Abdull Kazi
JF-Expert Member
- Dec 29, 2012
- 336
- 295
Baada ya ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG),kutoa taarifa ya ukaguzi wa vyama vilivyowasilisha mahesabu na kuipa hati yenye shaka chama cha ACT Wazalendo,leo hii kamati kuu ya Chama hicho inayokutana katika mkoa wa Kichama Kahama imekutana na maofisa wa ofisi ya CAG kutoka makao makuu kwa ajili ya kupokea taarifa zilizosababisha upungufu huo kwa ajili ya kufanyia kazi.
Akizungumza mbele ya wajumbe wa kamati kuu ya ACT Wazalendo mwakilishi wa CAG,Benjamini Majura, amesema chama hicho kimekuwa chama cha kwanza nchini kukutana na ofisi ya CAG kwa ajili ya kupata ufafanuzi juu ya sehemu waliyokosea
Majura alisema kimsingi chama hicho kimekuwa cha mfano tofauti na vyama vingine ambavyo hata uwasilishaji wa taarifa zao tu zinakuwa ni za mashaka kabla ya kukaguliwa.
"Kimsingi ninyi mmefanya jambo la msingi hesabu zenu zimeenda sawa kwa sehemu kubwa ila baadhi ya maeneo ndiyo mkaguzi wetu alitilia shaka na hii inawezekana kuwa imechangiwa na kuchelewa kuchukua uamuzi juu ya matumizi au usahaulifu wa nyaraka"alisema Majura