Kamati Kuu ya CCM Yaridhia Kikwete kusuka upya Baraza lake la Mawaziri

Rais mpaka apate baraka za CC ndinyo avunje baraza la mawaziri?? Si alisema hana ubia na mtu kwenye Urais sasa inakuwaje anatafuta baraka za akina Nape??? No wonder Nape ana kibri sana!!
 
Kamati Kuu iliyokutana leo tarehe 27/04/2012 chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dar es salaam, pamoja na mambo mengine imefanya yafuatayo.;

A. UTEUZI
Kamati Kuu imeteua wafuatao kuwa makaimu Katibu wa mikoa. Vituo vyao vya kazi vitapangwa baadae. Uteuzi huu unatokana na kuwepo kwa mikoa wazi mitano, mikoa hiyo ni;

Geita
Njombe
Simiyu
Katavi
Magharibi
Hivyo wafuatao wameteuliwa kuwa makaimu katibu wa CCM wa Mikoa.

1. Ndg. Hilda Kapaya
2. Ndg. Shaibu Akwilombe
3. Ndg. Hosea Mpangile
4. Ndg. Alphonce Kinamhala
5. Ndg. Aziz Ramadhani Mapuri

B. HALI YA KISIASA:
Rais amepokea taarifa na maazimio ya Kamati ya wabunge wa CCM na Kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM juu ya kilichotokea kwenye bunge lililopita mjini Dodoma.

Taarifa hizo zimewasilishwa kwenye kamati kuu na kujadiliwa. Pamoja na taarifa hizo kamati Kuu imepokea taarifa ya jinsi Rais alivyojipanga kuchukua hatua za kuwawajibisha mawaziri na watendaji wa serikali na wale wa mashirika ya umma waliobainika kuhusika na ubadhirifu ulioinishwa na taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali, Kamati za kudumu za bunge na wabunge bungeni.

Kamati Kuu imeamua yafuatayo;
1. Kamati Kuu inatambua na kuheshimu haki na wajibu wa wabunge kujadili utendaji wa serikali yao.Inapongeza juhudi za serikali kuhakikisha kuwa ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali inajadiliwa kwa uwazi na hivyo kuibua mapungufu yaliyojadiliwa.

2. Kamati Kuu imeridhika na imebariki uamuzi wa Rais KULISUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI na taasisi zingine zilizoanishwa katika ripoti hizo. Imesisitiza utekelezaji wa uamuzi huo ufanywe mapema iwezekanavyo.

Aidha kamati Kuu imeipongeza Kamati Teule ya baraza la wawakilishi Zanzibar iliyoundwa kuchunguza utendaji katika sekta mbalimbali kwenye serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa taarifa yao.

Kamati Kuu inawapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jinsi walivyojadili taarifa hiyo na pia Kamati Kuu inaipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuipokea taarifa na kuanza kuifanyia kazi.


Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
The Ideology and Publicity Secretary
Mbona kamati kuu haijapongeza wabunge wa upinzani na wachache wa magamba waliosukuma hawa mawaziri kujiuzulu na kusaini paper ya kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu na serikali yake??
 
Sikutegema maamuzi ya kuvunja baraza la mawaziri yatatokana na kikao cha chama bali uamuzi wa rais mwenyewe kutokana na sababu zilizomridhisha yeye.

Pengine naweza sema hatua hii imedhihirhsa udhaifu wa JK zaidi kutokana na ile tabia ya kuogopa maamuzi ya CC kama ilivyotokea ktk muswada wa sheria ya Katiba mpya. JK aliwaambia wazi viongozi wa Upinzani kwamba alihofia kuchukua maamuzi tofauti na chama chake japokuwa alikubaliana na hoja zao kimsingi.

Hivyo japokuwa analivunja baraza zima lakini lengo la kina El ndio linafuata hivyo tusubiri kundi la EL ambao sasa wanajiweka ktk nafasi nzuri ya kugombea uchaguzi wa mwaka 2015.

Kifupi shamba linapaliliwa kwa maandalizi ya 2015 sio uwajibikaji kiutawala maana sheria haitafuatwa, hakuna atakaye simamishwa mahakamani wala kuhojiwa baada ya hapa, hivyo CAG haitapata majibu.. DEJAVU kama ile ya EL na kina Karamagi. Tutafungashiwa usafi ambao utakuwepo kwa muda tu kurudisha imani ya wananchi kwa chama tawala. Tujiandae na purukushani za hadaa kujivua magamba bila kutolewa meno ya sumu. Hili ndio lengo la kikao kizima cha CC ili kutufungashia kanyaboya, wananchi msidanganyike!
kwa hiyo tuseme saini za kutuokuwa na imani ulikuwa mkakati wa nitoke vipi?
 
Chanel ten

Ni taarifa toka ikulu kuwa kamati hiyo imemkubalia rais wao kubadili baraza la mawaziri.

Sasa sijui chama na serikari tofauti yake nini hivi ikulu ndo genge la kukutania chama na kivp chama kina mamlaka ys kuingilia mamuzi ya taasisi kama ya rais?
 
mkuu hapa chama na serikali ni kitu kimoja. Wanatumia facility za serikali kwa shughuli za chama.
 
Mi nasikitika sana linapovunjwa baraza ni mzigo kwa serikali kuna gharama nyingi inatumika kuwalipa mafao yao na pia kuwalipa mafao hao wapya watakapokuja na ishu nyingine kedekede napinga kwa nguvu zote baraza kuvunjwa na tutaandamana kupinga lisivunjwe!!
 
Mawazili wote waliohusika wapelekwe mahakamani na sio kujiuzuru tu


Kajifunze kiswahili kwanza. Hili ni pigo kwa wale waliodhani Rais na Waziri Mkuu watafarakana, na hasa mafisadi na mawakala wao.
 
Chanel ten

Ni taarifa toka ikulu kuwa kamati hiyo imemkubalia rais wao kubadili baraza la mawaziri.

Sasa sijui chama na serikari tofauti yake nini hivi ikulu ndo genge la kukutania chama na kivp chama kina mamlaka ys kuingilia mamuzi ya taasisi kama ya rais?

Hiki ni kituko cha mwaka, tangu lini rais akapata kibali cha c.c kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri?
 
Hivi jamani, cc ya ccm ndio inausika kwenye kuvunja baraza la mawaziri? Kazi ipo...
Tuwavumilie, itachukua muda mrefu kidogo kutenganisha utendaji wa serikali na chama cha siasa. Mpaka hapo tutakapoondokana na maneno 'Viongozi wa Chama na Serikali'. Haya maneno bado yanatumika mpka leo!!
 
Haya, wameumbuka wote waliokuwa wanakebehi! Eti Kikwete hawezi kuchukua maamuzi magumu. Sasa kuna maamuzi magumu kisiasa kuliko kusuka upya Baraza la Mawaziri? Jamani, mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe. JK kaza uzi uzidi kuwaacha utupu wambea wote.
 
kama hatambadilisha pinda,uozo utaendelea!jee hao wabadhirifu watafikishwa mahakamani?
 
Mawaziri jambazi wote wafikishwe mahakamani,haitoshi kuvuna baraza halafu kina NGEREJA WAENDELEE KUPETA.Na uwaziri kiranja apewe MR MITUSI LIMITED,Lusinde ktk Jimbo linaongoza kwa wananchi OMBAOMBA La mtera pale Dom.
 
Kwahiyo Rais hana ruksa ya kubadili baraza lake la mwawaziri bila kuwauliza cc ya chama chake? Kumbe Urais wake ni wa ubia na cc! Siku za nyuma tulishaambiwa kuwa urais wake hauna ubia.
 
Mawaziri jambazi wote wafikishwe mahakamani,haitoshi kuvunja baraza halafu kina NGEREJA WAENDELEE KUPETA.Na uwaziri kiranja apewe MR MITUSI LIMITED,Lusinde ktk Jimbo linaongoza kwa wananchi OMBAOMBA La mtera pale Dom.
 
Back
Top Bottom