Kamati Kuu ya CCM pamoja na Sekretarieti yake ya vunjwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati Kuu ya CCM pamoja na Sekretarieti yake ya vunjwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Vumbi, Apr 10, 2011.

 1. V

  Vumbi Senior Member

  #1
  Apr 10, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amevunja Kamati Kuu pamoja na sekretarieti ya chama hicho inayoongozwa na Katibu Mkuu, Yusuf Makamba.

  Hatua hiyo imechukuliwa usiku huu na Mwenyekiti wa chama hicho,Rais Jakaya Kikwete kutokana na hali ya chama hicho kuwa mbaya katika swala zima la utendaji.

  Hali bado ni tete mjini Dodoma ambako ndiko kunakoendelea kufanyika vikao vya chama hicho vilivyotanguliw a na sekretarieti na baadae Kamati Kuu.

  Uamuzi huo mzito uliotolewa na Mwenyekiti wa chama hicho,Rais Jakaya Kikwete usiku huu kutokana na kufanyika kwa mambo ambayo hayakinufaishi chama zaidi zaidi yanakididimiza chama.

  Hivyo ili kuhakikisha chama kinatakiwa kusimama imara na kuwa na watendaji wazuri katika chama hicho,imebidi Mwenyekiti wa chama achukue uamuzi huo ili kuhakikisha mambo yanakwenda kama yanavyostahiki kwenda.

  Alipotafutwa Katibu Mkuu wa chama hicho,Yussuf Makamba hakutaka kuzungumzia lolote zaidi ya kusema kwamba "Huu ni wakati wa kulala na si wa kuzungumzia swala lolote".

  Hivyo Globu ya Jamii inaendelea kutega sikio lake huko Dodoma na itaendelea kukujuza kila kitakachokuwa kinajiri toka mkoani humo.

  Source: Issa Michuzi Blog
   
 2. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duh, ulikuwa wapi mkuu? Hii taarifa imejadiliwa hapa hadi imepauka
   
 3. V

  Vumbi Senior Member

  #3
  Apr 10, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mkuu nilipo ndio saa 12 asubuhi ndio tuna amka ncha ya kaskazini ya dunia, hivyo ndio tunaaza kupitia habari za nyumbani. Nilijaribu kuitafuta hapa JF sikuweza kuiona nikaamua kuangalia kwenye mitandao mingine, nadhani TZ inaweza kuwa 11:58 am kama sikosei. Anyway kupata taarifa hakuwezi kukuathiri kwa vyovyote.

   
 4. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
 5. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  nabado dawa wa wezi wakula dhambi zitawatafuna mpaka kweye familia zao
   
Loading...