ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,013
- 7,209
Leo CHADEMA imetoa uamuzi wa kuwapa wabunge wake 19 wa viti maalum nafasi ya kuomba msamaha ili waendelee kuwa wanachama.
Katika tamko lao, hawajakaripia wala kujitenga na Mbunge wa Nkasi Kaskazini Aida Khenan.
Hapo awali, CHADEMA ilitoa amri kwa Aida Khenan kutokushiriki Bunge. Hata hivyo, Aida alihudhuria Bunge, akaapishwa sambamba na Wabunge wengine.
Leo, ilikuwa ni fursa kwa CHADEMA kutoa kauli juu ya Ubunge wa Aida iwapo ingekuwa haiutambui. Ukimya wa Kamati Kuu ya CHADEMA, umetuma ujumbe rasmi kuwa CHADEMA imelegeza msimamo wake juu ya Mbunge huyo.
Kwahiyo, mahesabu ya Wabunge ya CHADEMA mpaka sasa ni 20 (mmoja anatambuliwa, 19 wamepewa nafasi ya kuomba msamaha)