kununua bidhaa, ana haki ya kwenda sokoni kariakoo kununua matunda, kwenda Soko la Tandale, Kisutu, Mwananyamala na kwenye shopping malls zote kubwa. Ana haki ya kwenda kwa shoe shines kung'arisha viatu vyake, ana haki ya kuchukua aina ya magari ya watalii na kuzunguuka mijini etc

2. Tembelea majirani zako hapo Tegeta na hani misiba

Pita kwa majirani zako, waulize habari zao katika miaka mitatu iliyopita wakati ulipokuwa haupo nchini, hani misiba yao, washukuru kwa sala zao na maombi yao.
Mtume Muhammad alifundisha kuwa Malaika Gabriel alimsisitiza sana sana kuwa vizuri mno na majirani mpaka mtume akaanza kuhisi kuwa labda hiyo ni amri mpya ya lazima kutoka kwa Mungu

3. Baada ya kukuzuia kufanya Kampeni, basi huu ndo muda wa kuendelea kuwashukuru wananchi kwa kukuchangia pale ulipopigwa risasi na pia kutoa elimu ya uraia

Watu walikuandama kuwa unaongelea sana kupigwa kwako risasi badala ya sera, Ulipoanza kumwaga sera rasmi wakapagawa mpaka sasa wamekuletea figisu. Sasa mheshimiwa Lissu hizi siku saba kwa kuwa wamekuzuia kumwaga sera, Huu ni muda wa kuzungumzia wewe kupigwa risasi, kulitaka jeshi la polisi lichunguze tukio, kuwashukuru wananchi kwa kukuchangia. Ukifanya hivi siyo kosa, ni haki yako ya kikatiba kuzungumza. Ukifanya hivi utakuwa hufanyi kampeni na hivyo siyo kosa kwa mujibu wa NEC. Pia unaweza kuendelea kutoa elimu ya uraia kwa wananchi, unaweza kuamua kufanya indoor au nje kwenye mikutano ya chama n. k

Missile of the Nation
Nimeipenda ile namba 4. Mh Mbowe achukue nafasi ya Lissu kwa hizo siku 7, kwa ratiba ile ile ya tume Mbowe apite. Ninafahamu kuwa Mh Mbowe ana uwezo mkubwa sana wa kuwakilisha hoja na wananchi watamuelewa. Na baada ya hapo Lissu aendelee.
 
Back
Top Bottom