Kamati Kuu CHADEMA yawavua Uanachama Madiwani 5 walioingia muafaka Arusha

Maamuzi kama haya huchukuliwa na administrators mahala pa kazi au kwenye ofisi za umma, kwa kifupi ni maamuzi ya kiserikali zaidi kuliko chama cha siasa.
Unaweza kutwambia kwa nini? na utupe mfano kusherehesha maelezo yako..
 
Kweli pesa sio nzuri yaani huyu jamaa ameshasahau yaliyotokea siku ya uchaguzi batili wa meya wa Arusha................

MT1tGFsg1jAAAAAElFTkSuQmCC
 
Kakalende,
Labda nikukumbushe tu kwamba kanuni hii sii ya chama CCM bali vyama vyote duniani na kama diwani haelewi hilo basi huyu hakuwa mwanasiasa toka mwanzo kwa sababu huwezi kushinda kisha ukaafiki kutekeleza sera na Ilani za mwenzako..

Inasema hivi:-
MASHARTI YA UONGOZI KATIKA SERIKALI​
1. "Kila mwanachama wa CCM anayegombea na hatimaye kuchaguliwa kushika nafasi yoyote ya uongozi katika Serikali, anapashwa kukiri kwa dhati kwamba maendeleo halisi ya wananchi yanayosimamiwa na Serikali ya CCM katika kipindi kinachohusika, yatapatikana kwa njia ya utekelezaji uliokamilika wa ILANI za CCM za uchaguzi. Kwa hiyo wajibu wake wa kwanza ni kusimamia utekelezaji wa ILANI hizo katika eneo lake.."

Nikukumbushe pia hiyo CDM CC, wananchi wa Arusha pamoja na wanachama wa CDM wametoka wapi - Bofya hapa
 
CDM inavyozidi kuimarika, kuna watu very influential, ndani na nje ya chama wanajawa hofu.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
kudadadeki yametimia
yakaisari mpe kaisari
sasa niwakati wa kudai tume huru ya uchaguzi(igunga na arusha) hapa ndo pakuanzia.
 
Naomba niulize,yule diwani rasta wa cdm arusha ni miongoni mwa waliofukuzwa?
 
Huu haukuwa uamuzi mgumu hata kidogo; uamuzi mgumu ungekuwa ni kuendelea kuwa na mpasuko wa chama kule na kuuacha uendelee. Hata kwa upande wa CCM uamuzi mgumu hauko kwenye kuwatimua mafisadi ndani yake ila uko katika kuwaacha waendelee kuwemo ndani ya chama kwani hilo kwa kweli lataka ujasiri wa aina yake. Utaona kuwa huu ulikuwa ni uamuzi sahihi uliochelewa sana, next time baadhi ya vitu kama hivi vishughulikiwa withini few weeks (kama hakuna factual complications) na uamuzi utolewe swiftly, precisely and boldly.

Vinginevyo itakuwa kama viongozi fulani ambao hawaachi kuwaonya viongozi wabovu miaka nenda miaka rudi. Angalia ripoti ya CAG uone jinsi gani uzembe na kutokuwajibika kunavyovumiliwa.
 
Big Up CDM. Haiwezekani CDM ikubali kufuata barabara walikopita hao magamba ambao wanaelekea kaburini sababu ya migogoro ya aina hiyo.
Hao madiwani watakuwa waliahidiwa makubwa kutoka kwa magamba na sasa imekula kwao. CDM chama makini kinaongozwa na kitaendelea kuongozwa na watu makini.
 
Huyu malah ndiyo naona kadandia gari kwa mbele .yetu macho ni ukweli usiopingika kuwa wananchi tunazidi kukhpenda chama cdm hoyeee mpaka kieleweke wanataka kuambukiza magamba huku tuwatimue
 
Chadema hatuogopi kufanya maamuz magumu na sahih, naipongeza kamati kuu kwani maamuz haya tulitegemea yatoke mapema kabisa ila busara za chama ndizo zilichelewasha; niwahakikishie wana chadema na wana JF wote kuwa kata zote zitaendelea kuwa mikononi mwetu!
 
Maamuzi kama haya huchukuliwa na administrators mahala pa kazi au kwenye ofisi za umma, kwa kifupi ni maamuzi ya kiserikali zaidi kuliko chama cha siasa.

Chama cha siasa ambacho hakina uwezo wa kuchukua maamuzi kama mahali pa kazi na ofisi za umma (which I'll argue chama cha siasa kina qualify on both counts) basi hakistahili kuwa chama cha siasa. Chama cha siasa si mkusanyiko wa watu wanaozungumza, kubishana, kubezana na kusumbuaana bila mtu kuwa na uwezo wa kuleta order ndani ya chama. Kitakuwa ni chama dhaifu sana kikiwa hivyo. Kuna wakati wa kuzungumza na kuna wakati wa kunyamaza. Katika hili la mgogoro wa madiwani limekwisha.

Hao madiwani wakitaka wanaweza kwenda na kulalamika na kuita CDM majina yote na vyovyote vile lakini ni matumaini yangu uongozi wa CDM baada ya kuwafahamisha fate yao hawatakuwa na muda wa kuanza kubishana nao. This is a closed deal, sasa ni kuanza kupanga tu wagombea wengine ili kuvichukua hivyo vitu na hivyo kuwaonesha watu kuwa uamuzi ule ulikuwa unaungwa mkono na wanachama wengi wa Arusha.
 
Back
Top Bottom