Kamati Kuu ya CCM Yaridhia Kikwete kusuka upya Baraza lake la Mawaziri

Mawaziri 8 kuhusishwa na ufisadi/ufujaji wa mali ya Umma ni anguko la Serikali... Tunasubiri hatua zaidi zitokanazo na ripoti ya CAG na ya Kamati ya Bunge ya Mahesabu ya Serikali!!!!!
 
labda kama Mtoto wa mkulima naye kaweka shinikizo na kulia , kwa kusema nimedhalilishwa saana, ili ionekane waziri mkuu hafai blah blah blah, sasa nasema hivi uwatoe hao mawaziri au mimi naenda zangu kibaoni kulima na kuangalia miradi mingine.
 
Raisi anapokea maazimio ya Bunge la Jamhuri ya Tanzania au ya wabunge wa CCM?

Hilo ndio swali la kujiuliza.
Inamaana alikuwa haoni umuhimu wa kulivunja hilo baraza la mawaziri mpaka apate ushauri wa nape na mukama?
Kwa vile hii motion ilianzishwa na upinzani, thats why ameonelia aimalize kwa style hii.
Huyu rais ni hopeless ana mambo ya ngomani sana.
 
Mzigo mwingine kwa wananchi....

Andaeni fomu za malipo ya penseni za kila mwezi na kiinua mgongo kwa hao wanaoondoka.
 
Hilo ndio swali la kujiuliza.
Inamaana alikuwa haoni umuhimu wa kulivunja hilo baraza la mawaziri mpaka apate ushauri wa nape na mukama?
Kwa vile hii motion ilianzishwa na upinzani, thats why ameonelia aimalize kwa style hii.
Huyu rais ni hopeless ana mambo ya ngomani sana.

Mkuu kwani hukuwahi kusikia alienda Bagia ya Moyo kwenye ngoma ya mmoja wa wanandugu?
 
CLOUDS TV WALITUPIA MAANDISHI YAFUATAYO MUDA WA DAKIKA ISHIRINI ZILIZOPITA!!!!!
Kamati Kuu ya CCM iliyoketi leo Jijini Dar es Salaam Imeridhia Uamuzi wa Mwenyekiti wake Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE kulivunja na kulisuka Upya BARAZA LA MAWAZIRI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Mimi wa Rufiji haya mambo ya mjini niwekeni sawa wakuu, kwani huyu Rais anafanya kazi kwa maelekezo ya CCM au ni nini humuongoza kutekeleza majukumu yake?

Kama sieleweki, swali langu ni hili: Kama Rais ameona ipo haja ya kuvunja baraza na CC ya MAGAMBA haikuridhia, ina maana Rais hawezi kulivunja? Na kama itakuwa hivyo, mbona kelele zetu hatukuzielekeza kwa CC ya CCM na badala yake ikawa PINDAAA PINDAAA?!
 
1. Hili liwe fundisho kwa viongozi wetu. Hawataki kujiuzulu hadi wawajibishwe.. ivi waliposhutumiwa na kutakiwa wafanye hivyo wangejiuzulu haya yangetokea??

2. Hili ni jawabu kuwa CCM imeshindwa kuongoza na pia uteuzi wa JK haukuwa makini na kuwa anateua marafiki zake bila kuangalia uwezo. Hii ni kulichezea taifa na kufanya majaribio ya kuongoza nchi kwa kuchezea kodi za wananchi... kila mmoja anapewa ale kisha aende zake....Fadhila.... Wapo kina karamagi, chenge..nk... watu walifanya mambo ya hovyo kabisa lakini wapo tuu wanapeta...hata hapa ataondoa baadhi wengine wataendelea kupeta wakati ripoti zipo wazi.. hii nchi inachosha sasa inafikia wakati wa kuona aibu kusema unatokea Tanzania....Haya ndio matokeo ya kupiga kura hovyo na kutokulinda kura.... hili liwe fundisho 2015.
 
Taarifa inasema KULISUKA UPYA BARAZA LA MAAZIRI, sasa hizi taarifa za kulivunja zinatoka wapi?
kumbuka kulisuka upya maana yake anaweza badilisha baadhi ya mawaziri bila kumgusa Waziri mkuu.
 
iwe maapema isiwe ni upepo ili kutupooza
ifanywe ndanai ya wiki moja.
nimemsikia Nape BBC swahili mda huu akizungumzia pia kuwajibiswa kwa wote waliohusika.
kama kweli wana nia hiyo basi tutaujua ukweli wameshaona wananchi wanahama na kutubu dhambi ya kuwa magamba
na kujivika upya ngozi ya mwanakondoo yaani Chadema, na CUF huko tandahimba
 
Back
Top Bottom