Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,445
- 7,810
Baadhi ya wajumbe walimtaka Lowassa aombe radhi hadharani kutokana na tukio hilo(Kwenda Ikulu) lakini busara ilitumika kwa kutaka jambo hilo liishe kwa Lowassa kutoa taarifa hadharani.
Raia Mwema liliambiwa pia kwamba wajumbe wa kikao hicho walielezwa kuwa Lowassa kwa sasa amekumbwa na changamoto kadhaa katika maisha yake binafsi na si busara kumuongezea mambo mengine mazito.
Miongoni mwa changamoto za Lowassa ambazo zimetajwa kwenye kikao cha kamati kuu ni pamoja na suala la familia yake(Mtoto wake kuhamishwa benki kuu na mkwewe kuwa mahabusu).
"Kamati kuu imemkubalia Lowassa abaki ndani ya chama hicho kutokana na kwamba kama ni changamoto hata mwenyekiti wetu pia amekumbana nazo na bado anakabiliana nazo.
Lakini pia chama kimeonya wale wote waliotoa matamko baada ya uamuzi ule wa Lowassa". Alisema ofisa mmoja wa CHADEMA kwa sharti la kutotajwa jina.
Mbali na makubaliano hayo, kamati kuu pia ilitoa karipio kwa viongozi wake ambao walionekana kumsema Lowassa hadharani mara baada ya kutokea kwa tukio hilo na kuwakumbusha kuwa chama kina wasemaji wake rasmi ambao ni mwenyekiti, katibu mkuu na msemaji wa chama(Makao Makuu).
Mara baada ya taarifa za mkutano huo wa Lowassa na DK. Magufuli kuwekwa hadharani, baadhi ya vigogo wa chama hicho walitumia mitandao ya kijamii kumshutumu mbunge huyo wa zamani wa Monduli.