Kamati Kuu ya CHADEMA, mkiteua wabunge wa Viti Maalumu kuingia Bungeni, mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana

Ndugu Chadema potezeeni hii Mada hapa jamvini..
Mshazoe kushika mshiko. Nawashauri msiache kwenda bungeni kwa Viti Maalumu
1. Mbowe
2.Mdee
jazia wengine!
 
Kwanza nianze kwa kusema kuwa, Katika vitu ambavyo CCM kwa sasa wanatamani vitokee, ni kupata wabunge wa upinzani japo wachache ili kuondoa dhana ya Bunge kuitwa Bunge la CCM-Bunge la chama kimoja.

Kwa sababu hiyo, tarajieni kuona wale wale waliowadhulumu haki zenu wakigeuka wema kwenu na kuanza kuonyesha upendo wa kinafiki kwenu na hata wako wataojidai kuwahurumia ila kamwe msiwaamini na wala msiwasikilize.

Hata hill Bunge likianza mtarajie wabunge hawa hawa wa CCM waliofaidika na matokeo haya, wakaanza kutoa kauli za kukumbuka michango ya wapinzani Bungeni ,na hata wanaweza kuja na mapendekezo ya kuwapa mialiko ya kwenda Bungeni kama wageni. Kumbukeni baadhi yao pia nafsi zao zitakuwa zinawasuta na watayatenda haya katika kujaribu kutuliza nafsi zao.

Sio hivyo tu,wanaweza kubadili sheria kuongeza idadi ya wabunge wa kuteuliwa na Raisi, na pia kubadili kanuni/sheria kuongeza wabunge wa vitu maalumu ili nyinyi mpewa nafasi, ila nawambieni kamwe msikubali bali waachieni wao na Bunge lao watimize azima yao na zaidi wakose kisingizio cha kuja kusema wapinzani wanachelewesha /wanakwamisha maendeleo.

Nawaambia angali mapema kabisa kuwa, mkiwa tayari kupeleka wabunge katika Bunge hili, basi pia muwe tayari na masimango: bila huruma ya Raisi au Spika,wengine msingekuwa humu ndani, tumewabeba, hamna shukurani na kauli zingine za aina hiyo pale mtapopishana nao mitazamo ndani ya hilo Bunge.

Pia, iwapo mtapeleka wabunge katika hili Bunge, matapoteza haki na uhalali wa kupinga huu uchaguzi na watatumia uwepo wenu katika hilo Bunge kama hoja ya kujibu tuhuma zozote zinazohusu makandokando ya huu uchaguzi.

Pia, tambueni hata wao wanaelewa mna wafuasi wengi sana katika nchi hii, hivyo ili kutuliza hasira na machungu ya mashabiki wa upinzani na zaidi chuki inayoweza kujengeka,watataka muwepo Bungeni walau kwa uchache na hapa viongozi wa juu wa vyama vya siasa vya upinzani wanaweza kujikuta katika mtihani wa kukubali ubunge wa kuteuliwa na hata kupewa vyeo serikalini.

Kwahiyo, Kamati Kuu ya CHADEMA, mkikaa myatafari haya yote na mengine ambayo sijayataja hapa kabla ya kufikiri kukubali kuteua wabunge wa vitu maalumu kuingia katika hili Bunge kwani mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana la kisiasa kwa kukubali kuwa sehemu ya hili Bunge ambalo uhalali wake ni wa kuhojiwa.

Agenda kuu inapaswa kuwa ni kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi na si kufikiria kuteua wabunge wa vitu maalumu kwenda katika hili Bunge.

Wapinzani, kama kweli mnataka kushika dola, basi lazima muwe tayari ku-sacrifice baadhi ya mambo vinginevyo msahau kuingia Ikulu.

No easy walk to freedom.
Niuzieni CHAMA chenu wakuu, ili nipeleke wabunge wangu bungeni.
 
Kama viongozi wa CHADEMA wana MTAZAMO mpana na chama basi hawatakiw kupeleka wabunge wa viti maalumu, ili kuwa na future kubwa na kuendelea kukubalika. Lakin kama wakitaka mwisho wa CHADEMA uwe 2025 basi wapeleke viti maalumu. Kupeleka viti maalumu kuta prove jambo moja ambalo ni hatari kisiasa, na jambo hilo ni 1:, itaonesha nguvu ya chadema ndipo ilipoishia kupata mbunge 1, ndio maana wamekubali kupeleka wabunge wa viti maalumu. 2 , wamekubaliana na matokea na zile kelele za awali ilikuwa hasira tu sasa zimeisha.
Finally, atakuja pole pole ataitaa press conference, kuwananga, asema mbona wamekubali special seat, does it mean hata matokeo wamekubali ilikuwa siasa tu. Then 2025, chadema itakuwa bye bye, maana wafuasi wengi watajua uchaguzi ulikuwa sawa, lkn chama kimepoteza mvuto hivyo hakuna wa kupapalika na CHADEMA tena. Mara Chadema inakuwa TLp version so sad. They need to act smart.
 
Umefikilia swala la kuwa chama kitaishi vipi?

Umefikilia swala la kuwa kimya kwa miaka mitano yote?

Unataka chama chako kiwe chama kikuu cha upinzani then utaki kupeleka wabunge bungeni
 
Wabongo ubinafsi ndio unaotumaliza. Majina yatapelekwa tu NEC. Watu hawapo kutetea mslahi ya wananchi bali matumbo yao, na famia zao.
 
Chama siyo Saccos. Kujali ruzuku badala ya kutetea principles ni kugeuka kuwa chama "ruzuku". Chama cha namna hiyo bora kife kije kingine kinachopigania chaguzi za wananchi ziheshimiwe na tupate mifumo ya kuwezesha hilo. Unfortunately hilo haliwezi kuwezekana kupitia bunge hili la CCM.

Chama kiendelee kutoa elimu ya uraia kwa wananchi kuhusu umuhimu wa tume huru ya uchaguzi na katiba mpya, Wananchi wao wenyewe watajua cha kufanya come the day isiyo na siku wala jina.
Lakini CCM wakuibie Ngamia kisha wakupe sungura na wewe unapokea tu huo ni ujuha na wananchi wataidharau Chadema zaidi.

Yaani wakuvurugie uchaguzi wa wabunge na rais, kisha wakupe viti maalum halafu useme eti ukipiga kelele bungeni kutetea wananchi watajali, let me tell you one thing They care nothing kuhusu kelelekelele hizi za eti maslahi ya wananchi, wangekuwa wanaheshimu maslahi ya wananchi wasingewadharau wananchi kwa kuwaharibia uchaguzi wao!
Mkuu una akili sana

Sent from my vivo 1611 using JamiiForums mobile app
 
Chadema msidanganywe ...hao wanaowambia msusie watawapa fedha za ruzuku...hao kweli wanaweza kuwachangia hata milioni hamsini kila mwezi..akili za kuambiwa changanya na za kwako. Mimi ninawashauri msisuse..mtaumia zaidi..afadhili kushiba kwa masimango kuliko kufa kwa njaa..wenzenu cuf walisusia Zanzibar walipata Nini...

si mmeona mwendo umekuwa ule ule..na Sasa hivi wasusie pia...wataendelea kupoteana.. kikubwa Mimi naona ruzuku Ni muhimu kwenye kujenga chama...kwa kauli yenu ya chadema msingi.

Kikubwa tumuonge mkono mheshimiwa rais kuijenga Tanzania yetu..kwa upendo na amani..uchaguzi umeisha tuijenge nchi sasa
We jamaa ni KILAZA kweli, kwani ile FAINI ya 300m nani alilipa?

Sent from my vivo 1611 using JamiiForums mobile app
 
Unawadanganya viongozi wako na unawaingiza chaka kabisa.Mwaka huu kulikuwa na wagombea urais 13 ccm inao uwezo wa kupata wabunge wa upinzani bila hata chadema na ACT kuwemo.Zanzibar Seif alususa lakini serikali haikusimama na ilikubalika kimataifa.
na hicho ndicho kinatakiwa kiwe kwa mazingira ya sasa. vinginevyo kukubali uteuzi ni tusi na dharau kubwa kwa cdm , act na waNanchi kwa ujumla na teuzi hizo katu na kamwe haziwez kujenga utawala wa kidemokrasia na kisheria ambayo ndiyo hoja ya msingi ya cdm act na wananchi walio wengi. mandela aliambiwa achugue kati ya kuacha kudai demokrasia lakin awe huru((yeye binafsi) au aendelee kudai demokrasia lakin aozee jela.....Madiba alichagua njia ngumu ya kuozea jela miaka 27 ili demokrasia ipatikane. njia iendayo motoni ni pana sana lakini ili iendayo mbinguuni ni nyembamba sana na ina miba na mateso mengi ila muda mrefu baada ya mateso inakufikisha mbinguni
 
Walioshinda ubunge kama yule dada wa Nkasi aende bungeni (japo namtilia shaka nyendo zake), viti maalum nao waende bungeni, na wale wanaoona wameonewa kwenye majimbo yao hawakushindwa kihalali waende mahakamani.

Jiwe ni mbabe, na hiki alichofanya kafanya makusudi akitegemea ndio atawapoteza Chadema kabisa, na ndio furaha yake, sasa namna ya ku deal na huyu mtu inahitajika akili ya ziada, sio kukubali defeat kirahisi kwa kugoma, he won't care.

Chadema lazima iendelee kusikika masikioni pa watanzania, zaidi wakiwa bungeni, na ni muhimu waendelee kutoa michango yao kwaajili ya maendeleo ya watanzania, sio kisirani cha mtu mmoja kiwaondoe relini, kwanza mwerevu siku zote hakasirishwi na mpumbavu.

Warudi bungeni wakapiganie Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi, na watumie platform nyingine zote kudai hivyo vitu viwili.

Kama ni kususa, huko kususa kusiishie bungeni tu, maana halisi ya kususa ni pana zaidi ya unavyofikiri; watatakiwa waendelee kususia mpaka uchaguzi mkuu ujao 2025, wasishiriki kama Tume itaendelea kubaki hii iliyopo, sio kususa kwenda bungeni halafu next time washiriki tena uchaguzi, na kwa kufanya hivyo ndio watakuwa wanajifuta wenyewe kwenye ramani ya siasa Tanzania.

Sasa kama wataamua kumsusia fisi butcher wakidhani wanamkomoa, pole zao.
Acha kuwadanganya hawakupigania katiba wakiwa wengi na vichwa wataweza leo ushauri wangu chadema wakubali kupoteza tu
 
Kama serikali inawatambua Hao watu ww ni Nani Mpaka ujifanye una akili Sana?

Kwani ccm hakuna matajiri?
Wale wakina Rostam, Asas, wale ni maskini?

Huna hoja
Hatukatai watu kuwa matajiri, swala ni kwamba hatutaki ujanja ujanja wa kula pesa za walipa kodi na kuwafanya walipa kodi wajinga. Mlevi wa Konyagi yeye ni kutumia Saccos kujitajirisha bila kufanya kile ambacho wananchi wa tanzania wanataka afanye. Mnalialia mambo ya dictatorship lakini mnaelewa kweli maana ya neno hilo? Au mnakariri tu kama kasuku?
 
Sijui elimu yako ni ya level gani
Umewahi kufatilia ukaguzi wa CIG kwa vyama vya siasa?
 
Kuna mnyukano huko wa hatari kina Matiko, Mdee, Bulaya, Magelesi and the likes wameunda women wing kushinikiza kamati kuu kuwaruhusu wateuliwe na kushiriki bingeni kama viti maalum, vinginevo wakiwahama wasilalamike.
Wahame tu,cdm ni taasisi si watu
 
Walioshinda ubunge kama yule dada wa Nkasi aende bungeni (japo namtilia shaka nyendo zake), viti maalum nao waende bungeni, na wale wanaoona wameonewa kwenye majimbo yao hawakushindwa kihalali waende mahakamani.

Jiwe ni mbabe, na hiki alichofanya kafanya makusudi akitegemea ndio atawapoteza Chadema kabisa, na ndio furaha yake, sasa namna ya ku deal na huyu mtu inahitajika akili ya ziada, sio kukubali defeat kirahisi kwa kugoma, he won't care.

Chadema lazima iendelee kusikika masikioni pa watanzania, zaidi wakiwa bungeni, na ni muhimu waendelee kutoa michango yao kwaajili ya maendeleo ya watanzania, sio kisirani cha mtu mmoja kiwaondoe relini, kwanza mwerevu siku zote hakasirishwi na mpumbavu.

Warudi bungeni wakapiganie Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi, na watumie platform nyingine zote kudai hivyo vitu viwili.

Kama ni kususa, huko kususa kusiishie bungeni tu, maana halisi ya kususa ni pana zaidi ya unavyofikiri; watatakiwa waendelee kususia mpaka uchaguzi mkuu ujao 2025, wasishiriki kama Tume itaendelea kubaki hii iliyopo, sio kususa kwenda bungeni halafu next time washiriki tena uchaguzi, na kwa kufanya hivyo ndio watakuwa wanajifuta wenyewe kwenye ramani ya siasa Tanzania.

Sasa kama wataamua kumsusia fisi butcher wakidhani wanamkomoa, pole zao.
Hiyo ndiyo umeona ni akili?
Hakuna kuruhusu mbunge wala diwani kwenda kuapa
Akienda yeyote afutwe uanachama papo hapo
 
Kweli chadema Mambo ya viti maaluum achana nayo Kama ni pesa za kuendesha chama wanachama watachangia, sio mda wa viti mahalum kwa Sasa mje na FAMILIA YA CHADEMA NCHI NZIMA KUSHIKAMANA NA KUSAIDIANA KATIKA SHIDA NA RAHA
CHADEMA miaka 5 ya ruzuku hakuna kilichofanyika

CHADEMA ikachangisha tiba ya Lissu, zikaliwa

CHADEMA ikachangisha fedha za kulipia kifungo cha viongozi wao, wasishukuri wala kuomba msamaha

CHADEMA hao hao wakatembeza bakuri la kampeni, kiongozi mjanja akazikwapua

Sasa ati mnataka kutembeza bakuri lingine, hamjifunzi?
 
Ruzuku za ccm zaidi ya billion kwa mwez wamefanya kitu gani?

Chadema ruzuku yao ni 250milion kwa mwez na ccm ni bilion moja plus

Unauliza mwenye pesa ndogo amefanya nn why usiulize mwenye pesa nyingi?
 
Back
Top Bottom