Kamati Kuu CCM kukutana kujadili Rasimu ya Katiba

Na bado watakaa tuu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kinana amekosea wapi? Huu ni ugumu wa uelewa wa lugha tu, mtu akisema haiungi asilimia mia moja maana yake kuna asilimia fulani ina mapungufu.

Tume imeleta rasmu ili tuijadili tuondo hayo madoa ya upungufu unayoifanya isiwe isiiungwe asilimia mia moja.

Nahata tume ikijifungia miaka kadha haiwezi kuleta katiba iliyo bora asilimia 100.
 
Bora habari hii imeandikwa na mtanzania ingeandikwa na tanzania daima vijana wa lumumba wangekuja na yao,lakini wafanye yote wakichakachua watanzania tutakuwa tumeshamjua adui yetu kwa sababu tume imemaliza kazi vizuri na kazi waliyoifanya tumeiona.sasa ccm ingieni kwenye mtego tuwape mambo.
 
Ninasubiri kwa hamu kubwa kuwasikia waliosema kwa sauti kubwa nahadharani kabisa kuwa Tume ya Mabadiliko ya katiba nchini haina watu wenye weledi kwa kazi hiyo tena wakaenda mbali kuwa haiko huru tume hiyo kufanya kazi wanayotakiwa kufanya. Sasa baada ya rasimu hii natamani kuwasikia tena wakisema nakurudia maneno yale na pengine kwa kuyapigia mstari mkubwa!!
Huyu jamaa huwa anakurupuka bila kuelewa anachosema nafikiri siku anaanzisha thread hii hata rasimu yenyewe alikuwa hajaisoma vizuri, nasubiri nione nini Nape Nnauye atachangia kwenye CC.
 
Last edited by a moderator:
Lakini Chama cha Wananchi (CUF) nacho hakiko nyuma, kwani Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba amekwisha tangaza nia ya kugombea urais kwa mara ya nne mwaka 2015.

Mtanzania[/QUOTE]

Ni mara ya tano siyo ya nne, 1995,2000,2005,2010 na sasa 2015
 
CCM wanataka Katiba kwa faida yao peke yao ili waendelee kubaki madarakani tu? Ina maana huyu Kinana moja anaposema hiyo Rasimu chama chao hakiungi mkono kwa 100% hakuna hata mazuri machache?

Hayo mapovu yote wanayoyapinga ina maana ni kuhofu kwamba huenda wakaondoka madarakani wakati wamezoea maisha ya madaraka tangu walipokuwa wadogo hadi watakapokufa? Kwa kauli ya Kinana inatia mashaka sana na ha sa ukizingatia kwamba wajumbe wa Mabaraza ya katiba 100% wamejaa mburula wa ccm, hivyo kauli ya ccm itakayotoka ndiyo itakayofanyiwa kazi na Mabaraza ya Katiba Nchi nzima.

Wadau hapa nadhani ndipo pia Jaji Mstaafu Warioba atakapojidharau kwani Chadema na wadau wengine walionya sana kuhusiana na Mabaraza haya ya Katiba kwamba ayafumue na Wananchi wachaguane upya akaweka Nta masikioni, sasa madhara yake ni pale itakapoona Rasimu nzima ya Katiba inafumuliwa na hawa maccm waliojaa ndani ya mabaraza ya Wilaya na kupendekeza Rasimu itakayokidhi matakwa ya ccm.

Mapendekezo yangu:

Kwa kauli hii ya Kinana na Msimamo utakaotoka kwenye CC ya ccm wiki ujayo kama walivyo ahidi kuipinga Rasimu hii kwa zaidi ya 100% na kwa kuwa wao ndo chama tawala kwa sasa, mie napendekeza iundwe sheria ya kupata Tume huru ya uchaguzi tu itakayohusisha wajumbe/ wa vyama vyote vyenye uwakilishi kwenye ngazi za Kiserikali, NGOS, madhehebu ya DINI, wawakilishi kutoka Serikalini ila wasiwe Wakurugenzi wa Halmashauri ama Watendaji wa Vijiji/ Kata. Tuingie kwenye Uchaguzi Mkuu 2014/2015 ili kama Watanzania wataamua kubadilisha Serikali basi Serikali hiyo mpya itapewa kazi ya kuratibu mchakato mzima wa kupata Katiba mpya kwa Matakwa ya Watanzania na si vyama na Watawala ambao leo wapo na kesho hawatakuwepo lakini Tanganyika na Zanzibar zitadumu milele.

Hitimisho

Wadau, tukumbuke tangu mwanzo kabisa ccm walitamka mapema sana kuwa katiba mpya si adhima yao na hata kwenye ilani yao ya uchaguzi 2010 - 2015 haikuwemo hivyo walilazimishwa tu!.
 
Mimi naona hili ni jambo jema kwa sababu zifuatazo:

1. Kama CCM haikubaliana na kila kitu asilimia mia ina maana kuwa mchakato ulikua huru. Kuna baadhi ya watu walikua wana lalamika kwamba mchakato umebakwa na CCM sasa hii ni kiashiria tosha kwamba kamati ya katiba mpya ilikua independent.

2. CCM kama vyama vingine vya siasa na kama kundi lolote kwenye jamii ina haki ya kutoa maoni yake. Kwa hiyo sioni neno wao kuitisha kikao kuijadili. Ndio maana nzima ya rasimu (draft).
 
Wadadisi na wafuatiliaji wa mambo walio ndani ya CCM, wanaeleza iwapo muundo wa Serikali tatu za Zanzibar, ya Tanzania Bara na ile ya Jamhuri ya Muungano kama zilizopendekezwa na Tume ya mabadiliko ya Katiba utaridhiwa, CCM kinaweza kuambulia ukuu wa Serikali ya Muungano pekee.
Kwanini CCM isishinde serikali ya Tanganyika hofu yao nini, au wanajua wameshalikoroga.
 
CCM hata wapepese macho vipi ngoma imekamilika ole wao waje na vioja vyao.Kwani walilazimishwa kumteua JAJI WARIOBA na timu yake??? kama walitaka mawazo yao yawemo si wangemteua JAJI TENDWA na akina shimbo wawe wajumbe?? hawakujua kama warioba ni jembe la mjerumani, lile ni jembe hata ukiamua KULIMA juu ya jiwe linapasua.

Wasiomjua jaji warioba wamuulize mzee mkapa alimpa tume ya wara rushwa alichopendekeza mkapa anajua.
JAJI WARIOBA WEWE NI PETRO NA JUU YAKO TANGANYIKA ITAZALIWA NA KUJENGWA UPYA.
 
Sasa watapataje Serikali ya Muungano na huku wakose ya Zanzibar na Tanganyika. Mimi naona CCM wanatoka KAPA maana wanakosa kote
 
Wewe ni wa ajabu hebu soma tena nilipo bold uone ulichoandika, hivi wewe ukipata ulichokitaka hata kwa 80% aibu itatoka wapi tena, au ulikuwa unamaanisha ndivyo sivyo.

Maana ni hiyo hiyo, labda kama wewe una maana yako
 
Hii Rasimu imekuwa kama kaburi la CCM inawafanya wa weweseke kama wameshikwa na degedege

ccm wameshikwa pabaya,Kwanini CC isiombe repoti ya wanachama wao kutoka Wilayani na Mikoani na kuunganisha na kuona wanachama wametoa maoni gani badala ya Kamati ya Kikwete ya watu 15 tu ndio iamulie wanaccm wengine zaidi ya milion tano?.Ni ukosefu wa maadili na utawala bora.
 
Mwanamme mmoja alikuwa akipigwa na mkewe, kila alipopigwa aliyekuwa analia na kutoa sauti kubwa alikuwa mkewe, watu wakifika wanamlaumu mwanamme lakini kumbe aliyekuwa anadhibitiwa kwa kipigo ni mwanamme.

Msiangalie kilio cha Kinana mkaamini kwamba CCM nayo hairidhiki na rasimu ya Katiba, Jamani hii ni BONGO kama wanaua tembo na hawakamatwi, Twiga na urefu wake anakunjwa na kupandishwa ndege na kwenda Qatar, kama kusoma hamjui hata picha nayo tabu,

Akili kichwani kwenu....................
 
[h=2]Kamati Kuu ya CCM itakutana wiki ijayo kujadili Rasimu ya Katiba Mpya[/h] 07/06/2013
0 Comments


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa wiki ijayo kuongoza Kamati Kuu ya chama hicho kujadili Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyozinduliwa hivi karibuni.

Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana alisema msimamo wa chama juu ya rasimu hiyo utajulikana baada ya kikao hicho.
Alisema kwa sasa hawawezi kupinga wala kupongeza mpaka watakapoijadili kwa pamoja.

Alisema hayo wakati akizungumza katika mahojiano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kufanya mazungumzo na wajumbe wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam waliowasili nchini juzi kwa malengo ya kuimarisha uhusiano na CCM.

Kwa mujibu wa Kinana, baada ya kuchambua kifungu kwa kifungu, chama hicho kitatoa msimamo wake. Alisema katika suala hilo siyo vizuri kutoa msimamo bila kushirikishana kwani bahati nzuri chama hicho kina vikao halali vya kujadili masuala mbalimbali.

Kikao hiki cha Kamati Kuu kitafanyika Jumatatu ijayo chini ya Mwenyekiti wake Rais Kikwete kisha kupata msimamo wa chama chetu, alisema Kinana.

Kinana alisema watajadili kwa kuzingatia hali halisi ya sasa kwa taifa la leo na lijalo ili kuweka kuunga mkono rasimu hiyo au kuipinga.​


Source: wavuti.com - Blog
 
ccm wameshikwa pabaya,Kwanini CC isiombe repoti ya wanachama wao kutoka Wilayani na Mikoani na kuunganisha na kuona wanachama wametoa maoni gani badala ya Kamati ya Kikwete ya watu 15 tu ndio iamulie wanaccm wengine zaidi ya milion tano?.Ni ukosefu wa maadili na utawala bora.
kwa katiba hii hakuna mwanachama wa machadema hata mmoja mwenye sifa ya kugombea urais, sana sana wataishia kwenye uenyekiti wa kijiji
 
Rasimu ya katiba mpya inaonekana kuitesa sana Ccm kwa kuhofia ndo mwiba kwao,wameahidi kutoipitisha kwa 100%.nadhan kwa katiba hi endapo vurugu itatokea basi ni ccm watakuwa ndo waanzilishi hakika,wananch tusikubali ccm kutuandalia katiba ya nch yetu,Kamati kuu ya ccm kukaa jumatatu kujadili,mtajiju,
akili yako ina mashaka makubwa ndani yake..angalia watembea na sumu wanavyoweweseka...hapo chini kwenye red ni kundi ambalo chadema hawalipendi kabisa
CHADEMA yajipanga kuikosoa rasimu ya Katiba

na janet josiah
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepanga kutoa tamko kuhusu rasimu ya mabadiliko ya Katiba iliyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba.
Akizungumza na Tanzania Daima jana Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri wa CHADEMA John Mrema alisema kwa sasa viongozi wa juu na watalaamu wanaisoma na kuichambua.
"Hatuwezi kutoa maoni ya juu juu kuhusu rasimu ya katiba… ni kitu nyeti ambacho kinatakiwa kufanyiwa kazi kwanza ili chama kitakapozungumzwa iwe kwa ajili ya manufaa ya Watanzania wote na si ya mtu mmoja ndiyo maana kazi hii tumeikabidhi kwa wataalam," alisema Mrema.
Pamoja na mambo mengi wachambuzi hao watapitia mambo yaliyokubaliwa na yaliyoachwa ili kuionyesha tume hiyo kuwa kuna ambayo yana manufaa kwa taifa ingawa wameyaacha.
Katika rasimu hiyo mambo yaliyoachwa ni pamoja na serikali ya majimbo kwa sababu kuwa gharama za kuiendeshea zitaongezeka endapo serikali tatu zitakuwapo pamoja kuweza kufumuka mambo ya udini, malalamiko, dalili za kujitenga, ukabila na ukanda.
Mambo mengine yaliyokataliwa katika serikali ya muungano ni Mahakama ya Kadhi kwa maelezo kwamba nchi washirika zinaweza kulijadili.
 
angalia unavotokwa povu kwenye meno hadi unajijibu mwenyewe, uvivu wa kufikiri unakuponza...shame sana kwako





  • user-online.png
    mecy

    Today 06:50
    #2
    Senior MemberArray


    Join Date : 16th July 2012
    Location : dar es salam
    Posts : 206
    Rep Power : 388
    Likes Received22
    Likes Given4


    [h=2]
    icon1.png
    [/h]

    quote_icon.png
    By mecy
    Rasimu ya katiba mpya inaonekana kuitesa sana Ccm kwa kuhofia ndo mwiba kwao,wameahidi kutoipitisha kwa 100%.nadhan kwa katiba hi endapo vurugu itatokea basi ni ccm watakuwa ndo waanzilishi hakika,wananch tusikubali ccm kutuandalia katiba ya nch yetu,



    hakika wananch tusikubali kamwe ccm watupangie katiba.​







  • user-online.png
    mecy

    Today 06:54
    #3
    Senior MemberArray


    Join Date : 16th July 2012
    Location : dar es salam
    Posts : 206
    Rep Power : 388
    Likes Received22
    Likes Given4


    [h=2]
    icon1.png
    re: Kamati Kuu CCM kukutana kujadili Rasimu ya Katiba[/h]
    mtajiju ccm.huo ndo mwanzo tu,tunashukuru anguko la ccm sasa tunaliona dhahiri.​




 
ccm ni chama kikubwa lazima kitoe maoni yake kama ambavyo hapa jf tangu ile rasimu imesomwa,hadi leo jukwaa limetawaliwa na maoni ya watu kuhusu mapungufu kadhaa na wengine wakipongeza...mleta mada amebeba nazi yenye uji mzito juu ya mwili wake
 
Back
Top Bottom