ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 605
- 1,536
Kamati Kuu ya ACT Wazalendo inafanya kikao leo 02 Agosti 2020. Kikao hichi ni maandalizi ya Mkutano Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 05 Agosti 2020.
Kikao kinafanyika Lamada Hoteli jijini Dar-es-salaam.
Pamoja na mambo mengine. Kamati Kuu leo inategemea kupendekeza majina ya wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar na kupitisha Rasimu za Ilani ya Uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Uchaguzi wa Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Chama, Ndugu Ado Shaibu, akitafakari jambo na baadhi ya wajumbe kabla ya kuanza kikao.
Naibu Katibu wa Idara ya Habari, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma ndugu, Janeth Rithe akizungumza na waandishi wa habari mapema leo kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya chama.
Taswira mbalimbali za wajumbe wa Kamati Kuu wakijadiliana kabla ya kuanza Kikao chao.
#KaziNaBata #TheFutureIsPurple