Kamati Kuu CHADEMA yawavua Uanachama Madiwani 2 Jiji la Mwanza

Alijua kuwa amefanya faulo na maccm, ndiyo maana akajidai hatagombea umeya. Ishu siyo kugombea umeya ishu ni kufuata taratibu,Huyu ni muhujumu tu ni kama sita!!!!!
 
Tatizo lako nini? Kama ameenda kinyume na kanuni za chama inabidi awajibishwe.swala kuwa naye udsm hicho ni kitu kingine.


uko sahihi,
Utakatifu wa jana hausafishi dhambi ya Leo. Kama Udsm alikuwa mzuri leo kavunja kanuni za Chadema. Uzuri wa Udsm utakusaidiaje kutokuadhibiwa leo?
 
Matata ni diwani wa kitangiri ni Muislam, kwa kukusaidia ni kaka yake na Farida Matata.

Si mmewakaribisha Kafu??
Wachukueni watawasaidia.

Wakati nyie mnaongea kuvua magamba huku mkilea wakina chenge, lowassa na the rest of them crooks, sisi tunaondoa maguhu mapema kabisa.

Nendeni mkawape hela ya kukata rufaa ili hizo kata zibaki wazi mpaka 2015. That is how you solve issues.

Tabia za kenge kutaga na kula mayai ya wenzake.

Hatuvumilii upuuzi. Ccm imetufikisha hapa kwa upuuzi wao na udhaifu wa huyu mpenda misiba.
 
Kamati kuu iwe inatafakari consequences kabla ya kuchukua hatua, anyway nawapongeza kwa kuchukua maamuzi magumu
 
Sasa what next ni kwamba hawa wanakoma kuwa madiwani halafu chaguzi ndogo zinaitishwa? au wanaendelea na udiwani hadi mwisho wa term?
 
Last week alikuwa EATV alionekana yuko very composed na alisema hatagombea umeya kwa sababu lengo lake ni kukijenga chama. Mara anafutwa uanachama...duh, kweli kuishi kwingi kuona mengi!

Hakuwa EATV bali alikuwa Star Tv Tuongee asubuhi.
Siasa zina gharama yake na pia kuna kanuni zake kama huwezi kuzifuata then utaishia kuwajibishwa kama hutaki kuwajibika.
 
Matata ni diwani wa kitangiri ni Muislam, kwa kukusaidia ni kaka yake na Farida Matata.
Ritz uko sahihi,
Wajumbe wa kamati kuu ya Chadema wote na maaskofu na wachungaji. Hakuna mwislamu hata mmoja mle ndani. Kwa hiyo, hawa jamaa wote 2 ni waislamu ndo maana wametimuliwa. Akina saidi Arfi, Zitto, Mohamedi Mzee, Hamadi, Prof Abadallah Safri sijui waliondolewa lini.
Pili, hakuna diwani mwislamu mwanza wala wala mahali pengine nchini kwa sababu nao wangeondolewa kwa kigezo cha dini. Ritz, hapa tuko pamoja nadhani. Propaganda nyingine huwa hazilipi mkuu.
 
Wamechemka! Wangetoa ONYO KALI. May be Mwanza hupajui? Wanamwanza hawana dogo!
Mkuu,
Kanuni za Chadema yapo makosa ya kupewa onyo na yako makosa ya kutimuliwa mmoja kwa mmoja. Usiwe na hofu na uwezo wa kisheria wa akina Prof. Abdallah Safari, Lissu na Marando
.
 
sababu chagulani sio mchagga ndio maana
Mwenzio Ritz anasema sababu ya dini, wewe unasema sababu siyo mchaga. Kule Arusha mbona kuna mchaga alikuwepo kati ya waliotimuliwa. Au walikosea mkuu.
Pili, unataka kusema wale madiwani wote walikobaki ni wachaga siyo. Au!!

 
Hapa bado kabisaa chama kichanga, full migogoro. Kikikua kitakuwaje????

tafsiri ya migogoro kwako nini hasa? magamba uamuzi kama huu hamjakomaa bado na hamuuwezi kamwe siasa za kubembelezana na kupeana na kufuga ubovv hazina nafasi ndani ya chama makini! M4C DAIMA MAPAFU YA MBWA FATA UTOE ULIMI NJE
 
Huyo Meya si imeonekana alishindwa kazi? Yaani CHADEMA nao mtu akiwa mwiba kwa viongozi walioshindwa kazi anafutwa uanachama!!!

Mkuu,
Meya kushindwa ni jambo moja, na Chagulani na Henry kuvunja katiba na kanuni za Chama ni jambo jingine. Huwezi kusema mimi nisifungwe jela kwa kosa la kuua kwa sababu wewe uliyemwua ni mwizi. Haviendi namna hiyo.
 
ni muislam aliingiaje huku????????????????

nilisha kuona kuwa umelewa dini toka post ya kwanza, ona sasa unavyojinyea hovyo na kujikojolea barabarani watoto wanakuzomea, aibu kwa kizazi kijacho kuwa bb kasababisha hata usoni hatuonani sabab ya ulevi wa dini. Kama huwezi nunua udini kaa nyumbani kwako kisha kunywa mpaka uzimie sio hapa jf.
 
Kamati kuu imechemka, ilipaswa iwape ONYO then mengine ndio yafuatwe! ADAMU CHAGULANI NI KIONGOZI MWENYE UDHUBUTU, VERY INFLUENCIAL! CDM JIPANGENI!

thibitisha kuwa hawakupewa right to be heard. Mkuu kumbuka cdm haiwezi kukurupuka tu
 
Sasa ulitegemea nini, na huyo Adam Ibrahim.

naona bado mnalewa pombe ya udini na kujinyea hovyo barabarani nami siwaonei aibu nawachora tu na kuwasema tu kuwa mmejinyea acha pombe mbaya.
 
Ndio maana nawaambia vijana kila siku ukombozi mnaouzungumza mdomoni hautoshi, ingieni field muone kazi ilivyo ngumu. Sasa huyu Chagulani pamoja na jitihada zake za kuijengea CHADEMA imani kwa wanamwanza ambao wameshakuwa disappoited na CHADEMA anaishia kufutwa uanachama!!!

Kaka yangu ZeMarcopolo hayo ndio maamuzi magumu haijalishi umefanya nini lakini pale unapokosea lazima uwajibishwe nafikiri Viongozi wa CDM lazima walikuwa wameshampa maonyo hapo awali lasivyo watakuwa hawajamtendea haki
 
Moja ya mambo yaliyokichaza CCM kama chuma kilichopiga kutu ni 'kutofanya maamuzi' pale mtu anapokwenda kinyume na taratibu/kanuni za chama kama institution. Kwa miezi kadhaa Nape alikuwa anazunguka nchini kutangaza kuwa kuna watu ndani ya CCM wanatakiwa waondoke, na akasema wamepewa siku 90. Ningetaka kuamini kuwa chama (CCM) ndicho kiligharamia matembezi hayo ya Nape. Nini kimefanyika baada ya siku 90 kuisha?

China wamemtosa kigogo mmoja - tena kigogo wa kukata na shoka baada ya mke wa kigogo huyo kukumbwa na kashfa ya kumuuwa mfanyibishara wa Uingereza. CCM ambao wamekuwa wananyweshwa juice na hiki chama cha kikomunisti cha China wanazunguka nchi nzima kutoa siku 90 kwa watu kuondoka, muda unapita na ghafla topic inabidilika! Matekeo yake chama kinaonekana kama kikundi cha mzaha.

CHADEMA cannot afford to kufuata mtindo wa CCM wa kucheza ping-pong na maadili ya uongozi.
 
Back
Top Bottom