Kamati Kuu CCM yawaka moto; Taarifa ya Kamati ya maadili yaumiza kichwa wajumbe

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

22 NOVEMBER 2011

*Taarifa ya Kamati ya maadili yaumiza kichwa wajumbe

Na Pendo Mtibuche, Dodoma

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. Jakaya Kikwete, amefungua kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho cha siku mbili huku taarifa ya Kamati ya
Maadili ya cama hicho ikiwaumiza kichwa wajumbe kutoa maamuzi mazito.

Kamati ya Maadili ya CCM inaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara bw. Pius Msekwa na Katibu wake Bw. Abulrahman Kinana, ilielezwa kuwasilisha taarifa ya kazi yao ya kuwahoji watuhumiwa wanaodaiwa kutaka kukivuruga chama hicho na kutoa mapendekezo mazito ya hatu za kinidhamu kwa baadhi ya viongozi hao.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, baadhi ya vigogo waliotakiwa kuchukuliwa hatu ni wamo pia vigogo wa Umoja wa Vijana wa chama hicho UVCCM, Katibu mmoja wa Mkoa, na wengine.

Ilielezwa kuwa Rais Kikwete alionyesha hali ya ukali tofauti na hali yake ya kawaida huku akiwataka wajumbe 31 waliohudhuria Kikao hicho kutoa mawazo yao kwa uwazi na kwa maslahi ya chama hicjo na si kuangalia mtu.

"Mtihani mzito kwetu ni taarifa ya Kamati ya Maadili, kusema kweli imetuweka njia panda maana ni lazima tutoe maamuzi, mpaka sasa bado mbichi kabisa ila kila kitu kitaeleweka,"kilisema chanzo chetu ndani ya CCM.

Awali akifungua mkutamno huo Rais Kikwete alitumia maneno mafupi ya "kikao kimefunguliwa," kisha kuwaruhusu wajumbe kuanza kazi ya kujadili agenda.

Akitoa taarifa ya utangulizi kwa Rais Kikwete muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao hicho Katibu Mkuu wa CCM Bw. Wilson Mukama, alisema kikao hicho hutakiwa kuwa na wajumbe 38 na kwamba saba wametoa udhuru wa kutohudhuria hivyo kubaki 31.

Awali Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi Bw. Nape Nnauye, akizungumzia dhana ya kujivua gamba ndani ya chama hicho alisema hilo ni sehemu ya mageuzi 26 ndani ya chama chao.

"Ndugu wanahabari nimekuwa nikizungumza na ninyi mara nyingi juu ya mambo mbalimbali ya kukiimarisha chama chetu, niliwahi kuwaeleza kuwa mtu unapotaka kuoga lazima uanzie kichani ndipo ushuke sehemu zingine huwezi kuanza kuoga mwili mzima hivyo hivyo ndani ya chama yapo mambo mengi tuyayoyafanyia kazi si jambo moja tu la kujivua gamaba,"alisema.

Alisisitiza umuhimu wa uadilifu ndani ya chama hicho na kuweka wazi kuwa viongozi wanapaswa kuwa na sifa njema ili waweze kuwatumikia wananchi waliowachagua na kuwaweka madarakani na kwamba mtu akienda kinyume na maadili hatavumiliwa kwa manufaa ya chama na taifa kwa ujumla.

Baada ya Kamati Kuu kumaliza kikao chake leo, kesho ndio kindumbwendumbwe cha Halmashauri Kuu (NEC) kitaanza kikao chake ambacho ndicho kitaridhia maamuzi yote ya Kamati Kuu. Siku ya Ijumaa na Jumamosi kutakuwa na semina maalum kwa watendaji wa chama hicho wakiwemo viongozi wote wa mikoa










 
kwa nini hili lichama halifi tuu?lijifie mbali tupate mbadala wa kuleta maendeleo
 
Taarifa zisizothibitishwa zinadai EL na Chenge wamevuliwa gamba
 
yale yale hwana uwezo wa kumtoa EL ww hiyo number nyingine na ndie mgombea uris 2015 mtake msitake!!
 
hakuna ubunifu. chama nakilaza pema peponi. bwana ametoa na bwana ametwaa. jina la bwana libalikiwe.
 
wanaanza kwa kukubali then mbele wanakubali heee ghafla wanakataaa wanakanusha yale waliyotuambia jana
 
yale yale hwana uwezo wa kumtoa EL ww hiyo number nyingine na ndie mgombea uris 2015 mtake msitake!!

Tunaweza tusimzuie kuwa mgombea lakini tuna uwezo wa kumzuia kushinda uchaguzi. Focus yetu ni hili la pili!
 
wanaanza kwa kukubali then mbele wanakubali heee ghafla wanakataaa wanakanusha yale waliyotuambia jana
........wameuona moto wake, wamepima upepo, moto wa Lowassa unachoma, tena unachoma kweli kweli . shelukindo Bite upoooooo? umuunge mkono Lowassa ili tupime integrity yako kwake kwa lolote atakalosibuliwa nalo, najua wewe ni mojawapo wa waumini wake
 
Sasa hapa kinacho umiza kichani nini?
  • M/kiti kufungua kika o na kusema kila mtu awe huru
  • wajumbe 31 kuhudhuria badala ya 38
kimsingi sijaona cha ajabi hapa JIPANGE UPYA mkuu
 
Back
Top Bottom