Kamati Kuu ya CHADEMA kukutana katika kikao chake maalum, siku ya Jumatano Agosti 15

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) itakutana katika kikao chake maalum, siku ya Jumatano Agosti 15, mwaka huu, kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali muhimu kuhusu chama na taifa kwa ujumla.

Kikao hicho kitakachofanyika jijini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Freeman Mbowe, kitajikita katika masuala mawili; kupokea taarifa na kujadili kwa kina juu ya chaguzi za marudio za ubunge na udiwani na hali ya siasa nchini.

Wanachama wa CHADEMA na umma wa Watanzania kwa ujumla utatarifiwa kuhusu maazimio baada ya kikao hicho.

Imetolewa leo Jumanne, Agosti 14, 2018 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
 
Chadema achaneni na chaguzi za hovyo, waache wapite kama watakavyo maana hakuna sababu ya kupoteza jela yenu huku mkijua jiwe alishaamrisha kuwa wapinzani hata wakipata kura nyingi lazima mgombea wa ccm atangazwe mshindi kama yeye alivyotangazwa na NEC wakati mshindi alikuwa el
 
Watawala wanaichezea amani yetu
Muda sio mrefu tutalia na kusaga meno
 
Hicho kikao kama kitatoka na lawama kwa serikari kama siku zote bora wasikae kabisa kuharibu pesa za ruzuku, sasa hivi wapenda haki tunataka kusikia namna gani tunafanya kupata tume huru ya uchaguzi na katiba mpya(Busara hazina nafasi tena kwa hawa walevi wa madaraka), Mbowe na hizo busara zake bora akae tu kimya, watu wameumizwa sana kwa ajili ya chama, chama hakina nguvu tena ya kupambana na wababe, chama kimejaa busara mbele ya watu wasio na hekima wala busara, Bila uimara wa Dr. Dlaa wakati wa Kikwete uwenda naye angekua kama Jiwe, ila alithibitiwa na wananchi waliwekwa tayari muda wote. Sasa Jiwe sasa anajifanyia anachotaka kwa sababu ashajua Chadema wanajidai wazee wa busara.
 
Kuna watu wanaamini kukaa kimya ni busara. tukikubali hilo basi kila mtu anaweza kunyamaza na kila mtu akapata busara. Hiyo haiwezekani. Tunawaomba viongozi wa upinzani mkuu, CHADEMA na hasa Mh. Mbowe ujitokeze ili tupate ufafanuzi wa mashitaka tunayopata toka kwa hawa wanaohama. MUnapoonewa mara nyingi kelele zenu tunazisikia. Iwje sasa hatuwasikii?

Mbowe unatuhumiwa kutumia chama kama mradi wako. Je, ni kweli ndani ya chama unajiamulia wewe pamoja na walio karibu nawe? Ni kweli unajilipa madeni yasiyo na mwisho, mwaka hadi mwaka? Binafsi naweza kukubali maana sioni maendeleo ya chama pamoja na ruzuku munazopata, misaada wakati wa uchaguzi toka vyama rafiki na hata akina Sabodo. Kwa nini mmeshindwa hata kujenga jengo la chama mkoa wowote ule. Muko wapi? Hata wapiga kelele wazoefu hatuwasikii.

Kwa ubora huu basi, CCM watawanunua kwa bei ya bure.
 
Back
Top Bottom