Kamati Kuu ya CCM Yaridhia Kikwete kusuka upya Baraza lake la Mawaziri

Ng`wanakidiku

JF-Expert Member
Apr 18, 2009
1,195
232
Kamati Kuu iliyokutana leo tarehe 27/04/2012 chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dar es salaam, pamoja na mambo mengine imefanya yafuatayo.;

A. UTEUZI
Kamati Kuu imeteua wafuatao kuwa makaimu Katibu wa mikoa. Vituo vyao vya kazi vitapangwa baadae. Uteuzi huu unatokana na kuwepo kwa mikoa wazi mitano, mikoa hiyo ni;

Geita
Njombe
Simiyu
Katavi
Magharibi
Hivyo wafuatao wameteuliwa kuwa makaimu katibu wa CCM wa Mikoa.

1. Ndg. Hilda Kapaya
2. Ndg. Shaibu Akwilombe
3. Ndg. Hosea Mpangile
4. Ndg. Alphonce Kinamhala
5. Ndg. Aziz Ramadhani Mapuri

B. HALI YA KISIASA:
Rais amepokea taarifa na maazimio ya Kamati ya wabunge wa CCM na Kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM juu ya kilichotokea kwenye bunge lililopita mjini Dodoma.

Taarifa hizo zimewasilishwa kwenye kamati kuu na kujadiliwa. Pamoja na taarifa hizo kamati Kuu imepokea taarifa ya jinsi Rais alivyojipanga kuchukua hatua za kuwawajibisha mawaziri na watendaji wa serikali na wale wa mashirika ya umma waliobainika kuhusika na ubadhirifu ulioinishwa na taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali, Kamati za kudumu za bunge na wabunge bungeni.

Kamati Kuu imeamua yafuatayo;
1. Kamati Kuu inatambua na kuheshimu haki na wajibu wa wabunge kujadili utendaji wa serikali yao.Inapongeza juhudi za serikali kuhakikisha kuwa ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali inajadiliwa kwa uwazi na hivyo kuibua mapungufu yaliyojadiliwa.

2. Kamati Kuu imeridhika na imebariki uamuzi wa Rais KULISUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI na taasisi zingine zilizoanishwa katika ripoti hizo. Imesisitiza utekelezaji wa uamuzi huo ufanywe mapema iwezekanavyo.

Aidha kamati Kuu imeipongeza Kamati Teule ya baraza la wawakilishi Zanzibar iliyoundwa kuchunguza utendaji katika sekta mbalimbali kwenye serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa taarifa yao.

Kamati Kuu inawapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jinsi walivyojadili taarifa hiyo na pia Kamati Kuu inaipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuipokea taarifa na kuanza kuifanyia kazi.

Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
The Ideology and Publicity Secretary

Ijumaa, 27 Aprili 2012

Kikwete atafanya mabadiliko ya baraza la mawaziri

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ameiarifu kamati kuu ya CCM kwamba atafanya mabadiliko kufuatia shutuma za matumizi mabaya ya fedha.

"Kamati kuu imepokea kwa furaha na kwa kweli imeridhia na kubariki uwamuzi wa rais wa Jamhurri ya Muungano wa Tanzania, kulisuka upya baraza la mawaziri'" amesema Nape Nnauye.

Kufuatia mjadala mkali bungeni kuhusu matumizi mabaya ya fedha na juhudi za kutaka kuwasilisha hoja ya kutokua na imani na Waziri Mkuu, Rais Kikwete ameiarifu kamati kuu ya chama tawala cha CCM katika kikao cha dharura kwamba atafanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nnauye ameiambia Sauti ya Amarika kwamba, "kamati kuu imepokea kwa furaha na kwa kweli imeridhia na kubariki uwamuzi wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kulisuka upya baraza la mawaziri, na kuwawajibisha mawaziri kwa mujibu wa jinsi walivyohusika na kuhusishwa kwenye zile taarifa."

Mahojiano na nape nnauye

icon-download.gif
Download: MP3
Right click (Control click for Mac) and choose Save Link/Target As

Bw. Nnauye alisema mbali na kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri atawawajibisha watendaji wa serikali na baadhi ya mashirika ya umma, ambao wamehusishwa kwenye hizo taarifa.
Msemaji wa Ikulu Salva Rweyemamu amethibitisha uwamuzi huo alipozungumza na Sauti ya Amerika akisema Rais mwenyewe ndiye aliyeliagizia bunge kujadili kwa kina ripoti zote za kamati ya mahesebu ya serikali kwa sababu hiyo ndio kazi ya bunge.

Mahojiano na Salva Rweyemamu

icon-download.gif
Download: MP3
Right click (Control click for Mac) and choose Save Link/Target As

Anasema kufutia matokeo ya ripoti na mapendekezo ya wabunge Rais hana budi ila kuchukua hatua kulingana na jinsi anavyo ona yeye binafsi.
Bw.Rweyemamu anasema hajui lini Rais Kikwete ataamua kufanyamabadiliko ya baraza la mawaziri lakini haitachukua muda mrefu kabla ya yeye kuwaarifu wananchi juu ya uwamuzi wake.
 
[h=6]CLOUDS TV WALITUPIA MAANDISHI YAFUATAYO MUDA WA DAKIKA ISHIRINI ZILIZOPITA!!!!!
Kamati Kuu ya CCM iliyoketi leo Jijini Dar es Salaam Imeridhia Uamuzi wa Mwenyekiti wake Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE kulivunja na kulisuka Upya BARAZA LA MAWAZIRI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.[/h]
 
Hii tabia ya kuweka thread kama ni habari kamili huku mahudhui yakiwa tofauti na heading imeshamiri sana humu JF nowdays, jaribuni kupita tu kama hamna news ya kupost.
 
Kwamujibu wa chanzo changu cha kuaminikika toka kikaokiku cha mkutano wa cc ya ccm, kinapasha kuwa baraza lote la mawaziri limevunjwa!

Nimejiridhisha na habari hii,asilimia 99%

Confirmed!

Rasmi baraza limevunjwa, sasa rais kuunda baraza jipya!
 
Kamati Kuu iliyokutana leo tarehe 27/04/2012 chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dar es salaam, pamoja na mambo mengine imefanya yafuatayo.;

A. UTEUZI
Kamati Kuu imeteua wafuatao kuwa makaimu Katibu wa mikoa. Vituo vyao vya kazi vitapangwa baadae. Uteuzi huu unatokana na kuwepo kwa mikoa wazi mitano, mikoa hiyo ni;

Geita
Njombe
Simiyu
Katavi
Magharibi
Hivyo wafuatao wameteuliwa kuwa makaimu katibu wa CCM wa Mikoa.

1. Ndg. Hilda Kapaya
2. Ndg. Shaibu Akwilombe
3. Ndg. Hosea Mpangile
4. Ndg. Alphonce Kinamhala
5. Ndg. Aziz Ramadhani Mapuri

B. HALI YA KISIASA:
Rais amepokea taarifa na maazimio ya Kamati ya wabunge wa CCM na Kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM juu ya kilichotokea kwenye bunge lililopita mjini Dodoma.

Taarifa hizo zimewasilishwa kwenye kamati kuu na kujadiliwa. Pamoja na taarifa hizo kamati Kuu imepokea taarifa ya jinsi Rais alivyojipanga kuchukua hatua za kuwawajibisha mawaziri na watendaji wa serikali na wale wa mashirika ya umma waliobainika kuhusika na ubadhirifu ulioinishwa na taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali, Kamati za kudumu za bunge na wabunge bungeni.

Kamati Kuu imeamua yafuatayo;
1. Kamati Kuu inatambua na kuheshimu haki na wajibu wa wabunge kujadili utendaji wa serikali yao.Inapongeza juhudi za serikali kuhakikisha kuwa ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali inajadiliwa kwa uwazi na hivyo kuibua mapungufu yaliyojadiliwa.

2. Kamati Kuu imeridhika na imebariki uamuzi wa Rais KULISUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI na taasisi zingine zilizoanishwa katika ripoti hizo. Imesisitiza utekelezaji wa uamuzi huo ufanywe mapema iwezekanavyo.

Aidha kamati Kuu imeipongeza Kamati Teule ya baraza la wawakilishi Zanzibar iliyoundwa kuchunguza utendaji katika sekta mbalimbali kwenye serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa taarifa yao.

Kamati Kuu inawapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jinsi walivyojadili taarifa hiyo na pia Kamati Kuu inaipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuipokea taarifa na kuanza kuifanyia kazi.

Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
The Ideology and Publicity Secretary
 
Kwamujibu wa chanzo changu cha kuaminikika toka kikaokiku cha mkutano wa cc ya ccm, kinapasha kuwa baraza lote la mawaziri limevunjwa!

Nimejiridhisha na habari hii,asilimia 99%

100% Nape amesikika katika Clouds fm kuwa CC imeridhia ripoti ya CAG
 
Unataka kupaisha jina lako wakti lipo juu but sio jina lako na surname yenyewe haikusaidii.
 
Hivi jamani, cc ya ccm ndio inausika kwenye kuvunja baraza la mawaziri? Kazi ipo...
 
Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM iliyoketi leo Jijini Dar es Salaam imeridhia uamuzi wa Mwenyekiti wake Rais JAKAYA KIKWETE kuvunja na kulisuka upya Baraza la Mawaziri wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uamuzi huo wa Rais KIKWETE wa kuliunda upya Baraza hilo umekuja baada ya kupokea taarifa ya maazimio ya Kamati ya Wabunge wa CCM iliyoketi Mjini Dodoma wakati wa vikao vya mkutano wa saba wa bunge uliomalizika hivi karibuni.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa NAPE NNAUYE ameeleza kuwa pamoja na Kamati Kuu kuridhia uamuzi wa Rais KIKWETE pia imemtaka awawajibishe watendaji wakuu wa Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali ambao wamehusika katika ubadhirifu wa mali na rasilimali za umma.

Katika hatua nyingine Kamati Kuu imeipongeza Kamati teule ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa ripoti yao ya uchunguzi iliyobaini ubadhirifu katika baadhi ya sekta ndani ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Chanzo, bonyeza hapa
 
Back
Top Bottom