Kamati kuu ya ccm yaipongeza tume ya warioba - viva jk

Mtumbatu

Mtumbatu

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2012
Messages
327
Likes
81
Points
45
Mtumbatu

Mtumbatu

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2012
327 81 45

Kamati Kuu inaipongeza Tume ya Mabadiliko ya
Katiba nchini kwa kazi nzuri na kukamilisha kazi kwa wakati.

Kamati Kuu imepokea rasimu hiyo na kuelekeza
kuwa;
Kwa kuwa rasimu hii ni ya kwanza ambayo
inapelekwa kujadiliwa tena kwa wananchi kupitia mabaraza mbalimbali ya katiba
baada ya kuisha kwa hatua ya kutoa maoni.

Kamati Kuu imekiagiza Chama kijipange
kuijadili rasimu hiyo ndani ya Chama kama baraza la kitaasisi la katiba na
kuwataka wanachama na wapenzi wa CCM wajitokeze kwa wingi na kushiriki kwenye
mabaraza haya.

Ushiriki huu wa CCM baada ya kupokea rasimu
umekusudia kushirikisha wanachama wetu kwenye ngazi ya tawi, wilaya, mkoa na
Taifa.

Lakini pia Jumuiya za CCM zimekusudia kushiriki
kama mabaraza ya Katiba na hivyo kuongeza ushiriki wa wanachama na wapenzi wa
CCM katika mchakato huu.

CCM kama baraza la katiba la kitaasisi
litaipitia rasimu iliyowasilishwa kifungu kwa kifungu na
kwa kuzingatia maoni ya CCM yaliyotolewa
mwanzoni kabisa mwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba, wanachama wetu
watashiriki kutoa maoni yao.

Pamoja na kazi nzuri ya Tume ya Mabadiliko ya
katiba, Kamati Kuu inaiomba Tume hiyo kueleza vizuri mchakato mzima kutoka
rasimu ya kwanza mpaka rasimu ya mwisho ili kuondoa mkanganyiko kwa wananchi
juu ya mchakato mzima hasa baada ya rasimu ya kwanza kutoka.

Kamati Kuu inawasihi Watanzania kushiriki tena
kwenye kutoa maoni kupitia mabaraza ya katiba kwa rasimu ya kwanza, bunge
Maalum la katiba kwa rasimu ya pili na kupitia kura ya maoni kwa rasimu ya
tatu, kwa amani,utulivu na kuvumiliana ili mwisho wa siku tupate Katiba nzuri
ya nchi yetu kwa masilahi ya Watanzania walio wengi.
 
B

Bocho

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2013
Messages
1,489
Likes
3
Points
135
B

Bocho

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2013
1,489 3 135
Acha tusubiri tuone hayo maoni ya CCM kupitia mabaraza ya katiba.
 
F

Fitinamwiko

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2012
Messages
4,807
Likes
258
Points
180
F

Fitinamwiko

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2012
4,807 258 180
Tumwamini nani Nape au Kinana?
 
Gefu

Gefu

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Messages
6,952
Likes
273
Points
180
Gefu

Gefu

JF-Expert Member
Joined Nov 30, 2010
6,952 273 180
...wanabahati sana wamesoma upepo unaendaje wakaficha makucha yao,tunawasubiri kwenye mabaraza,wakichakachua tu tunao....
 
DALLAI LAMA

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2012
Messages
8,614
Likes
409
Points
180
Age
37
DALLAI LAMA

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2012
8,614 409 180
Sasa mbona Nape na Kinana walikuwa wanatoka mapovu?
 
Radhia Sweety

Radhia Sweety

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2011
Messages
4,443
Likes
357
Points
180
Age
33
Radhia Sweety

Radhia Sweety

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2011
4,443 357 180
Hawa manyang'au siyo ya kuyaamini kabisa.
 
C

Chikaka Sumuni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2013
Messages
1,339
Likes
5
Points
0
C

Chikaka Sumuni

JF-Expert Member
Joined May 16, 2013
1,339 5 0
Poleni wana CCM hayo yote yatapita tu na TANGANYIKA ndo isharudi tayari. Kumbukeni wosia wa Nyerere msipoangalia ndo yanatimia maana CCM mmetuchezea na kutudanganya kuhusu Kero za Muungano kumbe ilikuw janja ya kula pesa tu.

Haya kazi kwenu sisi yetu macho na masikio,

Kocho

Kocho

Senior Member
Joined
Jun 5, 2013
Messages
120
Likes
1
Points
0
Kocho

Kocho

Senior Member
Joined Jun 5, 2013
120 1 0
mijizi tu imesoma nyakati lkini imegundua hawana pakutokea ila tuwe macho inatafuta nafasi tu wachakchue hasa huko kwenye mabaraza. mpika sumu kaonja mwenyewe mwaka huu hawatoki nyama unusu
 
G

Getstart

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
6,253
Likes
780
Points
280
G

Getstart

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
6,253 780 280
Taarifa hii inaonyesha kuyokukubaliana na Rasimu. Reading between the lines, it inficates some frustration. Itakuwa vigumu sana Rasimu hii kubadilika sana na hasa eneo la muundo wa muungano, huu ndio ukweli ambao nafikiri unawasumbua CCM. Lakini kama wanavyoelekeza tuna nafasi ya kutoa maoni ya kuiboresha ingawa mfumo unaotumika wa mabaraza si mzuri sana. Unawanyima wengine kupata nafasi ya kusikilizwa walionyiomwa kuingia kwenye mabaraza haya na hawako kwenye makundi yanayosemwa. Tume ikubali kupokea maoni ya watu wote wanaoweza kuiandikia au hata kuzungumza nayo.
 
MwanaDiwani

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Messages
5,536
Likes
15
Points
135
MwanaDiwani

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2013
5,536 15 135
mijizi tu imesoma nyakati lkini imegundua hawana pakutokea ila tuwe macho inatafuta nafasi tu wachakchue hasa huko kwenye mabaraza. mpika sumu kaonja mwenyewe mwaka huu hawatoki nyama unusu
Huo ujumbe ungeulekeza kwa CHADEMA ambayo ilisema hivi,
Mheshimiwa Spika,
kushindwa kwa Serikali kuleta Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ili kufanya marekebisho katika maeneo tajwa ni ushahidi wa wazi kwamba Serikali ya CCM haina nia ya dhati na dhamira safi ya kuhakikisha Tanzania inapata Katiba Mpya inayoistahili.

Aidha, si nia ya CHADEMA kuendelea kushiriki na kubariki mchakato huu kama ulivyo sasa kwani ishara zote ziko wazi kuwa Katiba inayokusudiwa ni ile tu itakayokidhi matakwa ya Wana- CCM na Washirika wake na hivyo kutokutimiza azma ya kuwa na Katiba itakayoponya majeraha mbalimbali na kurejesha uzalendo, mshikamano na upendo wa dhati miongoni mwa Watanzania na kisha mfumo wa Utawala utakaokidhi mahitaji ya wakati.

Kwa sababu hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA inatangaza rasmi kwamba: CHADEMA itajitoa ushiriki wake katika mchakato wa Katiba Mpya endapo mambo yafuatayo hayatapatiwa ufumbuzi hadi kufikia mwisho wa mwezi huu, yaani tarehe 30 Aprili, 2013:
Leo tarehe 11/06/2013 hakuna kilichobadilika na serikali haikuleta chochote lakini tayari kwa sasa CHADEMA wamedandia meli ya rasimu ya katiba na kujifanya wamesahau kile walichokitaka kutoka serikalini.
 
KASHOROBANA

KASHOROBANA

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2011
Messages
3,247
Likes
408
Points
180
KASHOROBANA

KASHOROBANA

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2011
3,247 408 180
...wanabahati sana wamesoma upepo unaendaje wakaficha makucha yao,tunawasubiri kwenye mabaraza,wakichakachua tu tunao....
SWADAKTA BABA TUKO MAKINI SANA TENA STANDBY... WALETE TU UMAGAMBA WAO WATASALIMU AMRi
 
KASHOROBANA

KASHOROBANA

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2011
Messages
3,247
Likes
408
Points
180
KASHOROBANA

KASHOROBANA

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2011
3,247 408 180
Huo ujumbe ungeulekeza kwa CHADEMA ambayo ilisema hivi,

Leo tarehe 11/06/2013 hakuna kilichobadilika na serikali haikuleta chochote lakini tayari kwa sasa CHADEMA wamedandia meli ya rasimu ya katiba na kujifanya wamesahau kile walichokitaka kutoka serikalini.
AH AH AH KAJIFUNZE TENA USHABIKi MANDAZI... IVI BILA MKWALA ULE WA CHADEMA UNGEPATA RASIMU NZURI KIAS IKI???
KUMBUKA KITENDO CHA MAGAMBA THRU VIJIMEMO VYA MIGIRO. NNAPE NA NCHEMBA KWENDA TUME VILIVOLENGA KUCHAKACHUA KAM VIMEMO VLIVO KUWA VIKISEMA...
AH AH AH NA BADO CCM TEGENI TU KALIO MPAKA DAWA IINGIE. KIKAO IKI CHA NINI KM C KUWEWESEKA????
 
F

Fitinamwiko

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2012
Messages
4,807
Likes
258
Points
180
F

Fitinamwiko

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2012
4,807 258 180
Mwamini bosi wao JMK ambaye ni mwenyekiti.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
JMK haikuwa chaguo la swali langu. Ukwenda shule nini?
 
B

Bob G

JF Bronze Member
Joined
Oct 5, 2011
Messages
2,354
Likes
12
Points
135
B

Bob G

JF Bronze Member
Joined Oct 5, 2011
2,354 12 135

Kamati Kuu inaipongeza Tume ya Mabadiliko ya
Katiba nchini kwa kazi nzuri na kukamilisha kazi kwa wakati.

Kamati Kuu imepokea rasimu hiyo na kuelekeza
kuwa;
Kwa kuwa rasimu hii ni ya kwanza ambayo
inapelekwa kujadiliwa tena kwa wananchi kupitia mabaraza mbalimbali ya katiba
baada ya kuisha kwa hatua ya kutoa maoni.

Kamati Kuu imekiagiza Chama kijipange
kuijadili rasimu hiyo ndani ya Chama kama baraza la kitaasisi la katiba na
kuwataka wanachama na wapenzi wa CCM wajitokeze kwa wingi na kushiriki kwenye
mabaraza haya.

Ushiriki huu wa CCM baada ya kupokea rasimu
umekusudia kushirikisha wanachama wetu kwenye ngazi ya tawi, wilaya, mkoa na
Taifa.

Lakini pia Jumuiya za CCM zimekusudia kushiriki
kama mabaraza ya Katiba na hivyo kuongeza ushiriki wa wanachama na wapenzi wa
CCM katika mchakato huu.

CCM kama baraza la katiba la kitaasisi
litaipitia rasimu iliyowasilishwa kifungu kwa kifungu na
kwa kuzingatia maoni ya CCM yaliyotolewa
mwanzoni kabisa mwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba, wanachama wetu
watashiriki kutoa maoni yao.

Pamoja na kazi nzuri ya Tume ya Mabadiliko ya
katiba, Kamati Kuu inaiomba Tume hiyo kueleza vizuri mchakato mzima kutoka
rasimu ya kwanza mpaka rasimu ya mwisho ili kuondoa mkanganyiko kwa wananchi
juu ya mchakato mzima hasa baada ya rasimu ya kwanza kutoka.

Kamati Kuu inawasihi Watanzania kushiriki tena
kwenye kutoa maoni kupitia mabaraza ya katiba kwa rasimu ya kwanza, bunge
Maalum la katiba kwa rasimu ya pili na kupitia kura ya maoni kwa rasimu ya
tatu, kwa amani,utulivu na kuvumiliana ili mwisho wa siku tupate Katiba nzuri
ya nchi yetu kwa masilahi ya Watanzania walio wengi.
Ni taabu sana kuiamini ccm HAIAMINIKI na Haitakiwi kuaminika.
 
Forum statistics

Threads 1,273,551
Members 490,428
Posts 30,484,754