Kamati kuu CHADEMA kujadili ukandamizaji wa Bunge na haki ya kupata habari

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Habari wanaJF

Ifuatayo ni taarifa rasmi juu ya kikao cha kamati kuu cha Chama cha Demokrasia na maendeleo kinachofanyika mjini Dodoma. Kikao hicho kinatarajiwa kujadili mambo mazito yahusuyo taifa la Tanzania na mustakabali wa Uhuru wa Bunge na haki ya kupata habari chini ya utawala wa Rais John Pombe Joseph Magufuli.

===================


images


CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vincent Mashinji amesema kuwa kikao cha Kamati Kuu ya Chama kinachofanyika mjini Dodoma, kitajadili pamoja na masuala mengine, kwa uzito mkubwa ukandamizaji wa bunge na uhuru wa habari, unaofanywa na Serikali ya CCM chini ya Rais John Magufuli.

Amesema kuwa utawala wowote ule unaodiriki kuminya uhuru wa maoni hasa kupitia bunge na unaozuia vyombo vya habari kutimiza wajibu wake kwa manufaa ya umma, ni dalili za wazi kuwa utawala huo unapiga hatua kuelekea kukumbatia udikteta ili taifa litukuze mtu au watu badala ya mifumo na taasisi imara kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Kanuni za nchi.

Katibu Mkuu Dkt. Mashinji ameyasema hayo leo mchana alipokutana na kuzungumza na waandishi wa habari kwa ufupi kabla ya kuanza kikao cha siku mbili cha Kamati Kuu ya Chama, akisema kuwa kitajadili kwa kina namna ambavyo demokrasia ya wananchi inawekwa rehani tangu Rais Magufuli apoingia madarakani.

Akiambatana na Manaibu wake, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalim (Zanzibar), Katibu Mkuu Dkt. Mashinji amesema kuwa mwenendo wa Serikali ya CCM chini ya Rais John Magufuli kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya televisheni kuonesha vikao vya bunge huku ikidhibiti vyombo vya habari kutimiza wajibu wake kwa uhuru, ni tishio kubwa kwa demokrasia ya wananchi na mstakabali mwema wa taifa.

“Kudhibiti bunge kufanya kazi zake kwa uhuru, kudhibiti vyombo vya habari kuripoti za bunge na badala yake wanapewa zilizochujwa, kudhibiti uhuru wa maoni kwa ujumla ni njia ya kuelekea kwenye udikteta ambako tunalazimishwa kutukuza mtu mmoja au watu wachache ambao hawataki kukosolewa. Hiyo ni hatari. Kamati Kuu itajadili na kufanya maamuzi ambayo tutayaleta kwa umma,” amesema Katibu Mkuu Dkt. Mashinji.

Kwa upande wake, NKMB John Mnyika amesema kuwa viongozi wa chama ambao ni wajumbe wa Kamati Kuu ambao wako bungeni, wataeleza kwa kina kuhusu madhara ambayo wabunge na wananchi wanayapata kwa Serikali na Bunge kudhibiti vyombo vya habari kutimiza wajibu wake katika kuripoti habari za bunge kwa maslahi ya wananchi.

Aidha, NKMZ Salum Mwalim amesema kuwa suala la mgogoro wa kisiasa unaoendelea Zanzibar pia litajadiliwa kwa kina na kufanyiwa maamuzi, hasa kutokana na taarifa ya hali ya siasa itakayowasilishwa kutokana na kikao cha Kamati Maalum ya Chama Zanzibar.

Kikao hicho cha kikatiba kilichoanza leo chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe, kinatarajiwa kufanyika kwa siku mbili, ambapo kitajadili na kufanya maamuzi kuhusu masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na hali ya siasa nchini, mwenendo wa Serikali ya CCM chini ya Rais Magufuli na uendeshaji wa chama.

Imetolewa leo Alhamisi, Mei 12, 2016 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA.


Waweza kupakuwa kiambatanicho hapa chini.
 

Attachments

  • KM DODOMA.pdf
    179.3 KB · Views: 93
Huwezi kuamini hiki chama jinsi kilivyokuwa na mvuto kipindi cha nyuma. Leo kimeishia kutoa matamko yasiyo na mvuto wala mashiko. Kweli kila chenye mwanzo kina mwisho.
 
Bunge ni shehemu ya kampeni kwa baadhi ya wabunge hivyo kujadiliwa na kamati kuu ni kuona mapungufu ya kampeni yao
 
Samahani jamani naombeni msahada juu ya hili, hivi mfano serikari ina kiuka taratibu pia ina kandamiza wananchi wake sambamba na ku kandamiza demokrasia ni hatua zipi huchukuliwa dhidi yake au kuna utaratibu wowote ambao uko ambao una weza uka chukulia na mataifa ili kuhakikisha serikali husika ina rudi kwenye mstari bila ra kuathiri inchi hiyo chin ya serikali yake ni sovereignty??
 
Hivi kwa akili ya kawaida,serikali ya CCM bungeni idadi ya wengi ni CCM.Hamuoni wazi mnapoteza mda tu! Matamko bila dola ni sawa kuupiga ngumi upepo.Kubalini,mmebanwa na hamna jipya tena ukawa.
 
Samahani jamani naombeni msahada juu ya hili, hivi mfano serikari ina kiuka taratibu pia ina kandamiza wananchi wake sambamba na ku kandamiza demokrasia ni hatua zipi huchukuliwa dhidi yake au kuna utaratibu wowote ambao uko ambao una weza uka chukulia na mataifa ili kuhakikisha serikali husika ina rudi kwenye mstari bila ra kuathiri inchi hiyo chin ya serikali yake ni sovereignty??
msaada pekee ni we unayeona unakandamizwa kuhama nchi!! sisi wengine tunaona serikali IPO fresh tu na maisha yanaendelea
 
badala ya kujadili upokwaji wa uhuru wa vyombo vya habari ni bora kwanza na muhimu wakajadili ni namna gani wataondokana na ombwe la uvamizi wa watuhumiwa wa ufisadi kutoka CCM. wao wenyewe walikuwa wakiwatuhumu iweje leo eti wamewasafisha. wakati walikuwa wakidai wana ushahidi wa kutosha usio na doubt.

wajadili pia namna gani mapesa yetu ya michango yameliwa ama kutumika! hatupati mrejesho wowote hasa watu wa mikoani. ukiuliza unaambiwa nenda kaulize kinondoni. utafikaje mtu wa mkoa. ukiuliza matawini katika ofisi za mikoani wanakwambia hawajui na wala hawajawahi sikia kitu kama hicho. wao wenyewe wanatoa pesa zao mifukoni lakini kwa biashara ambayo hailipi wala haina faida yoyote. kama ni ajenda za ufisadi tumeshaziua.
 
Wakuu mbona CHADEMA hawarushi LIVE kikao cha kamati kuu kinachoendelea Dodoma.

Watu tunataka kujua jinsi wanavyochangia humo ndani.

Ni haki yetu kidemokrasia kupata hiyo habari LIVE.
 
Mbona na wewe kikao cha familia yenu hakiko live, mnaficha nini???.KIKAO cha CDM kiko live kwa wahusika wa kikao hicho.
 
Back
Top Bottom