Kamati kuu CHADEMA, Mbowe, Slaa na Zitto mpo CHADEMA kwa masilahi ya nani?

Status
Not open for further replies.

Mghaka

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
320
126
Wanachadema katika mtafaruku huu wa kichama mpo upande gani na kwa maslahi yapi? Mimi nawakilisha kundi kubwa la Watanzania ambao wanaamini suluhu peke ya maendeleo ya watanzania ni uwepo wa vyama pinzani vya kisiasa na taasisi binafsi zenye utengamano, nguvu na imara. Chadema katika hili mnatusaliti watanzania na mwenendo wenu sasa hivi ni chukizo kwa wapenzi wa mfumo imara wa uwajibikaji ambao watch dog ni political parties and strong civil societies.

Wale ambao wanamuenzi Mandela ambae ni kielelezo cha kusameheana kwa gharama ya utulivu, umoja na uponyaji wa makovu yatokanayo na tofauti za kimtizamo katika kulinda masilahi ya makundi ya kisiasa wanasikitishwa na hali ilivyo sasa ndani na nje ya chadema. Kaburi la Mandela bado hata kukauka na kama alama ya kumunzi ebu kaeni tena mtafakari uamuzi wa kamati kuu kwa masilahi ya watanzania. Nawahakikishia kuwa bila kujali unaungwa mkono na nani au unapendwa na nani na kwa masilahi ya nani Zito nje ya Chadema ni simba mzee na chadema bila zito ni ng'ombe ambae amekatwa mkia (fikiria umuhimu wa mkia katika kuhami wadudu wasumbufu kwa ng'ombe). Wanachama ambao kwa sasa wanashabikia mtafaruku huu bila kuchanganua athari za chama ni maadui namba moja wa chama.

Naamini na nakubaliana na Kamati kuu kuwa hakuna demokrasia inayoruhusu kikundi kufanya mashambulizi kwa gharama ya kutafuta ushindi ndani ya taasisi ambayo dira yake ndio wanaitumikia, lakini hili linapokuwa limetokea tusikimbilie kuadhibu bila kutafakari athari za hatua zetu. Tumewavumilia wengi sana, mfano mkubwa ni Shibuda katika ngazi ya viongozi wa kitaifa kama wabunge kwa nini leo isiwe hivo kwa Zito na wengine? Natambua makosa anayofanya Zito kuanza mchakato wa kupita kule ambako Katibu Mkuu wake amepita huu ni ushindani wa kipuuzi na kwa kweli wale wanaompenda Zito na nchi hii na Chadema ambae zito kama namnukuu sawa amesema maisha yake ni sehemu ya CHADEMA na hayatenganishwi, wamshauri na naomba wampatie ujumbe huu. Akili nyingi na uwezo mkubwa wa kuchambua mambo bila kuweka chachu ya busara kidogo ni hatari katika maisha yoyote ya kisiasa.

Mbowe, Dr Slaa na Kamati Kuu Kubalini kushindwa ili Chadema ishinde, Zito na Wenzako kubalini kushindwa ili Watanzania washinde katika kujenga Demokrasia. Milango ya kujenga hoja kwa uvumilivu ndani ya Chadema bado iwazi iko siku watu watawaelewa. Tofauti zenu zimeingia kasoro pale ambapo wote mnaongozwa na ubinafsi zaidi. Naandika haya kutoka rohoni mwangu mimi ni CCM kiitikadi na kifikra na naamini CCM bora itaendelea kuwepo kama vyama pinzani bora na vyenye utulivu vitakuwepo. Kuleta mabadiliko si lazima muende Ikulu, hakuna anaepinga kuwa Katiba mpya ni zao la juhudi zenu hakuna asiyeamini kuwa mnaipatia changamoto serikali ya chama cha mapinduzi, mbona sasa mnalewa sifa mnaanza kuhamishia harakati za uamusho kwa kupambana wenyewe?
 

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,402
7,957
Unapoongelea CHADEMA usimuhusishe Zitto, muua Panya ameishajitanaibaisha kuwa yeye ni CCM. CDM ni taasisi, no individual is bigger than CDM. Zitto ameishafikia mwisho wake kisiasa and its a matter of time Tu tutamsahau kama wenzake akina Lamwai, Tambwe Hiza, Msabaha, Shitambala na mentor wake wa usaliti Warid Kaburu
 

kenwood

JF-Expert Member
Nov 29, 2013
757
97
Ukiamka Chadema ukilala Chadema ukikoroma Chadema. Aaaahhhh!!!
Hivii hamnaga habari nyingine au vyama vingine mkaandika.
Wapi CUF, wazee wa ngangari na matawi yao ya Chechnya, kosovo n.k
Tuwe tunapata habari za Chauma, TPP Maendeleo, UDP, DP??
 

hatari lakini salama

Senior Member
Nov 24, 2013
131
18
Unapoongelea CHADEMA usimuhusishe Zitto, muua Pants ameishajitanaibaisha kuwa yeye ni CCM. CDM ni taasisi, no individual is bigger than CDM. Zitto ameishafikia mwisho wake kisiasa and its a matter of time Tu tutamsahau kama wenzake akina Lamwai, Tambwe Hiza, Msabaha, Shitambala na mentor wake wa usaliti Warid Kaburu[/QUO

moyoni mnajua tu dogo anavyo wapeleka mbio!.
 

Mghaka

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
320
126
Unapoongelea CHADEMA usimuhusishe Zitto, muua Pants ameishajitanaibaisha kuwa yeye ni CCM. CDM ni taasisi, no individual is bigger than CDM. Zitto ameishafikia mwisho wake kisiasa and its a matter of time Tu tutamsahau kama wenzake akina Lamwai, Tambwe Hiza, Msabaha, Shitambala na mentor wake wa usaliti Warid Kaburu[/QUO

moyoni mnajua tu dogo anavyo wapeleka mbio!.

Msifanye kwa sababu historia ya huko nyuma inawapendelea na kwamba imewageuka walioigeuka historia yenyewe. Si kila siku ni Ijumaa, tunapenda sana kuona nidhamu isiyo zao la ukandamizi, pia tunapenda kuona demokrasia isiyo tunda la ukaidi na fujo. Kwa makundi yote tunapenda kuona mnafikia ukomo wenu wa kupata mkitakacho na chama chenu kikibaki kimoja na ndani yake kuna utulivu. Lema amewahi kutuambia kuwa heri simba mia moja porini kuliko nyoka mdogo ndani ya nyumba.Na mimi nawakumbushia kuwa heri simba mia moja ndani nyumba maana wako caged kuliko fisi moja ambaye ni so wild na yu nje ya nyumba. Hao mnao waona wachache kesho wakifukuzwa itabidi waanze kuwa wild na kupunch our leaders and the party in all fronts, badala ya kufanya maendeleo mnaanza kutumia muda mwingi kujibu mashambulizi kwa sababu tu ya maadui mliowatengeneza mwenyewe.
 
Status
Not open for further replies.
1 Reactions
Reply
Top Bottom