Kamati Kuu ya CCM Dodoma pamoja na Kamati ya Maadili na Usalama ya Chama hili la Handeni Vijijini litazamwe

NDULUMESO

JF-Expert Member
Nov 21, 2013
243
177
Kabla ya yote napenda kutumia fursa hii kwa kumshukuru Mungu muweza wa yote.

Pili naomba ni declare interest kwamba Mimi sio mgombea Wala mpambe wa mgombea yoyote yule katika mchakato wa kula za maoni uliofanyika hapo Jana na kumalizika majira ya saa 5 usiku.

Nije moja kwa moja kwenye hoja.

Kiukweli uchaguzi huo uligubikwa na utata kuanzia hatua ya awali ya upangaji wa majina ya wagombea kwenye karatasi za upigaji wa kula utaratibu ambao ndio pia ulitumika kuwaita wagombea kujinadi kwakuwa wagombea walipangwa kutokana na interest za katibu na watu wake wa karibu waliopanga udharimu huo.

Hatua hii ya upangaji imesababisha wagombea waliokuwa mwishoni kutopewa umakini kwani kikao chenyewe Cha kujinadi kilicheleweshwa kwa makisudi na kilianza saa 7 mchana huku wajumbe wakiwa hawajala.

Achilia hili pia kulikuwepo na malalamiko ya baadhi ya wagombea kujua namba zao za kura kabla ya wagombea wote kupewa namba na pia wajumbe kuonekana dhahiri dhahiri wakipigia kampeni mtu Fulani kitendo ambacho kinaonesha wameingia na mgombea wao.

Baada ya zoezi zima la kupiga kura kukamilika ndipo likaja zoezi la kuhesabu kura ambalo nalo liligubikwa na utata kutokana na uwazi uliosemwa na Mwenyekiti wa Chama kutokuwepo kwani Kamati ile ile iliyokuwa na mgombea wake mfukoni ndio ilitumika kuwapa wagombea kura zao kutoka kwenye masanduku ya kura bila wagombea kujiridhisha Kama kura anayopewa mgombea ni yake au si yake hivyo kutengeneza mwanya wa kutoa kugawa kura za wagombea wengine kwa mgombea wao.

Aidha waandishi wa habari kutolewa nje kipindi Cha kuhesabu kura. Mwisho ni jumla ya kura za wajumbe kuzidi idadi ya wajumbe wote waliopiga kura hivyo kuonekana Kuna kura ziliongezwa na pia kura za wagombea kutokufanana na idadi ya wajumbe waliopiga kura.

USHAURI
Kamati zinazohusika kufuatilia suala hili kwa kina kubaini ujanja huo ikiwemo kuhesabiwa upya kura hizo kwani Kuna harufu ya kutengenezwa mgombea ambae hakuungwa mkono na wanachama.

Katibu wa Chama kuwa na muda mrefu eneo hili kwa zaidi ya miaka 20 kitendo kinachofanya analotaka kuwa liwe,hivyo aangaliwe kwa jicho la kina

Zipo shahidi mbalimbali za rushwa za waziwazi zilizofanyika siku ya upigaji kura hivyo hili pia lifuatiliwe.

Naomba kuwasilisha malalamiko haya ya wajumbe na baadhi ya wagombea waliominywa kwenye uchaguzi huu na lisiofanyiwa kazi litaleta mpasuko kwenye Chama chetu.
 
Mfano wa malalamiko ya wagombea

 
Taarifa ni nzuri ila subiria kikao cha ngazi ya juu ya chama.
Yeah ni Kama kuwapa angalizo japokuwa najua nao walikuwa na macho yao hivyo hata majina sikutaja kuwapa fursa ya kutumia weledi wao kushughulikia malalamiko ambayo yameanza mapema kujitokeza.
 
Back
Top Bottom