Kamati Kuu ya CCM yakutana leo Ikulu kwa dharura!

Status
Not open for further replies.
- The dataz ni kikao cha dharura cha Kamati Kuu CCM, leo jijini Dar; ninataka kuamini agenda itakuwa mawaziri kujiuzulu, kuvunjwa cabinet, na kukirekebisha chama maana sio siri kinakokwenda sio kuzuri sana.

- Lets wait and see!

Es!
 
- The dataz ni kikao cha dharura cha Kamati Kuu CCM, leo jijini Dar; ninataka kuamini agenda itakuwa mawaziri kujiuzulu, kuvunjwa cabinet, na kukirekebisha chama maana sio siri kinakokwenda sio kuzuri sana.

- Lets wait and see!

Es!

Utazidi kutujuza maana saizi masikio yote ni Singida hukumu ya Tundu Lissu.
 
Hakuna lolote hapo ! mwenyewe alishasema UPEPO UNAPITA kama wa DOWANS, EPA LOLIONDO na mengineyo ! mtajiumiza bure kusubiri ! bora mtafute kazi za kufanya!
 
Na wewe wakuvue uanachama kwa kutoa rushwa kwenye uchaguzi wa EAC na kukiuka misingi ya chama chenu!!
 
Kwa nini JK anainajisi ikulu ambapo ni mahali patakatifu kwa kufanyia huko vikao vya CCM chama kilichojaa ufisadi wizi na kila uovu? kwa nini asifanyie Lumumba au Ofisi zingine za chama? Hivi JK hana hata uwezo kidogo tu wa kufikiria na kutenganisha shuguli za chama na shuguli za serikali?Dawa sio kuliweka baraza viraka ni kulivunja na kuweka watu wapya kabisa na ikiwezekana hata yeye mwenyewe aondoke tu!!
 
kwa niin vikao vya chama vifanyike ikulu ??? ina maana rumumba hakuna ofisi?
 
Jamani huyu kingwete ana kazi kweli atapata wapi mawaziri wakati ccm wote mafisadi mpaka wenyeviti wa mitaa mafisadi?? Labda akusanye wizara zote atafutepo mawaziri watatu...
 
Kwahiyo Hii Habari ni Uongo?

Kamati Kuu CCM kukutana leo Dar

Ijumaa, Aprili 27, 2012 05:26 Na Mwandishi Wetu - MTANZANIA

*Kujadili mabadiliko ya Baraza la Mawaziri
*Hoja ya wabunge wa CCM kuwasilishwa
*Mawaziri wapya watakaorithi mikoba watajwa
*Wamo Zambi, Tizeba, Makamba, Kigwangala

KAMATI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC), inakutana Dar es Salaam leo chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya chama hicho ambazo Mtanzania imezipata, kikao hicho kitafanyika Ikulu, kuanzia saa 4.00 asubuhi.

Chanzo hicho cha habari kilieleza kuwa wajumbe katika kikao hicho watajadili hoja mbalimbali ikiwamo hali ya siasa ndani ya chama hicho na utendaji wa Serikali.

Nyingine ni kuhusu mabadiliko ya baraza la mawaziri na mapendekezo ya wabunge wa CCM kuhusu kujiuzulu kwa mawaziri wanane wanaolalamikiwa kwa uzembe na ubadhirifu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mwenyekiti wa wabunge wa CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Katibu wake Jenista Mhagama, watawasilisha mapendekezo yaliyofikiwa mjini Dodoma na wabunge wa CCM katika kikao hicho (party caucus).

Chanzo hicho kilieleza kuwa kikao hicho kimeitishwa kufanya mabadiliko ya baraza la mawaziri ili kuifilisi CHADEMA na azma yake ya kutaka kwenda kwa wananchi na hoja ya kujiuzulu kwa mawaziri hao.

"Unajua kaka siku zote caucus ya CCM imekuwa ikikutana na kutoa mapendekezo lakini mapendekezo yamekuwa hayafanyiwi kazi, safari hii imekuwa tofauti.

"Hii hoja ya kutaka waziri mkuu apigiwe kura ya kutokuwa na imani na mawaziri wazembe wajiuzulu imekuwa tishio kubwa na chama kimeamua kuchangamka.

"Umesikia mwenyewe CHADEMA wametangaza kwenda kwa wananchi na hoja hii, tumesikia kamati kuu yao inakutana kesho au keshokutwa kujipanga.

"Sasa Rais Kikwete ameamua kufanya haraka kumaliza suala hili kabla hawajakutana ili kuwafilisi ajenda hiyo. Lengo ni kukinusuru chama mbele ya safari," kilisema chanzo hicho.

Kuhusu mabadiliko ya baraza la mawaziri, chanzo hicho kilisema mkakati mzima kuhusu suala hilo umekamilika na majina ya wabunge wa CCM watakaochukua nafasi za mawaziri watakoondolewa yako wazi.

Chanzo hicho kilitaja baadhi ya wabunge wanaotarajiwa kuingia katika baraza jipya kuwa ni pamoja na Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi.

Wengine ni Mbunge wa Handeni, Dk. Abdallah Kigoda, Mbunge wa Nzega, Dk. Khamis Kigwangala na Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile.

Wengine ni Mbunge wa Buchosa, Dk. Charles Tizeba, Mbunge wa Bumbuli, January Makamba na Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele.

Baraza la mawaziri linaundwa kwa kuzigatia kanda, ambako kwa mfano, akiondoka Naibu Waziri wa Uchukuzi, Athumani Mfutakamba, Mkoa wa Tabora lazima upate mtu wa kujaza nafasi hiyo.

Anapoondoka Waziri wa Uchukuzi, Omary Nundu ambaye ni Mbunge wa Tanga Mjini, mkoa huo lazima upate waziri kujaza nafasi hiyo kulingana na mgao wa katika kanda.
 
Nilijaribu kuchangia kwenye topic ya kwanza, inasema hii ni topic tofauti You Don't Have Permission by Admin
 
Rais JMK amegoma katakata kuvunja baraza la mawaziri.anasema kuwa mawaziri wake wanasingiziwa halafu hoja ya kuwaondoa zaidi imetoka upinzani hivyo akifanya hivyo atakuwa amewapa wapinzani ushindi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom