Kamati kuu CCM yawazuia Nape na Chiligati kwenda Igunga

Rais Kikwete amewatahadharisha makada wa CCM kuachana na hatua za namna yoyote za kumpuuza au kumshambulia Rostam katika majukwaa ya siasa.

Mbali ya hilo, ili kuhakikisha jimbo hilo linaendelea kubakia mikononi mwa chama hicho, Kamati Kuu iliwazuia makada wake wawili, Nape na John Chiligati, kwenda katika kampeni za chama hicho za kusaka mrithi wa Rostam huko Igunga.

Source: Gazeti la Tanzania Daima la leo.

Intelligensia yao imesoma alama za nyakati kuwa wao ndio walioshinikiza RA kujiuzuru au?? kumbe CCM sasa ndio wameamka na kujua lipi jema na lipi lisilo jema au? Nadhani wananchi wa Igunga wanatakiwa kujifunza neno mabadiriko huja wakati wowote na watakiwa kuwa tayari kuyapokea mabadiriko

Nape kuwa makini sana ...utapelekwa pabaya na JK.. mpaka sasa hivi jimbo la Igunga limeshapotea ..ccm watakuwa wapinzani

Intelligensia yao imesoma alama za nyakati kuwa wao ndio walioshinikiza RA kujiuzuru au?? kumbe CCM sasa ndio wameamka na kujua lipi jema na lipi lisilo jema au? Nadhani wananchi wa Igunga wanatakiwa kujifunza neno mabadiriko huja wakati wowote na watakiwa kuwa tayari kuyapokea mabadiriko
Unajua CCM si kwamba wamefanya kosa kumshinikiza Rostam kujiuzulu la ila roho inawasuta kuwa wamemuonea maana si peke yake aliyesababisha CCM kufika ilipo wapo wengi waliohusika je wamefanywa nini, wanajua yeyote hasa ngazi ya taifa atakayekwenda Igunga ataulizwa ina maana ni mbunge wetu (RA) pekee ndiye aliyesababisha haya?

Lazima wamgwaye si anajua siri zao wote, sasa wanogopa jamaa asije akaropoka mwarabu wa watu! sasa hivi wanambembeleza sana. CCM sera zake zilishapitwa na wakati.

CCM haijazuia viongozi wake kwenda wa kitaifa kwenda huko iSipokuwa watakwenda kwa awamu. Chama kikubwa kama hicho viongozi wote wahamie huko inaingia akilini kweli. Kwanza nape tu ni sawa na viongozi wote wa chadema ndio maana wanafuatana kama nyumbu. Uliona wapi nchi ikapeleka jeshi lote kwa wakati moja. Labda mandamano

Kweli ww ni mbayuwayu,he he he hadi nakuonea aibu,msalimie bwanako!

Naomba niulize swali moja kuu la msingi; Ni kitu gani kinaweza kubadilisha kambi nafasi ya CHADEMA kuwa chama kikuu cha Upinzani?
Nauliza hivi kwa sababu kama kwa mfano ikatokea kwenye chaguzi hizi ndogo kwamba CUF wanashinda (my assumption) hivyo kuwa na wabunge wengi kuzidi CHADEMA je CUF si ita-qualify kuwa chama kikuu cha upinzani?

Ikitokea hivyo, CUF ambayo statistically ina wabunge wengi toka Zanzibar hususan Pemba ina maana watakuwa ndio wasemaji wakuu kwa mambo ya Tanganyika? Tukumbuke hakuna bunge la Tanganyika na wabunge wa Zanzibar kwenye bunge la Muungano wana vote/say kwenye mambo ambayo ni (techinically) exclusive for Tanganyika! e.g Wizara za Ujenzi, afya, uwekezaji, ardhi, uvuvi na ufugaji nk. Sijui kama kuna mtu anaona huu moshi ninaouna kwa mbali ila hebu tufikirie hili kwa makini na objectively.

Wamegundua Vuvuzela la chama likienda huko, RA atasusia kampeni ya kunadi gamba jingine hivyo wananchi watakipa adhabu chama kwa kuwapa wapinzani. Igunga ikichukuliwa na Chadema tu basi hukumu ya vuvuzela Shibuda itakuwa mlangoni!

Nategemea mchuano mkali Igunga, ila nategemea pia muda wa mwisho wa kampeni Bibi harusi C .U. F itajiondoa na kumwachia Bwana harusi. lakini kama cdm itafanya mashambulizi kama yaliyofanywa tarime kipindi kile, haina shaka watachukua jimbo. mgombea hatakua na issue, hatakua na effect sana katika ushindi.

nchi hii ni kijinchi cha ajabu sana hivi kikwete anaona wanaigunga ni wajinga kiasi kama hicho?

Wanavizia kura za MY WIFE wao CUF, ile ndoa waliofunga kwa kutengua kanuni za Bunge kuhusu kambi rasmi ya upinzani Bungeni sasa ndoa yao inamimba ya miezi 9. CUF wanasubiri wajifungue katoto huko IGUNGA.

Nilipitia thread moja juu ya hili "Kumbe alieleta thread alikuwa akisema ukweli juu ya nguvu za CUF kule???"

Rais Kikwete amewatahadharisha makada wa CCM kuachana na hatua za namna yoyote za kumpuuza au kumshambulia Rostam katika majukwaa ya siasa.

Mbali ya hilo, ili kuhakikisha jimbo hilo linaendelea kubakia mikononi mwa chama hicho, Kamati Kuu iliwazuia makada wake wawili, Nape na John Chiligati, kwenda katika kampeni za chama hicho za kusaka mrithi wa Rostam huko Igunga.

Source: Gazeti la Tanzania Daima la leo.

Huo unaitwa ukomavu wa kisiasa! Pengine hili lingeangaliwa sawa na sakata la Mameya wa CDM kule Arusha!

Kwi kwi kwi teh teh teh te ha ha haaa,aaah kamati kuuu' kwahiyo wanamwogopa RA? Nape na Chiligati si mabingwa wa kuonge waacheni waende.HV NDIO HII KAMATI KUU ILIYOPO CHINI YA J K INAYOISHAURI SERIKALI KUPUNGUZA BEI YA MAFUTA YA TAA? Hv Pinda hayupo kamati kuu? Hv Kikwete akifika ikulu ataanza kumshauri rais wa nchi(KIKWETE) KWAMBA KAMATI KUU INAKUSHAURI WEWE MKUU WA SERIKALI(KIKWETE) UPUNGUZE BEI YA MAFUTA YA TAA! Halafu pinda ndiyo atapewa taarifa kumpatia mkulo na Ngereja? Au itakuwaje?

YAANI HIYO NI NGUMU SIJAPATA SIKIA WALA KUONA.

Hello Friend.
How Are You And Also About Your Present Condition Of Health I Know All Is Well With You If So Thanks Be To God Almighty For Making It So.
WELL WITH OUT WASTING OF OUR TIME.. My Name Is Miss mirian, A Young Girl I Am Looking For one who I Will Relate With for love and longterm relationship.
For More Info I will Send You My Photo For You To Know More About Me, Please Do Mail Me On This
email... mirian2love@yahoo.co.uk

Yours
mirian

Umepotea njia, hili jukwaa la siasa sio malavidavi. Mod ondoa hii kitu.

Back
Top Bottom