Uchaguzi 2020 Kamati Kuu CCM kuteua wagombea watatu (03) ambao watapigiwa kura wajumbe wa jimbo husika

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,819
11,509
Nimeona mchakato wa kuwapata wagombea ubunge ndani ya CCM kwa mwaka huu itakuwa tofauti, ambapo kamati kuu itateua wagombea watatu (03)ambao watapigiwa kura wajumbe wa jimbo husika.

Inakuaje kamati kuu iteue baadala ya kuwaachia wajumbe ambao wao ndio wanawajua wagombea wao.

Hakuna harufu ya uteuzi wa wapendwa wa mwenye Chama?
 
Kwani siku hizi kuna Chama hapo au kuna familia ya MTU?
Mwalimu aliko labda analia machozi, Mkapa na JK wanatoa macho hawaamini kinacho endelea.
Maana haiwezekani juhudi zote zile za kukipigania chama zimeishia kuwa mfukoni kwa MTU ambaye hajawahi kukipigania hata TANU youth league au UVCCM haijui
 
Mimi nafikiri watia nia wanachama ,kwanza wanachukuwa form,baada ya kutimiza masharti wanarudisha form.
Hayo majina ya watia nia yanayopelekwa ngazi ya juu,ambapo yanachujwa na kubakiza majina matatu.
Hayo majina matatu ndio yanapigiwa kura kumpata mmoja.
 
Mimi nafikiri watia nia wanachama kwanza wanachakuwa form,baada ya kutimiza masharti wanarudisha form.
Hayo majina ya watia nia yanayopelekwa ngazi ya juu,ambapo yanachujwa na kubakiza majina matatu.
Hayo majina matatu ndio yanapigiwa Kira kumpata mmoja.
Kwanini wachujwe kamati kuu baadala ya kupigiwa kura za maoni.
 
Kwanini kamati iteue? Kwanini ambao wamechukua fomu wasiachwe wachuane huko majimboni.
Nadhani kunakuwa na watu wameapply,tuseme watu 20,then kamati kuu ndo wanachambua na kupata majina 3,ambayo ndo yanarudi kupigiwa kura ngazi ya jimboni,,kuliko majina yatoke chini matatu halafu kamati kuu ichague jina moja,,
Utaratibu mzuri tu
 
Nadhani kunakuwa na watu wameapply,tuseme watu 20,then kamati kuu ndo wanachambua na kupata majina 3,ambayo ndo yanarudi kupigiwa kura ngazi ya jimboni,,kuliko majina yatoke chini matatu halafu kamati kuu ichague jina moja,,
Utaratibu mzuri tu
Kamati kuu inawajuaje wagombea wa majimboni, kwanini wajumbe wasiachwe wachague wenyewe.
 
Hao mamluki wachumia tumbo waroho wa madaraka, wasaliti, walionunuliwa kwa rushwa za mabilioni waliohamia kwenye CCM ndio watakaopendelewa na hiyo kamati. Ukweli hao watu majimboni hawatakiwi na wanachama asili wenye upendo na uchungu wa chama.

Mwisho wa siku JPM ataacha chama katika hali mbaya kwa atakayempokea kijiti, kwani hao watu ni kama mla nyama ya binadamu. Watahama tena kufuata maslahi
Mimi bado nipo kwa hawa wenzangu wahamiaji hatma yao upone? Maana kura za maoni sidhani kuna hata mmoja anaweza penya walau kwa top ten.
 
Back
Top Bottom